Fununu: Mabadiliko Jumatano ya Baraza la Mawaziri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fununu: Mabadiliko Jumatano ya Baraza la Mawaziri

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mwana siasa, Nov 11, 2007.

 1. m

  mwana siasa Senior Member

  #1
  Nov 11, 2007
  Joined: Aug 28, 2007
  Messages: 119
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35

  Wana jf nimepata fununu kutoka kwenye vyombo vyangu vya habari nimepata tetesi kuwa huenda mabadiliko ya cabinet yakawa jumatano ya wiki ianzayo kesho,kisha nikaendelea kudadisi nikaja kupata tetesi kuwa mabadiliko hayo yatawakumba wengi ikiwemo mawaziri waandamizi,na katika kutafuta habari hapa na pale nikaja kupata TETESI akuwa huenda hawa wafuatao wanaweza kupumzika kwa sasa,(kumbuka ni tetesi);
  1-Capt john chiligati-ni kwa sababu ana majukumu mengine makubwa ndani ya chama so itakuwa vigumu kufanya mambo mengi kwa mpigo
  2-joseph mungai
  3-prof juma kapuya
  4-magufuli
  5-dr Nchimbi
  6-masha
  7-dr mathayo
  8 ngeleja
  9-hawa ghasia
  10-prof mwandosya
  11-prof mssola
  12-mramba

  pia katika pita pita yangu ya hapa nakule nimeweza kupata tetesi kuwa wafiatao HUENDA wakawa ndani,
  1-aggrey mwanri
  2-jaka mwambi
  3-harrison mwakyembe
  4-makamba(inasemekana kwa yeye kupitishwa tena ukatibu ilikuwa si pendekezo na pia habari ya kutolewa ukatibu ilikuwa imezagaa mno) la wakubwa,so kitakachotokea huenda akaachia ngazi ya ukatibu ili nae aingie barazani
  5-rostam azizi
  6-na pia katika nafasi ya mpendwa wetu marehemu salome mbatia(rip)inasemekana nafasi yake inaweza ikachukuliwa na wafuatao;
  tatu ntimizi
  frolence kyendesya
  mama shelukindo
  jenista mhagama

  hizi ndo tetesi nilizoweza kupata,kama kuna mwengine ana lolote basi jamvi liko wazi
   
 2. M

  Mtu JF-Expert Member

  #2
  Nov 11, 2007
  Joined: Feb 10, 2007
  Messages: 472
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hakutakuwa na jipya zaidi ya kuendelea kuiba na kunenepesha vitambi vyao.nafasi ya marehemu mabtia lazima ishikwe na mwanamke tena?
  Vitu vingine vinalazimishwa tu ati lazima wanawake wawepo hata kama hawana uwezo wa kuongoza.
   
 3. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #3
  Nov 12, 2007
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  MTU: Kwa mazoea wizara ya maendeleo ya Jamii, wanawake jinsia na watoto huongozwa na wanawake kwa sababu hilo ndio eneo lao la kujidai
   
 4. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #4
  Nov 12, 2007
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Hizi tetesi kweli!

  Ila kama zitakuwa kweli basi kioja kingine? Makamba waziri?? na RA hakika itakuwa serikali ya kishikaji haswaaaaaaaa!

  Katika yote mbona sioni jina la Kara..???

  Bora zibaki kuwa tetesi! Kwani ni vigumu aondoke Ngeleja abaki kara...
   
 5. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #5
  Nov 12, 2007
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Umeanza vizuri kwa kusema hizo ni tetesi, je tetesi zako zinasemaje kuhusu sababu za cabinet reshuffle?
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Nov 12, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  JK bado ana nafasi mbili za Ubunge wa Kuteua.. natumaini atafanya hivyo muda si mrefu na mmoja wao/au wote wawili wanaweza kuingia as full minister. So, nani yuko CCM lakini si Mbunge na ana uwezo wa kuwa Waziri?
   
 7. YournameisMINE

  YournameisMINE JF-Expert Member

  #7
  Nov 12, 2007
  Joined: Aug 29, 2007
  Messages: 2,451
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 145
  ktk nafasi hizo za kuteuliwa I wish moja apewe Mheshimiwa sana, memba wa JF bwana Mkulukulu ES ili akatusaidia ku-shake up mambo bungeni kwa kumkoma nyani (sio Ngabu) giladi mchana kweupee!!.
  Asante......mambo ya jumapili haya, watu wanapiga "ustaadhi ushungi"
   
 8. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #8
  Nov 12, 2007
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Nachokijua wanaotoka ni Mramba na Mungai,na hili liko wazi..Mramba ameshaanza kujiandaa kuachia ngazi,Mtandao haumtaki.

