Furaha ya viongozi wa Dunia baada ya Trump baadhi ya wanaJf pia walilia!

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,991
17,888
Furaha ya viongozi wa Dunia baada ya Trump baadhi ya wanaJf pia walilia!

Furaha ya viongozi wa dunia kufuatia kubwagwa Trump, nembo ya kufeli Washington kimataifa

Nov 09, 2020 05:54 UTC

Baada ya vyombo vya habari kutangaza kubwabwa rais wa Marekani, Donald Trump katika uchaguzi wa Jumanne, Novemba 3, 2020 na kushinda Joe Biden katika uchaguzi huo, viongozi wa nchi mbalimbali duniani wamelipokea kwa furaha suala hilo ijapokuwa Donald Trump bado anang'ang'ania madai yake kuwa yeye ndiye aliyeshinda kiti cha urais wa Marekani.

Hasahasa viongozi wa ngazi za juu wa nchi za Ulaya, iwe wa Umoja wa Ulaya au wa nchi za bara hilo, mmoja baada ya mwingine wameonesha kufurahishwa kubwagwa Trump na kushinda Joe Biden wa chama cha Democratic katika uchaguzi wa Marekani. Haiko Maas, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani amempongeza Joe Biden kwa kushinda urais huko Marekani na kumlaumu Donald Trump wa chama cha Republican akisema: Siasa na vitendo vya rais wa hivi sasa wa Marekani vimetusababishia matatizo mengi. Trump anaelewa kwamba wakati wa kuondoka madarakani umefika.

Joe Biden, rais mteule wa Marekani
Kilichogusiwa na kiongozi huo wa ngazi za juu wa Ujerumani katika matamshi yake hayo ni majakamoyo makubwa yaliyosababishwa na Donald Trump katika ulimwengu mzima kutokana na siasa zake za kuchukia ushirikiano na wengine na kujikumbizia kila kitu upande wake kwa madai ya Marekani Kwanza. Migogoro hiyo imesababishwa na Marekani katika nyuga tofauti; za kibiashara, kiuchumi, kijeshi, kiusalama na kisiasa.

Trump amekosa heshima hata kwa waitifaki wa jadi wa Marekani. Trump alitoa matamshi ya jeuri na kejeli hata dhidi ya Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel na rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron. Mara kwa mara alikuwa akizilaumu nchi za Ulaya ikiwemo Ujerumani na kutaka zichangie zaidi gharama za Jeshi la Nchi za Magharibi NATO. Trump alipunguza idadi ya wanajeshi wa Marekani nchini Ujerumani kama njia ya kuishinikiza nchi hiyo iipunguzie Marekani gharama za kuendesha jeshi la NATO. Si hayo tu, lakini pia Trump alianzisha vita vya kiuchumi dhidi ya China kwa madai ya kulinda bidhaa za Marekani. Migogoro kati ya Marekani na Russia imeongezeka sana wakati wa urais wa Donald Trump huko White House.

Suala la Mashariki ya Kati na uadui wake wa kuchupa mipaka dhidi ya taifa linalodhulumiwa la Palestina ni jinai nyingine alizofanya Trump katika kipindi cha takriban miaka minne ya uongozi wake. Kujitoa kwenye mikataba ya kimataifa ambayo ni muhimu kwa nchi za Ulaya na nchi nyinginezo, kama mkataba wa hali ya hewa wa Paris, makubaliano ya kimataifa ya nyuklia ya JCPOA, mkataba wa kudhibiti silaha za nyuklia za masafa ya wastani INF, mkataba wa anga za wazi n.k, ni uborongaji mwingine uliofanywa na Trump wakati wa utawala wake huko Marekani. Jinai nyingine kubwa iliyofanywa na Donald Trump ni kuanzisha ugaidi wa kiuchumi, kijeshi na kimatibabu dhidi ya wananchi wa Iran baada ya kuitoa kijeuri Marekani katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA.

Chuki na uadui wa Marekani dhidi ya wananchi wa Iran ni mkubwa kiasi kwamba hata katika kipindi hiki kigumu cha ugonjwa hatari wa COVID-19, ameendelea kuweka vikwazo zaidi dhidi ya kufika aina yoyote ya madawa na vifaa vya tiba vya kukabiliana na ugonjwa huo nchini Iran. Kwa upande wa ndani ya Marekani pia, Donald Trump amefeli vibaya, kuanzia kwenye kukabiliana na ugonjwa hatari wa corona, hadi katika masuala ya kiuchumi na kiusalama. Yote hayo yameifanya Marekani izidi kutengwa kimataifa na izidi kupoteza itibari ndani na nje ya nchi hiyo.

