Fundisho gani serikali imepata kutokana na haya majanga?

Zipuwawa

JF-Expert Member
Nov 28, 2010
3,051
653
Hakika Mungu amejaribu kuionesha Serikali ya Tanzania kutokana na Mzaha mzaha unaofanywa na serikali hii. Uzamaji wa Boti Zanzibar umetokea wakati Wizara ya mambo ya ndani kupitia majeshi yake yanayopaswa kusimamia usalama na ukoaji yalivyoonesha udhaifu mkubwa kuanzia taarifa mpaka uokoaji.

Kwanza Kikosi cha Uokoaji kimeshindwa mpaka sasa kuokua miili ya waliopatwa na ajali hii ya Boti. Bungeni wabunge wamekuwa wakilaumu sana serikali kwa kutonunua vifaa vya kisasa lakini wabunge hao waliishia kupiga makofi na kuunga mkono hoja 100% kwa 100%. Leo hii tunashuhudia vikosi vya ukoaji vikishindwa kufanya kazi yake ipasavyo.
Zipo Wapi ndege za kupiga picha alizosema waziri wa Ulinzi? si zingeweza hata kupiga picha za tukio hilo Taarifa zimetolewa saa saba mchana eneo la tukio waokoaji wamefika saa kumi na moja Je hii si aibu kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?

Pili Tumeshuhudia majanga mengi kama ya moto yakitokea na kuteketeza mali zote huku vyombo hivi vikiwepo na watendaji wake wakilipwa mishahara minono na kusifiwa kuchapa kazi..Mfano soko la Tunduma wakati likiungua gari la zimamoto la kwanza kufika lilitokea Zambia na lile kutoka Mbeya mjini likfika hata moto umezima. Je kuna haja ya kuwa na taasisi hizi zinazotupotezea fedha nyingi za walipa Kodi?

Angalia yanapotokea maandamano polisi wanavyofika haraka katika eneo la tukio je kwanini Wizara hii isifanye majuukumu yake ipasavyo?

Nasikitika Serikali ya Tanzania mara nyingi imekuwa ya kuunda tume mbalimbali za uchunguzi ambazo zinasababishwa na wao wenyewe. Tutaendelea kupeteza ndg zetu na mali zetu mpaka lini?

Ni wazi kuwa Serikali yetu haina nia ya kutatua matatizo yatokanaoyo na majanga mbalimbali kwani hakuna hatua yoyote inaandaliwa kujipanga na majanga ya namna hii. Sasa hivi katka habari Miili ya maiti inaoneshwa kuelea na waokoaji wakilalamika kutokuwa na mafuta je Serikali imeshindwa hata kutoa mafuta kwa Boti za watu binafsi? Hii ndio serikali ya michakato yakinifu na sikivu? Je viongozi waliotoka bungeni ndio wameenda kupumzika kabisa?

Nasema hili ni pigo toka kwa Mungu ili kuonesha kuwa pajeti wanazopitisha Bungeni na kupigiana makofi zisizokuwa na tija sisiendekezwe. Wizara ya mambo ya ndani inapaswa kuhakikisha inalinda maisha ya watu na si kufanya michezo helikopter iliyopo ya polisi iko wapi au ni kwaajili ya kupambana na vyama vya upinzani tu? Nimetafakali sana na kuona serikali haiwajali watu wake viongozi wetu wapo kwaajili ya maslai yao kununua mashangingi na kuvinjali na familia zao.
 
serikali ya ccm haipati funzo lolote kwa sasa,itapata funzo pale itakapotoka madarakani
 
hela za mafuta za misafara ya viongozi wa nchi na mabalozi na wageni kutoka nje wanazo ila mafuta ya boti hakuna...welcome to bongoland
 
hela za mafuta za misafara ya viongozi wa nchi na mabalozi na wageni kutoka nje wanazo ila mafuta ya boti hakuna...welcome to bongoland[/Q
Basi mafuta ya mwenge yangepunguziwa huko kwani kosa mwenge kuruka mkoa? Mbona sioni faida yake?
 
Back
Top Bottom