Fundi hata umbane vipi akitaka kukuibia atakuibia tuu

atlas copco

JF-Expert Member
Jun 15, 2015
5,234
2,000
Fundi siku zote anategemea kula anapoenda kununua material, unapombana hapo lzm atafute namna nyingine ya kukuibia, kwa kifupi kila mtu anakula kwenye ofisini yake
 

Dagger-v

JF-Expert Member
Mar 6, 2020
2,202
2,000
Africa ina laana. Watu ni kuibiana tu. Lazima umbane kisomi. Ama sivyo utafanyiwa kazi mbaya. Suluhisho ni kusimamia ujenzi mwenyewe mchana na usiku. Au tafuta mtu mwaminifu asimamie hasa kuhakiki kazi ni imara, ratio za siment ni sawa. Unene wa nondo ni sawa. Pima maji, kobiro, na skwea zipo. Nk.
Africa imejaa laaana
 

DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
16,852
2,000
Hawa jamaa dawa yao ni kujenga nao urafiki na kama ikiwezekana hata msosi wapikiehapo kiasi fulani utapunguza mipango ya upigaji,ukisema uwabane sana utapotea maana jamaa wana mbinu nyng za upigaji
Exactly,
mafundi wakiwa na njaa Ni hatari Sana.

Mimi kwny kazi zangu,
Nasimamia mwnyw.

Na
Chakula Cha mafundi tunakula pamoja, na Ela ya chakula Ni nje ya Ela ya ufundi.

nawatengenezea urafiki na undugu flani wa muda ili kazi yangu iende.

Nnavojua,
Mafund Ni mabahili Sana Kutoa Ela ya kula. Hasa Kama ana wasaidizi wengi
 

DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
16,852
2,000
Binafsi mi hupendelea kufanya kazi na mafundi walevi.

Wasumbufu Sana wakifanyia kazi ofsini kwao.


Ila ukiwapa kazi wakafanyie saiti,
Na kreti la bia au mzinga wa konyagi uko eneo la tukio.

Mtafanya kazi vizuri Sana.

Ni waongeaji mno, matusi, kujisifia ndo jadi yao na kazi itaendelea bila kukuboa msimamizi.

Na wakichoka watalala usingz pale pale saiti.

Nguvu na akili ya kuiba vifaa haitokuepo hapo.
 

SMU

JF-Expert Member
Feb 14, 2008
9,612
2,000
Wizi mkubwa ni katika kununua materials na materials yenyewe (hasa kwenye ujenzi). Mara nyingi sana wana collude na wauzaji. Anakwambia kitu fulani twende tukanunue duka fulani....kumbe keshaongea na muuzaji, kaweka cha juu. Ukitaka kununua pengine, utaambiwa huko utauziwa feki au havina ubora anaotaka. Shida sana.

Au hapo hapo dukani kama haupo makini katika kuhesabu pia anakupiga. Amekuandikia anataka idadi x ya vitu, lakini wakati wa kupakia anaongea na mwenye duka apakie (x-y) hiyo y ni pesa ya fundi atakuja kuichukua baadae. Hivyo x-y visipotosha atakwambia vifaa vimeisha muongeze vingine ....inaweza kuwa hiyo y au zaidi.

Na wakiona mjanja kwenye kuhesabu, wanaenda kukupigia site kwako. Umeleta rolls 20 za wire za umeme, wao wanaiba 5, wanatumia 15 kwa kazi yako na zikipelea wanakwambia ukaongeze (na huna namna ya kupima kiwango cha waya kilichotumika).

Wengine ni wabaya zaidi. Unaleta vifaa (say hizo wire) original, yeye anabadilisha anakuwekea feki hizo original zako anauza. Hasa kama hufiki site Mara kwa Mara.

Kwa kweli wana mbinu nyingi sana. Ukikwepa huku, unapigwa kule. Usikimbilie tu fundi wa bei ya chini, mara nyingi wana namna ya kuhakikisha wanapata watakacho. But again, hata mafundi wa gharama wanaweza kuiba pia.
 

Miguel Alvarez

JF-Expert Member
May 28, 2019
693
1,000
Binafsi mi hupendelea kufanya kazi na mafundi walevi.

Wasumbufu Sana wakifanyia kazi ofsini kwao.


Ila ukiwapa kazi wakafanyie saiti,
Na kreti la bia au mzinga wa konyagi uko eneo la tukio.

Mtafanya kazi vizuri Sana.

Ni waongeaji mno, matusi, kujisifia ndo jadi yao na kazi itaendelea bila kukuboa msimamizi.

Na wakichoka watalala usingz pale pale saiti.

Nguvu na akili ya kuiba vifaa haitokuepo hapo.
Hakika mkuu na pia mafundi ukitaka kwenda nao sawa usioneshe wasiwasi kuhusu wao cha kufanya wewe waaminishe kuwa unawaamini utajikuta mmekuwa marafiki na wataanza kufunguka na utajua tuu michezo yao michafu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom