Furahia kila pumzi ya uhai wako na mshukuru Mungu kwa mambo yote yanayokufurahisha na yale yasiyokufurahisha yapishe kuepuka magonjwa yasiyoambukiza

mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
19,738
35,155
Nilikua napitia report ya afya nimesikitika kuona 34% ya vifo nchini hutokana magonjwa yasiyoambukiza na ugonjwa wa moyo ukiongoza. Magonjwa mengine sukari na cancer ambayo tunayaona yanavyozidi kutuvamia kwa kasi. Kwa tafakari ndogo maisha tunayoishi yamechangia hili kwa kiasi kikubwa.... Ifike mahali sisi wenyewe tusimame na kukataa maisha yanayotupelekea kwenye haya magonjwa hatarishi.

Turudi na kuangalia kile tunachokula na kunywa, na tuangalie shughuli zetu za kila siku kama vina mchango wowote kwenye kuimaraisha au kubomoa afya zetu.

Na katika maisha yale yanayotufurahisha basi yatupatie motisha wa kuendelea kuyafanya katika ubora zaidi na yale yanayotuumiza yatufundishe kwamba tunaweza kujibidisha sana lakini bado tukashindwa kuwa kila kitu tunachotaka au na hiyo isitunyime furaha

Kwa wale waamini wa uwepo wa Mungu basi tujifunze kumtanguliza kwa kila jambo; na tujifunze kumshukuru yeye kwa kila jambo... liwe lile tulilotaka au liwe kinyume chake tumshukuru kwani yeye anatuwazia mema kuliko tunayoyajua sisi.

Hata upate mafanikio unayoyaona kuwa madogo kiasi gani kumbuka zawadi uhai uliyopewa bure... Kumbuka uhai ulio nao ni nafasi nyingine kubwa aliyokupa Mungu ili kuweza kutimiza kile ulichomuomba na alichokutuma kufanya katika dunia hii

Kwa wale waumini wa Mungu na hata wale tusiokua waumini wa Mungu tufanye kazi kwa bidii na maarifa, tujifunze kuyaangalia maisha yetu kama zawadi kwa dunia hii, tujipende na kuwapenda wenzetu.
Tufurahie mafanikio yetu; na Tujifunze kukubali ukweli pale mambo yanavyoenda tusivyotaka sisi, hii itatusaidia sana kufanya maamuzi sahihi na kuendelea kuyafurahia maisha yetu hapa duniani




Cc Extrovert Wangari Maathai Rebeca 83 Saint Anne mrangi
 
Umeandika jambo jema sana swaiba.

Ila cha kusikitisha ni kwamba asilimia kubwa ya wanaoishi kama ulivyoandika ndio wanaoshambuliwa na hayo magonjwa.
 
Huku afrika unaweza ukafata kanuni za ulaji wa chakula bora na afya

halafu mlevi mmoja akakugonga na gari lake kisha unakufwaa
halafu kwenye msiba wako wakapika kuku wa kisasa na wakanywa bia
 
Watoto wanaozaliwa na magonjwa ya moyo wanaongezeka kwa kasi sana, na wamama wanaofariki katika uzazi kwa visababishi hivyo ni wengi pia.

Tufike mahala tuukubali ukweli kwamba ili mtoto apatikane kuwe na makubaliano ya mwanaume na mwanamke...

Wanaume mkisaidia kulisimamia hili tunaweza pungunguza kwa wamama na hata yale madhara yanayoenda kwa watoto

Maandalizi ya afya bora ya mtoto kwa asilimia kubwa yanatokana na maandalizi na matunzo bora kwa mama anapokua mjamzito

Wanaume msifurahie tuu kuchukua na kuweka waaaa halafu siku mbili unaambiwa mimba unaishia mitini
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom