Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 13,227
- 26,048
Baada ya DRC kuingia rasmi EAC , mataifa makubwa katika Jumuiya hii Uganda Kenya na Tanzania,yanaendelea kupambana kukamata fursa ili kushika soko la nchi hii yenye watu zaidi ya Milioni 100
Wakati Uganda akijenga Barabara kuingia majimbo ya kaskazini mwa Congo, Kenya anafungua Ofisi Mombasa Kwa ajili ya Wafanyabiashara wa Congo kuweka kituo chao ili kupitisha mizigo yao kupitia Bandari ya Mombasa na kuingia Congo kupitia Uganda . Kenya pia sasa anafungua viwanda na uwekezaji Congo.
Kwetu Tanzania tumefungua tawi la crdb ili kukamata mitaji ya wakongo na tunajenga Bandari ya Kalema ili kurahisisha mizigo kuingia mashariki mwa Congo kupitia Bandari ya Kalemii iliyopo Tanganyika upande wa Congo.
Zaidi Tanzania pia kupitia Wizara ya Kilimo na Bandari tumefungua Ofisi Congo kurahisisha usafirishaji wa Mazao na Mizigo bila kusahau SGR nyingine ambayo itafika Congo kupitia Kigoma- Burundi.
Sasa Congo nao wanaifanyia maboresho makubwa bandari yao ya kalemii ili kuendana na kasi hizi za maendeleo na tangu mwaka jana mchina ameshasaini mkataba kuanza ujenzi
Ili kukamata vizuri soko la Congo hasa Kwa upande wa mashariki na kusini, hatuna budi Tanzania tuanze kufanya haya;
1. Tujenge kwa Kiwango cha rami na zege, Barabara kutoka Tanganyika hadi bandari ya Kalemi kwa Mkoa wa katavi
2. Tuboreshe na kujenga reli kwa Kiwango cha kisasa kutoka Mpanda hadi Bandari ya Kalemi
3. Tuboreshe Tazara Kwa Kiwango cha SGR mpaka Zambia na tushirikiane na Zambia kuiboresha pia reli kutoka Zambia hadi Lubumbashi, kusini mwa DRC kwa Kiwango cha SGR hata Kwa kukopa
4. Tuite sekta binafsi wajenge meli kubwa za mizigo za kisasa katika Ziwa Tanganyika. Kama hata Kwa ubia na Serikali ni sawa tu
5. Tuboreshe kwa kiwango cha kisasa barabara kutoka Mbeya hadi Songwe kwa Kiwango cha kuhimili mizigo mikubwa Hasa malori . Barabara hii itanuliwe hadi njia nne ili kuwe na njia 1 Kwa ajiri ya Malori tu hadi mpaka wa Tunduma.
Muwe na jumapili njema
Kutoka Manyara
Lord Denning