Fumanizi ni lazima, labda... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fumanizi ni lazima, labda...

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Sipo, Jul 27, 2009.

 1. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #1
  Jul 27, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Wataalamu wa masuala ya mahusiano wanadai kuwa mtu anapotoka nje ya ndoa ni lazima atafumaniwa. Na kama hatafuniwa mwaka wa tatu tangu aanze uhusiano na huyo hawara yake basi kuanza basi lazima atafumaniwa kabla ya mwaka wa sita wa uhusiano huo haramu.

  Sababu za lazima ufumaniwe ni hizi:-
  • Kujisahau na kuweka ngao ya kujikinga chini mfano badala ya kwenda mbali kufanya mapenzi basi watafanyia karibu,

  • Kumwambia rafiki wa karibu wa kufa na kuzikana akiamini taficha siri,


  • Dhana ya kumilikiana uanza kuingia kati ya hawa wawili na kuanza kuuona kila mmoja ni mali ya mwingine,

  Unaweza kuamini kwamba wewe una maarifa sana na ni mjanja sana na una maarifa mengi ya kukanusha kuwa una nyumba ndogo na kuteleza husifumaniwe. Lakini kwasababu ni nguvu mbovu unazopanda ni lazima utazilipia kwani zitakurudia tu, utake husitake.

  Unapotoka nje ya ndoa jiandae kunaswa siku isiyokuwa na jina. Kama utaacha kabla hujanaswa, siyo kwasababu ni mjanja, bali ni kwasababu hiyo nguvu uliyoipanda ilikuwa haijakamilisha mzunguko wake.

  Unapoonywa na mpenzi/mke wako, au anapoonyesha wasiwasi kuwa unatoka nje, kama ni kweli inabidi uache. Kama utaendelea jua tu kwamba utapata shida, utaumia baadaye.

  Nawasilisha
   
 2. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #2
  Jul 27, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...te he heee :D hao wataalamu bana,.... watu mpaka wanasomesha sekondari fumanizi zero!
   
 3. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #3
  Jul 28, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  hiyo mpaka mtoto yuko sekondari ina mambo mawili:-
  1. Ni mke mdogo ambaye hata mke mkubwa anafahamu
  2. Ni mume alizaa nje ya ndoa kabla au baada ya ndoa lakini hakuna mhusiano tena baina ya wazazi wawili
   
Loading...