FURSA FURSA- UINGEREZA yarudisha viza ya miaka miwili kwa watakaohitumu masomo ya vyuo vikuu nchini humo.

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,396
Wizara ya mambo ya ndani ya Uingereza imeamua kurudisha viza ya miaka miwili kwa wahitimu wa vyuo vikuu nchini humo pindi wamalizapo masomo.

Viza hiyo inawawezesha wahitimu wenye sifa kadha wa kadha kutumia fursa ya miaka hiyo miwili kutafuta waajiri na kuhakikisha wanapata vibali vya kufanya kazi kabla ya viza hiyo haijaisha.

Viza hiyo ambayo hapo awali iliitwa "Tier ! post study Visa" iliondolewa mwezi April mwaka 2012 na kubakia kuitwa Tier 4 Student ambayo inawaruhusu wanafunzi wa kigeni kukaa miezi minne tu baada ya kuhitimu masomo yao.

Hivyo kuanzia mwaka 2020 visa mpya iitwayo "UK post-study work visa for Tier 4 visa" itaanza kutolewa na hivyo kuwapa fursa wahitimu wa shahada za kwanza na zile za uzamili kupata muda mzuri wa kutafuta kazi za kudumu na zingine zenye mishahara minono.

Uamuzi huo umekuja baada ya kushuka kwa kiasi kikubwa cha idadi ya wanafunzi wa kimataifa wanaojiunga na masomo mbalimbali katika vyuo vikuu nchini humo hivyo kusababisha ukosefu mkubwa wa mapato kwa vyuo vikuu.

Wanafunzi wa kimataifa wanachangia kiasi cha pauni bilioni 26 kwa mwaka kwenye mapato ya nchi hiyo.

Serikali ya nchi hiyo inatarajiwa kuwapa nafasi wahitmu wa shahada za maeneo ya hesabu, uhandisi na tekonolojia kupata kazi na hivyo kuboresha soko la ajira, na makampuni mbalimbali ambayo huwa yanatafuta vijana wenye akili katika maeneo hayo.

Namba ya wanafunzi watakaojiunga na vyuo mbalimbali nchini humo inatarajiwa kufikia 600,000 ndani ya miaka 10 ijayo.

Pia utaratibu huo unaondoa masharti ya kuwa kila mhamiaji nchini humo kuwa na kshahara wa kiasi cha pauni 30,000 kabla ya kupewa viza ya kudumu.

Viza hii mpya inatarajiw akutumiwa vilivyo na wahitimu watarajiwa kutafuta kazi yoyote ile ndani ya miaka miwili, na pia kuongeza muda wa viza endapo wanapata kazi hizo na pia kuongeza muda wa mikataba ya kazi endapo watakuwa wana mikataba ya kazi.

Hii ni firsa kwa vijana ambao kwa bahati nzuri wanapata nafasi za masomo nchini Uingereza na bila shaka wamalizapo masomo yao kuanza machakato wa kutafuta kazi zenye mishahara minono.

Nikiwa mmoja wa watanzania ambao nimewahi kuishi na kufanya kazi nchini humo, napenda kuwashawishi vijana wa leo kuchangamkia fursa hiyo adimu.

Hakika ukipata nafasi hiyo hautajuta.

Source: Vyanzo mbalimbali vya kutoka Uingereza.


============================================================================
World news story

UK announces 2-year post-study work visa for international students


The new ‘Graduate’ route will be open to all international students – including those from India – who have valid UK immigration status as a student and have successfully completed a course of study in any subject at undergraduate level or above at an approved UK Higher Education Provider. The visa will allow eligible students to work, or look for work, in any career or position of their choice, for two years after completing their studies.

This builds on UK government action to help recruit and retain the best and brightest global talent, as well as opening up opportunities for future breakthroughs in science, technology and research and other world-leading work that international talent brings to the UK.
Home Secretary Priti Patel said:

The new Graduate Route will mean talented international students, whether in science and maths or technology and engineering, can study in the UK and then gain valuable work experience as they go on to build successful careers.

It demonstrates our global outlook and will ensure that we continue to attract the best and brightest.

Sir Dominic Asquith, British High Commissioner to India, said:

This is fantastic news for Indian students, who will now be able to spend more time in the UK after completing their degree, allowing them to gain further skills and experience.

The UK is home to some of the best higher education institutions in the world and continues to welcome international students. I’m delighted that numbers of Indian students coming to study in the UK are constantly increasing, having doubled over the last three years. Last year alone we saw a massive 42% increase.

This exciting announcement will help ensure that the UK remains one of the best destinations for students across the world.

The UK welcomes genuine students from India and the rest of the world for the positive contribution they make to the UK. Indian student numbers have significantly increased over the last three years, reaching almost 22,000 in the year ending June 2019.

This was a 42% increase on the previous year – and almost 100% higher than three years ago. In addition, 96% of all Indians who apply for a UK visa are successful – meaning the vast majority of those who wish to come to the UK are able to do so.

This announcement follows the creation of a new fast-track visa route for scientists and the removal of the limit on PHD students moving into the skilled work visa route, which collectively aim to cement the UK as a science superpower and a world-leader in the STEM (Science, Technology, Engineering and Mathematics) sector.

Almost half of all Indian students (almost 130,000 since 2008/9) heading to UK in the last ten years chose a STEM subject.
 
Back
Top Bottom