Fundi wa kawaida VS Mkandarasi yupi ni bora?

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
2,056
2,515
Jana nilimwona Mkuu wa mkoa wa Shinyanga akimfokea kiongozi mmoja wa wilaya mmojawapo wa Mkoa wa Shinyanga akimuuliza kuwa ni yupi aliyeamuru Mkandarasi kujenga jengo husika badala ya Local Fundi.

Binafsi nilisikitika sana na kujiuliza kati ya Local Fundi na Mkandarasi yupi ni bora. Katika Tanzania hii mkandarasi anaichangia sana Serikali mapato kwa maana ya kodi ya mapato, Leseni, mapato anapoomba kazi, na mapato mengine mengi lakini kwa lugha ile ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga naona kama kwa sasa hakuna haja ya kuwa na Wakandarasi.

Ninawauliza CRB je kwa sasa mnawatetea vipi Wakandarasi kwa sababu naona kila mahali kama vile hawatakiwi hasa kwenye ujenzi wa majengo ya Serikali. CRB nawashauri kuwa tumieni utalaam wenu kwa kuishauri Serikali. Acheni woga.
 
Yupo sahihi, Force account unatumia local fundi.
Kwani mkandarasi anatumia fundi wa nchi gani?​
Hapa ni kuwanyima fursa wasomi wanaopambana angalau kujiajiri kwa kufungua kampuni.​
CRB nayo ipo kimya haimtetei mkandarasi kazi kukusanya fees tu.​
 
Mkandarasi siyo mtu Ni usajili wa kampuni yenye jopo la mafundi kwenye ngazi maalum ya kiufundi!
Mkandarasi anaweza kuwa fundi lakini fundi siyo lazima awe Mkandarasi
 
Back
Top Bottom