Funzo kutoka kwa Mbowe kwa kupigania uhai wa Mh.Tundu Lissu

Kinaeleweka

Senior Member
Nov 10, 2014
145
104
Ndugu zanguni wapenda amani,maendeleo,uzalendo na haki ni ukweli usiofichika kuwa Mungu ndio mtetezi wa maisha yetu na ndiye mwenye kupanga hatima ya maisha yetu.

Mie ni mmojawapo wa Watanzania wengi tuliopokea kwa huzuni kubwa taarifa ya kupigwa risasi Mh.Tundu Lissu(Mb na rais wa TLS) mjini Dododma akitokea bungeni na nilizidi kumwomba Mungu azidi kumfanyia uponyaji wa matibabu yake.

Katika kufuatilia hatua zilizochukuliwa na watu mbalimbali ikiwemo serikali kuharakisha matibabu ya majeruhi Lissu,hapa ndipo ninapoona kuna kitu cha kujifunza kutoka kwa Kamanda Mbowe na timu yake kuendelea kupigania uhai wa Mh.Tundu Lissu kutokana na sababu zifuatazo:

1. Kwanza kuhakikisha usalama wa Majeruhi Lissu
Kwa kuwa watu waliotaka kumuua mhe.Lissu hawajulikani,licha ya jaribio hilo kufanya mchana kweupe tena sehemu yenye ulinzi wa kutosha ni busara kubwa sana na ya haraka ilitumika katika kufanya maamuzi sahihi ni wapi majeruhi Lissu apelekwe kwa matibabu.Lakini pia kuhakikisha usalama wa kutosha upo pia sehemu anapopata matibabu licha ya kutofautiana na Spika wa Bunge na Waziri wa Afya waliokuwa wanasisitiza urasimu(Bureaucracy) ifuatwe

2. Hamasa ya michango kwa ajili ya Majeruhi Lissu.
Ni uzalendo na upendo wa hali ya juu umeonyeshwa na Mh.Mbowe na makamanda wengine katika kuhamasisha michango ya matibabu ya majeruhi Lissu kutoka kwa wadau mbalimbali ndani na nje ya nchi. Upendo na mshikamano ulioonyeshwa ni mkubwa sana.

3.Kuongea bila woga kuvishutumu vyombo vyetu ya ulinzi na usalama kukosa dhamira ya
kufuatilia na kuwakamata wahusika(Wasiojulikana) waliodhamiria kutaka kuuondoa uhai wa
Mh.Lissu.
Kwa sintofahamu nyingi juu ya matukio ya utekaji,kupigwa risasi na kutishiana bastola,ni
hakika Tanzania si sehemu salama tena na ni lazima kila mmoja kwa nafasi yake apaze sauti
na kukemee vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kwa kutochukua hatua madhubuti kudhibiti
matukio kama hayo.

Nafikiri nimeeleweka na sijatoa kutetea upande wowote ila muda wote ukweli ni lazima usemwe .

Nawakilisha
 
Tulikuwa tunayasikiaga haya mambo nchi za Rwanda,Burundi, Kenya, Uganda, Somalia, Congo, sasa na sisi tumeingia kwenye vita, kuwa mwanasiasa mpinzani tayari unakuwa kwenye risk!! I want my Tanzania back, a country of late Mwalimu.
 
Back
Top Bottom