Fundisho kwa mnaopenda kuchati chati hovyo

young MathematiciAn

Senior Member
Oct 31, 2016
160
361
Kama nusu saa zilizopita nilikuwa kwenye basi la Goms-Masaki nikirudi zangu kitaa.

Tukiwa kwenye foleni maeneo ya Ngozi,pale kwenye makutano ya Keko, Karume na Ngozi, kiukweli palikuwepo na foleni cha kizushi.

Mimi nikiwa siti ya mbele kabisa karibu na dereva nikishuhudia tukio la mzembe akilizwa na mjanja A-z.

Mara kidogo bodaboda iliyokuwa na watu 2. Dereva na mwenzake nyuma walipita katikati ya lanes 2, sasa gari fulani hivi ukilitizama linavutia sana jamaa wa lile gari alikuwa peruzi simu yake akivutia foleni itembee tembee sijui masikini ya mungu alikuwa anachati whatsap, ana peruzi JF, Fb au Instagram.

Mara paap yule jamaa aliyepakizwa nyuma kwenye bodaboda akashuka na kwenda kuchukua simu ya yule jamaa kiulaini bila bughudha yeyote kama vile chatu akimla mbuzi.

Baada ya tukio jamaa akatembea hatua 3 na kupanda bodaboda hao wakatembea na kutokomea pasikojulikana.

Jamaa kustuka anafungua mlango na kushuka ikawa too late kwa kihindi tunasema marighaya, ikabidi ashike kichwa na kuwatizama tu kama vile mfiwa akisindikiza jeneza, jamaa kwa unyonge akaingia kwenye gari lake akisubiri foleni itembee arudi zake kwake.

Fundisho;

1.Kwanini uchati ilhali dirisha umeacha wazi tena huna wasiwasi wowote.
 
Ni kweli kabisa hiyo style mbona ipo sana tu tuwe makini kwani imewahi kumkuta jamaa yangu yeye alikwapuliwa mkononi na mtu aliyepakiwa kwenye pikipiki hao wakatokomea zao.
 
Mimi nili uziwa maji ya bomba pale Nyegezi badala ya uhai. Nilimpa MTU alie dirishani aniitie MTU mwenye anauza maji, akaja mama MTU mzima kidogo akiwa na chupa mbili za maji, yule niliempatia Pesa akampa kisha akapewa maji

Kuyafungua, Imbombo NGAFU fijo, yamejaa hadi mdomoni, hayajafungwa, yana tope!!!

Kumtizama mama pale chini Maana tulikuwa kwa basi, alishatokomea kitambo ndani ya sekunde tatu tu nikawa nimelizwa buku
 
Hapo hapo mataa ya Chang'ombe waliikosa kosa simu yangu, nilikua nachat na kioo kiko chini. Sijarudia tena kuchat kioo kikiwa wazi
 
Mimi huwa watu wa Dar wananishangaza ..mtu anapigwa roba kweupe kabisa anatembea tu kwa miguu kutoka mataa ya Stanbic hadi Sealander na hamna wakumsaidia
 
Hapo hapo mataa ya Chang'ombe waliikosa kosa simu yangu, nilikua nachat na kioo kiko chini. Sijarudia tena kuchat kioo kikiwa wazi
wengine vi-baby walker vyetu havina kiyoyozi, inakulazimu ufungue tu. ngoja nikasukie nyavu madirisha maana nahisi kitecno changu kitajakwapuliwa muda so mrefu.
 
acha kabisa mkuu. hapa mjini mradi tu na wewe uwapigie honi watu. sasa na kibarabara cha kibangu-makoka t
kilivo rafu naona ndo kinakakongoroa kabisa ka only begotten baby-walker kangu.
Kile kinjia nilipita mwaka juzi. Kiko rafu sana
 
Hiyo ndiyo dar. Huku kwetu haufiki mbali, ushakuwa majivu.
Watu wa mikoani huwa hatulei upumbafu. Huku kwetu iba hata karanga tu za 100 utachezea kichapo cha kufa binadamu
Wamikoani mnavyojipaisha utafikiri wa huku dar wote ni wazaramo kumbe sisi pia tumetoka huko huko mikoani
 
Back
Top Bottom