Furaha iliyoje, Tanzania ya matamaniyo yangu imewadia na kuishuhudia!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Furaha iliyoje, Tanzania ya matamaniyo yangu imewadia na kuishuhudia!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Steve Dii, Nov 1, 2010.

 1. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #1
  Nov 1, 2010
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Bila kujali nani atachukua kiti cha urais, bila kujali ni chama kipi kinaongoza nchi, bila kujali kama mimi au wewe tunashikilia kadi za CUF, CCM, Chadema, NCCR, au TLP; leo, Novemba Mosi 2010 Tanzania ya matamaniyo yangu hatimae imewadia.

  Ni ile Tanzania niliyoiwaza na kuiombea iharakishe itufikie. Ni ile Tanzania ambayo wananchi wake wanaendelea kuwa wema, wakarimu na wajasiri. Tanzania yenye amani na mwamko mkubwa wa mabadiliko, haswa nyakati za chaguzi kuu. Jambo ambalo kwa pahala pengi Afrika limekuwa tata na chanzo cha maangamizi ya baadhi ya mataifa.

  Ni ile Tanzania ambayo kiongozi anateuliwa kwa ubora wake na siyo pesa zake, jina lake wala hila zake. Wananchi wanapohabarishwa na kutathmini utendaji wa waliyemchagua wanapatwa na ujasiri, na ari ya kidemokrasia ya kuweza kuendelea kumweka katika uongozi au kumng'oa na kumweka mwingine anayeonekana atawafaa zaidi.

  Tanzania niliyoitamani na kuomba iwadie mapema ni ile ambayo wananchi wake kwa mshikamano wanatambua nguvu waliyo nayo katika kuleta mabadiliko yao wenyewe kupitia kura kwa kung'amua hali waliyonayo na kulinganisha matarajio yao dhidi ya utendaji uliopo. Ni lile Taifa lililojaa wananchi wenye maamuzi kwa ajili ya maendeleo yao na Taifa lao kwa ujumla. Hakika Tanzania hii imewadia na nina imani itaendelea kudumu na kuimarika.

  Ni siku ya furaha kwangu na kwa Watanzania wenzangu, kwani kwa mara ya kwanza kabisa maishani mwangu natarajia kujionea Bunge litakalosimamia maslahi ya wananchi wake likiapishwa.

  Mungu Ibariki Tanzania.

  Steve Dii
   
 2. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #2
  Nov 1, 2010
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,519
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Bado MABINA. Vipi huko Kisesa nani kachukua udiwani?
   
 3. b

  bobsega Member

  #3
  Nov 1, 2010
  Joined: Sep 4, 2007
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kisesa Mabina kashinda udiwani CCM. Roho imeniuma sana
   
Loading...