Uchaguzi 2020 Funzo kwa CHADEMA: Next time msiandae mikutano yenu sambamba na ya CCM!

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
32,626
2,000
Napenda kuwapa somo dogo ndugu zangu wa CHADEMA kwa kuwa mnaendelea kujifunza siasa.

Kuna msemo wa kiswahili unaoonya kuhusu kumuiga Tembo Kunya....Mtamalizia wenyewe!!

Nimefuatilia mara kadhaa kamati kuu ya CHADEMA hasa katika kipindi hiki baada ya uchaguzi mkuu wa 2015 wakijaribu kupanga mikutano na matamko katika siku au wiki ambazo kamati kuu ya CCM au jumuiya zake muhimu zinapofanya mikutano.

Style hii ni mpya kidogo pengine ni katika juhudi za kuongeza ushindani dhidi ya Chama tawala CCM.Utaratibu huu unaelekea umeletwa na mmoja wa makapi kutoka CCM anayejaribu kuifanya Chadema ionekane kama Chama kinachoongoza dola CCM.

Sio mbaya kuiga mambo mengi na mazuri kutoka CCM kwani CCM ni chama kikongwe na chenye hazina kubwa ya ubunifu.

Hoja yangu ni moja tu siku ya leo..kwamba mnapoona mbinu mliyocopy na kupaste inagoma kuwaletea matokeo tarajali hamna budi mara moja kuachana nayo kwa kuwa bila kufanya hivyo mntaishia kupata aibu na kuwapunguzia morali.

Juma hili kamati kuu ya Chadema imekutana na ilitarajiwa kwa mujibu wa wanapropaganda wa Chadema mitandaoni kuja na maazimio au matamko mazito kama ilivyo desturi yao ya kututia kamba.

Ninachojiuliza ni kimoja tu....je kiherehere cha kupanga mkutano wao sambamba na mikutano kadhaa ya jumuiya za CCM walikitoa wapi?mimi sina jibu ila wanabavicha mnaeeza kunisaidia.

Ni aibu kubwa kwa mara nyingine kamati kuu ya Chadema inajizolea kwa kujaribu kujilinganisha na Chama kubwa CCM katika mazingira ambayo yanaonesha wazi utofauti wa kiwango cha Mbingu na Ardhi kati ya vyama hivi iwe ni kwa coverage,support,agenda na organisation.

Mfano:Mkutano mmoja tu wa jumuiya za CCM yaani mkutano wa UVCCM uliweza kuzima kabisa mjadala wa kikao cha kamati kuu ya Chadema.Hii ni aibu inayohitaji tathmini.

Niendelee kuwaasa ndugu zangu wa CDM kuwa wabunifu na kuja kivingine ili kweli kuonesha kuwa kama wapinzani mna jipya la kuiletea nchi.

Achaneni kupokea mawazo ya makapi ya CCM na mafisadi waliofanya Chadema kuwa chaka lao...watawapotosha.

KWA LEO NI HAYA TU...

HAPA KAZI TU!
 
mcubic

JF-Expert Member
Mar 3, 2011
10,311
2,000
Vipi kuhusu pato la Mtanzania limeongezeka ama limepungua?

Vipi kuhusu umeme.... Ni wa uhakika ama?
 
CHLOVEK

JF-Expert Member
Mar 8, 2017
536
1,000
Napenda kuwapa somo dogo ndugu zangu wa Chadema kwa kuwa mnaendelea kujifunza siasa.

Kuna msemo wa kiswahili unaoonya kuhusu kumuiga Tembo Kunya....Mtamalizia wenyewe!!

Nimefuatilia mara kadhaa kamati kuu ya Chadema hasa katika kipindi hiki baada ya uchaguzi mkuu wa 2015 wakijaribu kupanga mikutano na matamko katika siku au wiki ambazo kamati kuu ya CCM au jumuiya zake muhimu zinapofanya mikutano.

Style hii ni mpya kidogo pengine ni katika juhudi za kuongeza ushindani dhidi ya Chama tawala CCM.Utaratibu huu unaelekea umeletwa na mmoja wa makapi kutoka CCM anayejaribu kuifanya Chadema ionekane kama Chama kinachoongoza dola CCM.

Sio mbaya kuiga mambo mengi na mazuri kutoka CCM kwani CCM ni chama kikongwe na chenye hazina kubwa ya ubunifu.

Hoja yangu ni moja tu siku ya leo..kwamba mnapoona mbinu mliyocopy na kupaste inagoma kuwaletea matokeo tarajali hamna budi mara moja kuachana nayo kwa kuwa bila kufanya hivyo mntaishia kupata aibu na kuwapunguzia morali.

Juma hili kamati kuu ya Chadema imekutana na ilitarajiwa kwa mujibu wa wanapropaganda wa Chadema mitandaoni kuja na maazimio au matamko mazito kama ilivyo desturi yao ya kututia kamba.

Ninachojiuliza ni kimoja tu....je kiherehere cha kupanga mkutano wao sambamba na mikutano kadhaa ya jumuiya za CCM walikitoa wapi?mimi sina jibu ila wanabavicha mnaeeza kunisaidia.

Ni aibu kubwa kwa mara nyingine kamati kuu ya Chadema inajizolea kwa kujaribu kujilinganisha na Chama kubwa CCM katika mazingira ambayo yanaonesha wazi utofauti wa kiwango cha Mbingu na Ardhi kati ya vyama hivi iwe ni kwa coverage,support,agenda na organisation.

Mfano:Mkutano mmoja tu wa jumuiya za CCM yaani mkutano wa UVCCM uliweza kuzima kabisa mjadala wa kikao cha kamati kuu ya Chadema.Hii ni aibu inayohitaji tathmini.

Niendelee kuwaasa ndugu zangu wa CDM kuwa wabunifu na kuja kivingine ili kweli kuonesha kuwa kama wapinzani mna jipya la kuiletea nchi.

Achaneni kupokea mawazo ya makapi ya CCM na mafisadi waliofanya Chadema kuwa chaka lao...watawapotosha.

KWA LEO NI HAYA TU...

HAPA KAZI TU!
Tangu Machali aseme siasa zimehamia mtandaoni basi kila mwana lumumba ana ID zisizopungua 20 hivi, wewe ni mfano halisi.
 
samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
7,814
2,000
vipi darasa moja la shule zetu za msingi linabeba wanafunzi wangapi?
vipi mwalimu mmoja anahudumia wanafunzi wangapi?
vipi daktari mmoja anahudumia wagonjwa wangapi?
vipi vifo vya mama na mtoto vimepungua kwa asilimia ngapi?
vipi tatizo la umeme Tanzania limeisha?
Vipi barabara zetu zote tumeshaweka rami na taa?
Vipi pato la Mtanzania kwa siku limeongezeka?
Vipi wahitimu wote wenye sifa za kwenda chuo kikuu na uhitaji wa mikopo wanapata mikopo?
Vipi watanzania wote wanapata huduma ya maji safi na salama?
Vipi export zimeongezeka?
Vipi mzunguko wa hela mtaani umeongezeka?
Vipi Uzarishaji umeongezeka na mishahara kupanda?

NI VYEMA CCM IKAJIKITA KUTATUA MATATIZO AMBAYO IMESHINDWA KUYATATUA KWA KIASI KIKUBWA TOKA TAIFA LIMEPATA UHURU. MAANA YAKUONGOZA DOLA NI KUTATUA MATATIZO YANAYOLIKABILI TAIFA HUSIKA NA SIO KUJIKITA KUPAMBANA NA VYAMA MBADALA..
 
jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
32,626
2,000
Mkuu hiyo unayoona ni 6 kw wenzako ni 9. Inategemea umesimama wapi.
Wataalamu wa neuroanatomy hawaamini katika hiyo theory yako...sita ni sita hata ipinduliwe vipi haiwezi kuwa tisa.hata ukiisoma huku ukiwa kichwa chini miguu juu.
Ni nani asiyejua mlivyohangaika kujaribu kuipaiza habari ya mkutano wenu bila mafanikio?
 
samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
7,814
2,000
Huku mtandaoni hampambani na chadema hapana ila mnapambana na watanzania wanaohitaji maendeleo kama matokeo ya wao kulipa kodi na kutumia nguvu zao..
 
jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
32,626
2,000
Tangu Machali aseme siasa zimehamia mtandaoni basi kila mwana lumumba ana ID zisizopungua 20 hivi, wewe ni mfano halisi.
Hivi wana CCM mtandaoni walikuwapo kuanzia Machali aseme???
Kumbuka JK ,Samia na JPM kwa nyakati tofauti walivyotambua kazi ya wanaCCM mtandaoni.

Kwa kuwa hoja za mwanaCCM mmoja zinasimamisha makarai ya zege kama 1000 ni lazima umuone Jingalao kama nina ID nyingi.
Acheni woga!!
 
jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
32,626
2,000
Vipi kuhusu pato la Mtanzania limeongezeka ama limepungua?

Vipi kuhusu umeme.... Ni wa uhakika ama?
Ziko threads husika katika hayo...na tumeyatolea majibu.by the way kilo ya korosho ni 4000 kule kusini kutoka 1000 mwaka 2015.sasa utajaza mwenyewe kama pato la mkulima(75% ya watanzania) limepanda au la?
Ila nikiri kuwa pato la mtanzania fisadi limeporomoka kwa kasi ya ajabu sana.
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
37,412
2,000
Wataalamu wa neuroanatomy hawaamini katika hiyo theory yako...sita ni sita hata ipinduliwe vipi haiwezi kuwa tisa.hata ukiisoma huku ukiwa kichwa chini miguu juu.
Ni nani asiyejua mlivyohangaika kujaribu kuipaiza habari ya mkutano wenu bila mafanikio?

