Fununu: Mabadiliko Jumatano ya Baraza la Mawaziri

tatizo langu kubwa ni kuwa kama atakubali kufanya mabadiliko wakati huu atakuwa ameonesha udhaifu mwingine kama kiongozi, ule wa kutabirika!

Mwanakijiji nani amekutuma umtete..hakuna cha udhaifu wala nini?safari imefika kwa kina Mramba na Mungai kuachi ngazi??Baraza la Mawaziri linabadilishwa Desemba,na niko Lindi hapa..nitajitahidi kumchokonoa Muungwana kwa swali la kizushi,lini tutegemee Timu mpya?stay tuned..
Nina ujasiri kwa hili,si alisema wakina Mwanri atawapangia kazi nyingine?
 
Wana jf nimepata fununu kutoka kwenye vyombo vyangu vya habari nimepata tetesi kuwa huenda mabadiliko ya cabinet yakawa jumatano ya wiki ianzayo kesho,kisha nikaendelea kudadisi nikaja kupata tetesi kuwa mabadiliko hayo yatawakumba wengi ikiwemo mawaziri waandamizi,na katika kutafuta habari hapa na pale nikaja kupata TETESI akuwa huenda hawa wafuatao wanaweza kupumzika kwa sasa,(kumbuka ni tetesi)

Hizi kweli ni fununu...mazee hivyo vyako vya habari kuwa navyo makini...angalia vije kukuambia OSAMA ateuliwa kuwa balozi wa papa Pakistan....
 
Mwana Siasa,
Katika yote uliyosema hujakosea wala kijikanyaga. Yana ukweli wa 100% kama maandishi hayatabadilishwa. Jaka Mwambi anatinga Uwaziri kama mshkaji wa Mkuu wa Kaya toka old schools and college. Hata pale ikulu Dom baada ya Uchaguzi alinitonya hilo.

Kubwa nalotaka kuwatonya; ni kuwa katika mabadiliko haya. Waziri Mkuu atapunguziwa Wizara zilizokuwa chini yake kama TAMISEMI kutokana na Kutumia. Hii ni kumpunguzia kasi na uwezo wa kujijenga kisiasa. Maana tetesi ni kuwa W/Mkuu anatishia kutomsubirisha JK 2010. Tetesi hii imepata nguvu baada ya W/Mkuu kuzidiana kura chache sana na Mkuu wa Kaya NEC. Pia Membe atarudishwa mafichoni maana naye hawaangaliani uso kwa uso na Mzee kama ilivyokuwa zamani. Ikumbukwe Membe hakupiga kampeni kuwania NEC lakini kapuni unajua ziliingia ngapi za ndiyo.

Mkuu wa Kaya amepewa maelekezo kuanza kumwingiza Mtu makini, msafi wa ndani na nje, asiye na waa wala doa Balozi Charles Sanga katika siasa. Chama kinaona huyu mtu na Membe ndiyo pekee waweza kunena mema kwa Wadanganyika na kutenda wanalosema kwa kusimamia umma.
 
Tetesi mwishowe zikaishia kitetesi. Hata tarehe tulitajiwa. Tuiteje, unabii wa uongo? Hongera kaka JK kwa kukataa kuendeshewa serikali yako kwa mtindo wa tetesi, huu ndio msimamo unaotakiwa.
 
Back
Top Bottom