Fundi Bajaji wa Bagamoyo! Kulikoni?

mshikachuma

JF-Expert Member
Dec 2, 2010
2,853
0
Nikiwa mmoja kati ya watu waliobahatika hii leo kufatilia mjadala wa KATIBA
kupitia luninga ya STAR TV,pamoja na mambo yote yaliyozungumzwa ikiwamo
katiba ni nini,maoni,na michango ya simu kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje
ya nchi, ilitokea simu moja kutoka Bagamoyo kwa fundi bajaji. Pamoja na kuwa kila
binadamu anao uhuru wa kutoa maoni yake'lakini huyu jamaa kaniacha hoi bin taabani.
Eti anasema hakuna haja ya kuwa na katiba mpya ila kinachotakiwa ni uongozi bora serikalini.
Haitoshi anasema katiba ni janja ya wanasiasa wa vyama vya upinzani ili kutimiza malengo
yao. pia akaongeza kuwa kwa sasa tusidai katiba,ila tudai kuelimishwa ni nini maana ya katiba
ndani ya mika 5 au hata 10 kutoka sasa. Kusema kweli huyu jamaa kanichanganya. Na Je nyie
wenzangu muliofuatilia mjadala ule leo mnasemaje kuhusiana na kauli ya yule mtu?
 
chilamjanye

Senior Member
Oct 5, 2007
110
0
kweli hadhi yake ya kuchambua mambo ni yakibajajibajaji so muache ndo uwezo wake ulipofikia wa kuona mambo
 
Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
10,831
2,000
Nikiwa mmoja kati ya watu waliobahatika hii leo kufatilia mjadala wa KATIBA
kupitia luninga ya STAR TV,pamoja na mambo yote yaliyozungumzwa ikiwamo
katiba ni nini,maoni,na michango ya simu kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje
ya nchi, ilitokea simu moja kutoka Bagamoyo kwa fundi bajaji. Pamoja na kuwa kila
binadamu anao uhuru wa kutoa maoni yake'lakini huyu jamaa kaniacha hoi bin taabani.
Eti anasema hakuna haja ya kuwa na katiba mpya ila kinachotakiwa ni uongozi bora serikalini.
Haitoshi anasema katiba ni janja ya wanasiasa wa vyama vya upinzani ili kutimiza malengo
yao. pia akaongeza kuwa kwa sasa tusidai katiba,ila tudai kuelimishwa ni nini maana ya katiba
ndani ya mika 5 au hata 10 kutoka sasa. Kusema kweli huyu jamaa kanichanganya. Na Je nyie
wenzangu muliofuatilia mjadala ule leo mnasemaje kuhusiana na kauli ya yule mtu?

Mimi nikisema watu wa Pwani hamnazo mnaniita mimi mbaguzi.

lakini poa tu.
 
Kishalu

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
1,174
2,000
Lakini kuna ukweli ndani yake kwa watanzania wengi hawajui katiba ya tanzania ya sasa inasemaje maana bado wapo watu wengi ambao hata kusoma na kuandika bado hawajui kwa hiyo kinachotakiwa ni kuwaelimisha hasa hili kundi na wajue nini maana ya katiba na mabadiliko ya katiba yafanyike maana hata wakati wa kutafuta uhuru kwa wakoloni sio watanzania wengi walikuwa wanaamini kama inawezekana, kwa hiyo ni kutoa shule popote na wakati wowote inapohitajika lazima mabadiliko yawepo kwa sisi ambao hata tunaweza kupeana habari kwenye haka JF tunaweza kabisa kuwaelimisha na wakaacha hata kupokea hizo khanga,kovia na 3000 kutoka kwa mafisadi na wakaelewa hata maana ya kodi yao maana huyu jamaa wa Bajaji haelewi hata kodi yake inafanya nini

KATIBA KATIBA KATIBA Elimisha wote ambao haelewi
 
Malunde-Malundi

JF-Expert Member
Jan 10, 2008
1,288
0
Watu wengi wa pwai vilaza mkuu ndio maana tunawahamisha hata makazi na kuwatokomeza, nilimsikiliza ila anaonekana hata hakai bagamoyo bali ni waziri mmoja aliyejitam ulisha namna ile iila mawazo kama hayo ni sawa na ya kombani, hatuna muda wa kupoteza, katiba lazima sasa sticking. Haelewi hata anachohitaji
 
Lupweko

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
13,864
2,000
Watu wengine wakiwa na credit tu kwenye simu zao basi wanapiga simu hata kama ni utumbo. Lakini kwa kuwa ni wa Bagamoyo, hana tofauti na wa Chalinze!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom