Funguka: Wimbo wa Diamond - SIMBA na Harmonize -YANGA upi mkali?

feyzal

JF-Expert Member
Apr 20, 2016
6,784
12,593
Wakuu habari ya majukumu.

Mbali kufanya kazi ngumu za kutafuta kipato ila sio mbaya kuna mda unachangamsha mwili na akili kwa vitu vyepesi kupunguza machungu ya ugumu wa maisha, wengi wetu tunapenda mpira na kwa hapa Bongo timu zenye Mashabiki wengi ni SIMBA na YANGA.

Hivi juzi kulikua na tamasha la simba day na miongoni mwa mambo yalifonyakia ilikua msanii namba moja nchini Diamond platnumz kuwatungia wimbo na kufanya shoo kali pale kwa Mkapa,huku nao Yanga hawapo nyuma wakamsajili msanii namba mbili ama moja kwa sasa nchini nao amewatungia wimbo na pia atapaform kwenye tamasha lao mwisho wa mwezi huu.

Binafsi nimependa ubunifu huu ni wa kibiashara zaidi, sasa basi bila shaka tumeshazisikiliza nyimbo zote, tutoe maoni ipi kati ya hizo ni kali na ni kwanini?

Mimi kwa maoni yangu Nampa Diamond 80% na Konde boy 50%

Kwanini Diamond 80%
Biti kali ina vinanda vya kuamsha unaweza cheza mahala popote hata kutikisa kichwa
Melody imetuli
Kuna vionjo vichache amevitia viko poa
Mashairi hajaimba sana ila yana kejeli fulani kwa wapinzani pia kawasifu simba yapo poa.

Kwanini Harmonize 50%
Mashairi mazuri
Baadhi ya vitu amecopy kwa diamond ikiwemo sehemu ya mashairi alichofanya kuyageuza tu.
Biti imemuangusha imekaa local sana na haina vionjo.

Toa na wewe maoni yako

NB: Hapa hatutaki matusi na kejeli toa maoni kistaarabu
 
Back
Top Bottom