Trump mbele ya viongozi wa Ufaransa na Ujerumani
Tab'an si waitifaki wa Marekani pekee walioonesha kufurahishwa kwao na kubwagwa Donald Trump katika uchaguzi wa Novemba 3, 2020. Viongozi wa China wameonesha hamu yao ya kushirikiana na serikali ijayo ya Marekani katika kupambana na ugonjwa wa COVID-19 na wametangaza nia yao ya kuanza kuuza chanjo ya ugonjwa huo. Rais Nicolas Maduro wa Venezuela ambaye wakati wa urais wa Donald Trump nchi yake imewekewa vikwazo vya kiwango cha juu kabisa na Marekani, amesema Caracas iko tayari kufanya mazungumzo na serikali ijayo ya Marekani. Rais wa zamani wa Bolivia, Evo Morales naye amesema: Nimefurahi kuona Trump fashisti na mbaguzi wa rangi amebwagwa. Tab'an hii haina maana ya kwamba nimefurahishwa na ushindi wa Biden, hapana, bali kilichonifurahisha ni kuangushwa Donald Trump.

Tunapoyazingatia yote hayo tutaona kuwa, si sahihi watu kuwa na matumaini ya kutengenea mambo kwa kuingia madarakani Joe Biden huko Marekani kwani marais wote wanaochukua madaraka nchini humo lengo lao ni kufanikisha malengo ya muda mrefu ya Washington ya kuidhibiti dunia. Mbinu zao zinaweza kutofautiana, kiukubwa na kiudogo, kiukali na kiulaini, kijeshi, kisiasa na kivikwazo, lakini wote lengo lao ni moja, ni kuendesha siasa za kibeberu za Marekani.

My take:Baadhi ya wanaJf walilia hawakutaka Trump ang'olewe japo wengi humu tulifurahi mmoja wa pro trump wa humu tuliyefahamiana naye alinipigia simu akilia kisa eti mbaguzi kaangushwa

4bv58af84591501ku29_1200C675.jpeg
FB_IMG_16047808436173495.jpeg
4bpt73fd267e0319632_800C450.jpeg
1604918317119.jpeg
1604918331298.jpeg
1604918335051.jpeg
1604918335335.jpeg
 
Ina maana Biden atairejesha Marekani kwenye ule mkataba wa nyuklia wa Iran? Au huenda Iran itapata nafuu ya vikwazo?
 
Tump alikua na misimamo yako ambayo ilikua haiwafurahishi wengi... Na hilo wala alikua hajali...



Cc: mahondaw
 
Hivi kweli kuna mijitu ilimuelewa trump???
71 Millions wamempigia kura,halafu bado unauliza swali kama hilo?.Trump ana mapungufu mengi tu ila haina maana eti hana upande anaowavutia watu.Just like every human,tuna upande mbaya na mzuri...
 
Hahaha kwenye msafara wa mambo na kenge wamo eti mtu analia kabisa
Shida ya Trump ilikuwa personality yake nothing else.Msitake kuaminisha watu kwamba Trump alikuwa mbaya kiasi hicho.Amepigiwa kura na 71 millions Americans,tena kura halali.Big number kuliko rais yeyote wa republican aliyepita hata Obama alizozipata 2008 na akiwa anapendwa kweli kweli.
 
Trump hiyuhuyu aachie Nchi???


Ataachia endapo tu states za PVA,NDA,GA, nanyingine anazozituhum, Zitarudia kuhesabu Kura.


Trump ni Rais anayekubalika sana na Jeshi la Marekan.
Ataachia tu ifikapo january,Ila alegations anazo zi rise hazitakiwi kuwa dismissed,wachunguze wapate ukweli wame.Sasa hivi tena wanasema kulikuwa na software glitch kwenye system ya uchaguzi,eti ikawa inampa Joe kura 6,000/.kila inapotokea glitch.sasa wanajiuliza,how hiyo glitch impe favour mtu mmoja tuu???
 
Pumba tupu za mamtu yenye elimu za maajemi
Haaaaa ila mkuu nyie sindo mlisema Trump atauangusha utawala wa Iran?
Mwisho kaanguka yeye kamuacha Ayatollah ana dunda kwa raha zake.
 
Haaaaa ila mkuu nyie sindo mlisema Trump atauangusha utawala wa Iran?
Mwisho kaanguka yeye kamuacha Ayatollah ana dunda kwa raha zake.
Kura ndio zimemuondoa kwa sababu kapoteza majimbo muhimu sana ambayo aliyashinda in a previous election.

Alafu America sio sawa na Sithole Iran, America Rais sio mfalme, America Rais sio Mungu mtu hata gavana anamvimbia kwenye jimbo lake yeye akae na federal yake.

Sasa huko Iran ayatollah ndo Mungu mtu after he says something imeisha embu acha kufananisha U.S na utopolo huo wa jangwani
 
Back
Top Bottom