Furaha ya kuwa/kuishi Tanzania iko wapi?

Mhafidhina

JF-Expert Member
Feb 6, 2008
549
22
Wanajamii,

Kwa kweli mpaka sasa siku zinavozidi kwenda, furaha yangu ya kuwa Mtanzania inazidi kupungua. Nasema hivi kwa sababu nilizonazo.

1. Suala la Umeme: Umeme kwa sasa umekua kama ni bidhaa adimu. KIla siku ni giza, giza na powe rationing, najiuliza ni lini haswa tutakua na umeme wa uhakika na kuachana na matatizo haya...?!

2. Maji: Tumepokea tangazo juzi kutoka DAWASA kwamba sasa maji ni kidogo na sasa maji nayo ni mgao, najiuliza hali kama hii itaisha lini? Hata kuoga siku hizi imekua ni kwa matatizo...! Jamani hali hii itaendelea hivi mpka lini?

3: Miundombinu: Hivi majuzi mvua ilinyesha kidgo tu, hali halisi ya miundombinu ilivoharibika kutokana na mvua hii kwa kweli inasikitisha...! barabara hazipitiki hapo suala la foleni ndio usiseme kabisa kwani nafikiri kila mtu linamgusa...!

4: Wizi, kati ya suala linaloninyima raha ni wizi. Hapa sizungumzii wizi wa kuibiwa na kunyakuliwa vitu kwenye gari, kuvunjiwa nyumba usiku tu, bali nazungumziwa kuibiwa na kuporwa na viongozi ambao wao ndio wanapora mabilioni ya shilingi ambazo ni kodi zetu...!

Kwa kweli kwa sababu hizo chache, Sasa najiuliza furaha ya kuendelea kuwa Mtanzania iko wapi?
 
hakuna raha kwa kweli yani tena inshu ya umeme jamani mpka nimechoka nilidhani ni sie watu wa kaskazini tu ndo tunaonewa hv
 
Hii ungeipeleka kule kwenye hoja mchanganyiko hapa kwenye malavi davi mmmhhhh hapana
 
Mkuu wewe ndio umeliona leo?Mimi nimeliona mapema nikajichepa zangu na kilichoniudhi ni kitendo cha mimi kudai malipo yangu halali ya malimbikizo yaliyokuwa yakifikia kama 2,000,000/=na badala ya kulipwa bila mizenge niliombwa rushwa toka kwa mbeba mafaili mpaka kufikia kwa ofisa anayeidhinisha malipo hayo nikakuta nimebakiwa na 1.5 nikaona ujinga huu ngoja niwaachi linchi lenu.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom