Funzo lipi hapa?-Hati ya kiapo ya mkapa kuwekwa kando mahakani. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Funzo lipi hapa?-Hati ya kiapo ya mkapa kuwekwa kando mahakani.

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Rutunga M, Jun 2, 2011.

 1. Rutunga M

  Rutunga M JF-Expert Member

  #1
  Jun 2, 2011
  Joined: Mar 16, 2009
  Messages: 1,556
  Likes Received: 230
  Trophy Points: 160
  Kwa wanasheria.Hapa tunapata funzo gani
  Soma hii story chini.

  nimeipata hapa


  Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es salaam, leo imekataa kupokea hati ya kiapo ya rais mstaafu Benjamin Mkapa, yenye maelezo ya ushahidi kwenye kesi ya balozi wa zamani wa tanzania nchini Italia profesa Costa Mahalu, na aliyekuwa meneja utawala na fedha wa ubalozi huo Grace Martin, wanaoshtakiwa kwa uhujumu uchumi ulioisababishia serikali hasara ya shilingi bilioni 2.


  Hakimu anayesikiliza kesi hiyo Elvin Mgeta, amesema mahakama haiko tayari kupokea maelezo hayo ya ushahidi kwa kuwa si muda mwafaka, na ameshauri upande wa utetezi kuwa, maelezo hayo yawasilishwe mara baada ya washtakiwa wenyewe kuanza kujitetea rasmi mahakamani.

  Msimamo wa mahakama hiyo unatokana na maombi ya mawakili wa balozi mahalu ambao walitaka mahakama ipokee hati ya kiapo ya bwana Mkapa, kama sehemu ya ushahidi kwa balozi mahalu.

  Kwa mujibu wa sheria ya marais na katiba ya tanzania,mkuu wa nchi au rais mstafu anaweza kutoa ushahidi,lakini halazimishwi na sheria kufanya hivyo.

  Mbali ya kuiomba mahakama kuipokea hati hiyo ya kiapo,upande wa utetezi pia umeiomba mahakama hiyo kutoa nakala ya hati za mwenendo wa kesi hiyo, kwani nakala ya awali ya mwenendo wa kesi hiyo ina kasoro.

  Kufuatia ombi hilo mahakama imekubali kutoa nakala sahihi ya mwenendo wa kesi hiyo ijumaa wiki hii.

  Kesi hiyo sasa itaanza kuunguruma julai 8 na 11 mwaka huu, kwa balozi Mahalu na mwenzake kuanza kutoa ushahidi wa kujitetea.

  Wanadiplomasia hao ambao wameonekana wana kesi ya kujibu, wanashtakiwa kwa makosa manne likiwemo la kufanya udanganyifu katika ununuzi wa nyumba ya ofisi ya ubalozi mjini Roma Italia.
   
Loading...