Fundi Trekta anapatikana

Habari za kazi wanaJF
Ningependa kutangaza upatikanaji wa huduma za kiufundi kwa wenye trekta na vyombo vinginezo vya ukulima kama vile combine harvester, generator, pump na kadhalika.
Tatizo liwe ni engine, mfumo wa hydraulic, transmission/gearbox au hata service za kawaida, huduma ni ya hali ya juu na kutumia vipuri halisi na bora.
Mawasiliano: twaeza tumia inbox ya hapa JF ili kuwezesha ufatiliaji kwa urahisi - reputation building.
Asanteni.
Ungetoa Contacts zako humu, kuzikimbizia Inbox inafanya watu wasikuamini.
 
Ungetoa Contacts zako humu, kuzikimbizia Inbox inafanya watu wasikuamini.
Unaamini mtu ukiona namba zake au kazi yake? Wewe je, unaaminika je kama namba wapatia watu wakitafuta soko la trekta zao. Hapo juu kichwa chasema nini? Dalali au Fundi?
 
Unaamini mtu ukiona namba zake au kazi yake? Wewe je, unaaminika je kama namba wapatia watu wakitafuta soko la trekta zao. Hapo juu kichwa chasema nini? Dalali au Fundi?
Sasa kazi zako tutaziona kupitia nini kama sio Namba na mawasiliano??
Mtu akitaka kuwasiliana na wewe atakupata humu JF masaa yote 24??
Wewe unashinda huku masaa yote??
 
Sasa kazi zako tutaziona kupitia nini kama sio Namba na mawasiliano??
Mtu akitaka kuwasiliana na wewe atakupata humu JF masaa yote 24??
Wewe unashinda huku masaa yote??
Nipo masaa yote kaka, kwa mawaidha, maoni na kadhalika. Ila kazi ni mambo tofauti, itafanyika je kupitia mtandao?
 
Kwa wale wanaotaka kuziona kazi zangu waeza tembelea Facebook wakatafuta Mercs & Marques.
 
Mkuu nataka kununua used massey MF 375 naomba ushauri
Juu ya 1. Capacity yake wakati wa kulima
2. Fuel Consumption
3. Durability yake

Naomba ushauri wako u compare na Mashine za sasa kama newholland
Hbr za kazi kaka,
MF 375 ina engine ya 3.9lt ya cylinder nne, New Holland TT60a pia ina engine ya ukubwa huo huo. Tukiziangalia vyombo hivi viwili, kwa maoni yangu, MF 375 naona iko juu kwa kazi za kilimo - mfumo wake wa hydraulic, three point hitch yake ina uwezo karibia tani mbili ilhali New Holland TT60a ina tani unusu! Kwa upande wa nguvu za engine MF 375 iko chini kwa horsepower mbili hivi hii kwangu inaashiria consumption yake itakua ya chini kiasi kwa kua engine imepunguzwa nguvu.
Kwa maoni yangu, MF 375 iko juu!
 
wakuu uzi tuendeleze, mi natafuta tairi za nyuma zile kubwa ambazo ni used size 18.4-30. mwenyejua zinapatikana tafadhali tusaidiane
 
Back
Top Bottom