Fundi wa Tanesco apigwa shoti ya Umeme na kukatika mkono akiwa JUU YA NGUZO ENEO LA COTEX AFRICANA

mzee wa njaa

JF-Expert Member
Jun 16, 2011
1,366
223
Fundi wa Tanesco apigwa shoti ya Umeme akiwa JUU YA NGUZO ENEO LA COTEX AFRICANA...............HAKIKA HII NI AJALI MBAYA AMBAYO IMEPATA KUSHUHUDIWA.

Alikuwa kakaa juu ya nguzo za Umeme eneo la kiwanda cha Cotex jioni hii karibia na Africana wakifanya marekebisho ya baadhi ya nyaya zenye matatizo na wakati huo umeme ulikuwa umekatwa kama kawaida ya Tanesco na ratiba halisi ni umeme ulitakiwa urudishwe kuanzia saa 12:00 jioni...............Kwa kawaida umeme eneo husika huwa unarudishwa saa 12:00 jioni ila leo saa 11:00 ukarudishwa ghafla huku mafundi wakiwa juu kwenye Nguzo...................Jamaa alipigwa shoti ya mkono na mkono ukakatika na kipande kuanguka chini kama tawi la mti na yeye kukaukia akiwa juu ya Nguzo......Ni tukio la kusikitisha sana...............Sasa cjui Tanesco itachukua utaratibu gani kutokana na tatizo hilo.

R.I.P Fundi wa Tanesco.
 
Hivyo ni kusema Tanesco imesababisha mauaji haya.. Nimestushwa na hii taarifa. Inaleta simanzi....
Mawasiliano haba baiona ya watendaji huleta misiba ktk jamii.

Mungu awarehemu wafiwa
 
wamezidi bana...watu kutwa simu zetu hazina chaji wanachezeachezea tu umeme...
 
R.I.P fundi.
Mauti haya yanayosababishwa na uzembe yataisha lini? Viongozi mlio na dhamana tafadhali wajibikeni.
 
Tanesco ni wazembe na ndio wansababisha migao kwa kuyokuwa na plan za muda mrefu na hata kama wanazo hawana ujanja wa kuzitekeleza, wao ni wazuri kutelekeza na wamesha-muangamiza huyu ndugu yetu kwa uzembe wao.

Its time Symbion should take over, or is it Dowans of USA.
 
Inasikitisha sana. Ila, Kwani hakuwa na vifaa? Kwanini apande bila kuwa na vifaa? Au aliamua kupanda bila vifaa kwa sababu umeme hamna? Je hivyo ndio ufundi unavyofundisha? Tanesco walikuwa hawana habari kuwa kuna marekebisho maeneo hayo? Kwanini hawakuzima transformer inayopeleka umeme maeneo hayo kama mafundi wengine wafanyavyo? Tuache hayo maana kuna kama kauzembe fulani hivi. Roho ya marehemu ipumzike kwa amani!
 
&lt;br /&gt;<br />
&lt;br /&gt;<br />
Inasememekana huyo fundi hakuwa mtu wa tanesco kwa mujibu wa taarifa ambazo nilizipata eneo la tukio,kutoka kwa mmoja wa mafundi wa tanesco w aliyokuwa wakipita eneo hilo baada ya kufanya mawasiliano na tanesco ili kujuwa kama kuna mafundi wowote ambao walipangiwa kazi eneo hilo.
 
thanx kwa kunipa data ndugu.
duh, kumbeee! Sasa tumwite mwizi au?
 
wamezidi bana...watu kutwa simu zetu hazina chaji wanachezeachezea tu umeme...
Sikutegemea comment kama hii kutoka kwako Kigogo!... Nachokielewa Tanesco wamesababisha mauaji maana service inapofanyika kunakuwa na taarifa katika eneo husika na baada ya service hufanyika mawasiliano ndipo umeme unawashwa.... hapa kuna mawili either service imefanyika bila mawasiliano au uzembe umefanyika kwenye sehemu ya kuwashia ......R.I.P Jombaaa
 
Back
Top Bottom