Fumbo La Siasa: Hazina Mmilki Maskini Asiyejua Thamani Yake. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fumbo La Siasa: Hazina Mmilki Maskini Asiyejua Thamani Yake.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by DSN, Oct 28, 2011.

 1. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Naomba msaada wa jibu toka kwa great thinkers, kuna Mwanakijiji katika kijiji xxxxx mwenye elimu ya uelewa wa kiwango cha elimu ya watu vijiji vyetu vilivyo vingi Nchini. Mwanakijiji huyo alibahatika kuchimba shimo ndani ya shamba la kijiji na kuibuka na kitu kigeni machoni [Treasure] pake lakini kinachomvutia kuwanacho nyumbani kwake japo ajui thamani yake, kwake yeye bora kiwepo Nyumbani lakini ajui umuhimu wala thamani [value] yake na ajui atakifanyia nini hicho kitu alichochimba na kukiopoa shambani. Japo Mwanakijiji huyu yu maskini lakini hajui hata hicho alichonacho ni nini na kina thamani gani kubadilisha maisha ya wanafamilia yake pamoja na kijiji chake kwa ujumla.

  Siku moja Kijijini pale akaja mtu toka mjini, kwa bahati akafika katika mji wa Mwanakijiji huyo na kubahatika kuona kitu hicho chenye thamani [Treasure] katika nyumba ya Mwanakijiji huyo, basi kwa kujua umuhimu na thamani yake akamua kumuomba Mwanakijiji huyo kifaa hicho ili akakitafutie soko mjini, lakini kwa kuwa Mwanakijiji anakithamini kuwa nacho machoni pake lakini ajui thamani ya kifedha au gharama yake alimgomea kumpa Mwanamjini huyo, huku akizungukwa na fikra kibao.

  Naomba msaada juu ya fumbo la hawa watu wawili Mwanakijiji na huyu Mwanamjini.Huyu Mwanakijiji ajui thamani yake kwa thamani ya kupimwa kwa vigezo [Value] lakini thamani yake iko kwenye kuwanacho tu na kukimilki, na kuwa anacho machoni mwake ni mali yake, na yeye ndiye aliyekivumbua kwenye shamba la kijiji.Wa pili ni huyu Mwanamji anaejua thamani ya hazina [treasure] hiyo lakini hana njia ya kuweza kumilki na kufanikisha kuiuza hazina [Treasure] hiyo ambayo itabadilisha maisha yake na maisha ya Mwanakijiji kwa vigezo kama hata mdhulumu Mwanakijiji huyo au kama anataweza pia kumdhulumu Mwanakijiji huyo.

  Nipeni njia kutatua mgongano huu wa maslahi ya watu hawa wawili.

  Nawasilisha
   
Loading...