  Mh. William Ngeleja kutoka ni vigumu,ni mmoja wa vijana ambao Kikwete anawaamini sana,na mara kadhaa Muungwana amekuwa akumfagilia,anaweza kumpa u -full minister.
  Masha,Dk Mathayo wanaweza kung'oka,Kwanza Masaha aliharibu sana wakati yuko Madini pamoja na Matahayo,REjea mabadiliko ya Mawaziri ya kipindi kile.
  Dk. Nchimbi ndie mchawi mkubwa wa kikwete,Kumng'oa yeye ni sawa sawa na kumuangusha JK,Kwa hasira anaweza kumuanika Muungwana hadharani.
  Professa Msola ,huyu anaweza kungoka,Wizara imemshinda na hata juzi wakati wanafunzi maakada walipokuwa Dodoma wanalalmika kukosa Mikopo kuchelewa JK alichukizwa na hili,na alimuuliza hivi ni lini utaacha kuwalea watu wa bodi?
  Profess Mwandosya hawezi kung'oka ,Kwanza itapunguza mtaji wa CCM katika kura hasa Mbeya ambako kanda ya kusini wanaamini Mwandosya ndio Rais wao.
  Mabadiliko yanakuja ila ni Desemba,ila nalolijua cabinet iliyopita Muungwana alikataa Kuwaongezea muda PSRC,kuna kashfa nzito ambayo ilimchukiza muungwana..
   
 9. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #9
  Nov 12, 2007
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Mwanakijiji mbona hautaki kuwa muwazi,Sema ni nani huyo aliyeitwa ikulu?
   
 10. S

  Si Kitiyi Member

  #10
  Nov 12, 2007
  Joined: Sep 26, 2007
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  VIPI KUHUSU WALIOTAJWA KWENYE KASHFA YA UFISADI: KAMA KARAMAGI, CHENGE NA WENGINEO? INA MAANA WATAENDELEA KUWEPO?
   
 11. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #11
  Nov 12, 2007
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  karamagi atfanyiwa reshuffle tu,
   
 12. J

  Jafar JF-Expert Member

  #12
  Nov 12, 2007
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Muungwana anashindwa kufahamu kuwa tatizo ni yeye mwenyewe na PM wake. Hata akiweka watu safi kiasi gana kwanza watakuwa sidelined na kuonekana hawawezi. Management style ya JK ndio tatizo.
   
 13. Domo Kaya

  Domo Kaya JF-Expert Member

  #13
  Nov 12, 2007
  Joined: May 29, 2007
  Messages: 530
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  UMEMSAHAU MH. KALAMAGI naye ni OUT arudi kwao akalime.
  msije shangaa nafasi yake akapewa ROSTAM AZIZI.
   
 14. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #14
  Nov 12, 2007
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Mramba akae Benchi bwana amechoka kwanza sidhani kama anaweza kukabiliana na challenge za kibiashara zilizopo hapa duniani.
  Akatusubiri tukapambane nae 2010 kule jimboni kwake alikobinafsisha.Asubiri kukabiliana na kizazi kipya

  Ila Makamba waziri tena? Duh,hii itakua mbaya kuliko ni bora JK asifanye mabadiliko
   
 15. K

  KakindoMaster JF-Expert Member

  #15
  Nov 12, 2007
  Joined: Dec 5, 2006
  Messages: 1,349
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Hii itakuwa hatari sana
   
 16. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #16
  Nov 12, 2007
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  nadhani wenye njaa sana wakiingizwa kilio kitaanza upya. nadhani usalama wa taifa wakihusishwa wanawajua wale ambao hawana kashfa wala nini. tuache mambo ya kishkaji na kubebana. sera ziwe ndicho kigezo cha kiongozi bora. hatutaki watawala bali viongozi maana watawala ni makatibu wakuu wa wizara hizo. naunga mkono mabadiliko ya kabineti hasa yakiwa chanya
   
 17. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #17
  Nov 12, 2007
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  ina maana viongozi wetu huwa wanapangwa na hawa watu wa Usalama??
   
 18. M

  Mpiganaji Member

  #18
  Nov 13, 2007
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mmh na yaje tu hayo mabadiliko maana, ila bila kuwatoa mafisadi itakuwa haina maana.
   
 19. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #19
  Nov 13, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280

  Mheshimiwa Admin.. naomba tuirudishe kule kwenye Siasa kwani kuna mambo mazito sana ndani yake.

  Ni wazi kuwa Baraza lililopo sasa licha kupewa semina ya Ngurdoto halijaweza kutimiza na kutuliza kiu na matarajio ya Watanzania.

  tatizo langu kubwa ni kuwa kama atakubali kufanya mabadiliko wakati huu atakuwa ameonesha udhaifu mwingine kama kiongozi, ule wa kutabirika!
   
 20. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #20
  Nov 13, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  On the other hand, Makamba akiunyaka Uwaziri nina uhaika atakuwa ni Waziri Mzuri kuliko hawa maprofesa walioulundikana kwenye maofisi yao yenye viyoyozi vinavyonguruma kwa kupiga mluzi! Makamba siyo political strategist ila yeye ni mtendaji na kiongozi kweli. Nafasi ya Ukatibu Mkuu haikumfaa lakini akiwa Waziri believe me watu watapenda utendaji kazi wake kwani ni miongoni mwa viongozi wachache ambao wanajitolea kikweli kweli katika kazi zao na ni mtu anayeshirikisha mawazo mbadala na kusikiliza.

  Cheo Kizuri kwa bwana huyu ni Uwaziri unaohusiana na maisha ya kila siku ya wananchi ambapo maamuzi ya kijasiri yanatakiwa. Mambo ya Ndani, Elimu ya Juu n.k zitakuwa ni nafasi nzuri kwake.
   
Loading...