Unapimaje mafanikio? Au unatumia kipimo cha kiccm kujua mafanikio. Wananchi wamepata ujumbe wa cdm na wale wanaukubali upinzani na kupuuza siasa za kishenzi hawatashiriki uchaguzi wowote unaoandaliwa na tume ya wahuni chini ya mwenyekiti wa ccm.
 
samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
7,814
2,000
Ni vizuri tukajikita kuipa pressure serikali ifanye kazi yake ambayo ilishindwa kufanya toka 1961 na kuwaondolea watanzania kero nyingi zinazowasumbua...

Watanzania wana kero nyingi sana ambazo mwisho wa siku zinaendelea kuwafanya wawe masikini na kufa kwa maradhi, ni vyema tukapambana na watawala kwa nguvu zetu ili watatue kero na si kupiga makofi kila kukicha huku bado taifa lingali masikini na watu wake wengi wanaishi kwenye umasikini na uprimitive uliopitiliza kutoka na madhara ya wengi wao kukosa elimu sahihi na wengine kuikosa kabisa..
 
jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
32,626
2,000
vipi darasa moja la shule zetu za msingi linabeba wanafunzi wangapi?
vipi mwalimu mmoja anahudumia wanafunzi wangapi?
vipi daktari mmoja anahudumia wagonjwa wangapi?
vipi vifo vya mama na mtoto vimepungua kwa asilimia ngapi?
vipi tatizo la umeme Tanzania limeisha?
Vipi barabara zetu zote tumeshaweka rami na taa?
Vipi pato la Mtanzania kwa siku limeongezeka?
Vipi wahitimu wote wenye sifa za kwenda chuo kikuu na uhitaji wa mikopo wanapata mikopo?
Vipi watanzania wote wanapata huduma ya maji safi na salama?
Vipi export zimeongezeka?
Vipi mzunguko wa hela mtaani umeongezeka?
Vipi Uzarishaji umeongezeka na mishahara kupanda?

NI VYEMA CCM IKAJIKITA KUTATUA MATATIZO AMBAYO IMESHINDWA KUYATATUA KWA KIASI KIKUBWA TOKA TAIFA LIMEPATA UHURU. MAANA YAKUONGOZA DOLA NI KUTATUA MATATIZO YANAYOLIKABILI TAIFA HUSIKA NA SIO KUJIKITA KUPAMBANA NA VYAMA MBADALA..
Jifunze kuzingatia matumizi ya "r" na "l" kwanza.
Pili kaisome ilani ya CCM 2015 na ushuhudie yaliyoahidiwa na jinsi yanavyofanyiwa kazi.

Thread hii inahusu Kisa cha aibu kilichowakumba Chadema.Rudi kwenye hoja.
 
kabombe

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
25,578
2,000
Hii ni ujumbe kwenu mliozoea siasa za usanii
Chadema hawajawahi kuwa serious wao ni.maigizo mpaka wanawachosha bendera fuata upepo
Huwezi kutoa tamko la kususia uchaguzi ukiwa.na saini ya Hashi Rungwe,wa Chauma,walifanya lini kikao cha kususia uchaguzi au Nld walikaa lini
Nasikia jamaa walikua wanataka wakatiwe kwanza ili walipe uzito tamko.koko
 
Mulhat Mpunga

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
27,344
2,000
vipi darasa moja la shule zetu za msingi linabeba wanafunzi wangapi?
vipi mwalimu mmoja anahudumia wanafunzi wangapi?
vipi daktari mmoja anahudumia wagonjwa wangapi?
vipi vifo vya mama na mtoto vimepungua kwa asilimia ngapi?
vipi tatizo la umeme Tanzania limeisha?
Vipi barabara zetu zote tumeshaweka rami na taa?
Vipi pato la Mtanzania kwa siku limeongezeka?
Vipi wahitimu wote wenye sifa za kwenda chuo kikuu na uhitaji wa mikopo wanapata mikopo?
Vipi watanzania wote wanapata huduma ya maji safi na salama?
Vipi export zimeongezeka?
Vipi mzunguko wa hela mtaani umeongezeka?
Vipi Uzarishaji umeongezeka na mishahara kupanda?

NI VYEMA CCM IKAJIKITA KUTATUA MATATIZO AMBAYO IMESHINDWA KUYATATUA KWA KIASI KIKUBWA TOKA TAIFA LIMEPATA UHURU. MAANA YAKUONGOZA DOLA NI KUTATUA MATATIZO YANAYOLIKABILI TAIFA HUSIKA NA SIO KUJIKITA KUPAMBANA NA VYAMA MBADALA..
mambo mi hili li id lake linanifanya hata nisimjibu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom