mshikachuma
JF-Expert Member
- Dec 2, 2010
- 2,853
- 626
Nikiwa mmoja kati ya watu waliobahatika hii leo kufatilia mjadala wa KATIBA
kupitia luninga ya STAR TV,pamoja na mambo yote yaliyozungumzwa ikiwamo
katiba ni nini,maoni,na michango ya simu kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje
ya nchi, ilitokea simu moja kutoka Bagamoyo kwa fundi bajaji. Pamoja na kuwa kila
binadamu anao uhuru wa kutoa maoni yake'lakini huyu jamaa kaniacha hoi bin taabani.
Eti anasema hakuna haja ya kuwa na katiba mpya ila kinachotakiwa ni uongozi bora serikalini.
Haitoshi anasema katiba ni janja ya wanasiasa wa vyama vya upinzani ili kutimiza malengo
yao. pia akaongeza kuwa kwa sasa tusidai katiba,ila tudai kuelimishwa ni nini maana ya katiba
ndani ya mika 5 au hata 10 kutoka sasa. Kusema kweli huyu jamaa kanichanganya. Na Je nyie
wenzangu muliofuatilia mjadala ule leo mnasemaje kuhusiana na kauli ya yule mtu?