FUNGUKA: ‘Nacheza Mechi Za Majuu Pekee’

Ethan Cruz

JF-Expert Member
Apr 29, 2021
231
331
condoms-875x500.jpg

KWA wengi suala la mahusiano ya pembeni katika ndoa haliruhusiwi kamwe.

Lakini licha ya haya, kuna baadhi ya wanaume ambao bado wana mwanya wa kurambaramba vya nje.

Daniel ni mmoja wao. Inapowadia katika masuala ya kusakata mechi za nje, yeye ni gwiji. Dume hili haliitwi gwiji tu bila sababu kwani viwango vyalo vya kusakata mechi za nje, ni vya kipekee.

Daniel ana mke, na pamoja na mkewe wamejaliwa watoto watatu. Yeye ni mfanyabiashara shupavu ambapo anamiliki majengo kadhaa ya kibiashara jijini Nairobi na Mombasa. Kwa upande mwingine, mkewe ni meneja wa benki moja jijini Nairobi.

Mbali na kuumbika kwelikweli, kaka huyu ana mapeni si haba. Biashara zake zinampa mapato mazuri na pamoja na mkewe, wanajiweza kifedha.

Hii inamaanisha kwamba hana tatizo lolote la kifedha na hakuna wakati hata mmoja ambapo familia yao imeonekana kupungukiwa.

Machoni mwa wenzake Daniel ana kila kitu anachohitaji maishani. Sio tu pesa na sifa, bali pia mke mrembo na watoto maridadi. Lakini licha ya haya, ameshindwa kabisa kuachana na mechi za ugenini. Hasa huwalenga wanawake wenye mifuko mizito na mara nyingi shughuli zake huzitekeleza kimataifa.

“Mechi zangu huchezwa katika miji ya nchi za ng’ambo kama vile London, Paris, New York, kwa kutaja tu michache. Kwa kawaida mimi hunasa mabinti wenye mifuko mizito, kumaanisha kwamba wana uwezo wa kifedha wa kugharimia ziara zetu.

Mimi hunasa wanawake mabwenyenye mtandaoni na kuwashawishi kufadhili hizo ziara zangu, vile vile kuishi katika baadhi ya hoteli ghali sana ulimwenguni.

Nina mpenzi katika sehemu kadha duniani, na sio tu wapenzi, mabinti walio na akaunti kubwa kubwa za pesa.

Nina mpenzi kutoka Uswisi niliyekutana naye mtandaoni na baada ya kufanya uchunguzi nilitambua kuwa ana hisa katika kampuni kubwa ya kuunda magari. Baada ya mazungumzo ya miezi kadhaa mtandaoni alinitumia tikiti ya ndege kwenda jijini Zurich. Huko tulikaa kwa wiki kadhaa na kuzuru sehemu kadha wa kadha nchini humo.

Tukiwa nchini humo nilipata fursa ya kukutana na milionea fulani kutoka Ujerumani ambapo alionekana kuvutiwa nami. Tulipokuwa tumekaa kwenye ukumbi wa hoteli pamoja na huyo mpenzi wangu raia wa Uswisi, niligundua kwamba binti huyo Mjerumani alikuwa akinikodolea macho kwa muda. Mswisi alipoondoka kwenda msalani, binti hakupoteza muda na kuniitisha namba ya simu.

Licha ya kuwa nina pesa zangu, binti huyo Mswisi amekuwa akinitumia kitita kikubwa cha pesa kila mwisho wa mwezi. Anafahamu kwamba nina mke na watoto, lakini hilo halimbabaishi. Hata anapotuma pesa, anahakikisha kwamba anamtumia pia mke wangu.

Pia, nina binti fulani kutoka Amerika ambaye tulikutana naye jijini Nairobi tukiwa katika kongamano la kibiashara. Kwa muda sasa amekuwa akifadhili ziara zetu katika miji mikuu kadha wa kadha duniani”.

Mke wangu anajua kuhusu maisha yangu haya ya pembeni na hana tatizo mradi niwe mwangalifu na kujikinga kutokana na maradhi ya zinaa. Anajua kwamba yeye pia hunufaika kifedha kutokana na mahusiano yangu haya”.


ok jombaaaa je nyinyi ama sisi tunaochepuka mechi za nje
je unaangalia yafuatayo
1,,pesa,,, uzuri,,,hadhi,,,mwonekano?
UNATAKIWA kama una mechi za ugenini/nje basi hakikisha kiwanja unachoruka nacho kimemzidi yule uliomwacha nyumban
ama ndani kz usichepuke na mtu t hana mbele wala nyuma yn mpk mkewako akikufumania anakudharau
sioumeona ktk makala yetu hapo mke wa daiel anafahamu mechi za mumewe lkn hajagomba koz jamaa anapiga
count atak za mbali na mkewe pia anafaidika japo kazidiwa kipesa na hadhi pia so
angalien huko mnapochepukia msifakamie t hadi wauza mihogo
 
😂😂 😂 nmependa sana hii nakala aloo yn mke kavu kala buyu
amempa tu jamaa NB; fakamia ila kuwa makini atumie kinga na afakamie watu wenye hadhi kumzidi na uzuri kumzidi yeye respect sn
 
Back
Top Bottom