Fumanizi-mwanaume anapokuwa kijogoo na mwanamke kahaba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fumanizi-mwanaume anapokuwa kijogoo na mwanamke kahaba

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by MziziMkavu, Aug 28, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 28, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]Mara nyingi hujikuta wakiwa na wakati mgumu


  Wanaume wengi huwachukulia wanawake kama mali zao, ambazo ni wao tu wanaotakiwa kuzimiliki kwa namna fulani. Mali yako ni mali yako, ikitumiwa na mtu mwingine, huumiza hisia. Lakini, mali hii inayoitwa mwanamke, mbona ina utambuzi wake? Kila wakati ukisoma kuhusu mauaji ya wivu wa kimapenzi, wanawake ndio ambao wanauawa zaidi.  Lakini ukija kusoma takwimu za wanaotoka nje, wanaume ndio wanaotoka kwa kiwango cha juu sana. Kama ni kuuawa, bila shaka wanawake wangekuwa wanawaua wanaume kila siku. Hata ukiangalia kwenye fumanizi nyingi, utashangaa kuona nguvu inapelekwa kwa wanawake, badala ya wote waliofumaniwa.


  naonekana kama anayefumaniwa ni mwanamke, yeye ndiye ambaye ametia aibu, na huonekana kama kahaba. Mwanaume ni mara chache sana kukumbana na misukosuko ya fumanizi, hasa kutoka kwa jamii, kwa sababu huonekana kijogoo.


  Kwa nini unadhani hali iko hivyo, wakati mwanaume ndiye mtokaji nje mzuri?


  Ni kwa sababu wanaume hujawa na wivu zaidi pale suala linapohusu mwili kuliko hisia. Wataalamu wanasema, mwanaume anapofikiria kuhusu kumfumania mke au mpenzi wake, picha zinazoenda kwenye mawazo yake ni zile zenye kuhusu mwili. Atatengeneza picha za mkewe au mpenzi wake na huyo mwanaume wakiwa pamoja kwenye tendo. Ataona kila kitu ambacho hufanya na mkewe kikiwa kinafanywa na mtu huyo na pengine ataona ziada. Lakini, picha zote zitakuwa zinahusu shughuli za kimwili.


  Lakini kwa mwanamke picha zitakuwa ni za mwili, lakini pia za kujali. Mwanamke atafikiria au kujenga picha kwamba, mumewe au mpenzi wake ameenda shopping na huyo hawara na anamnunulia vitu vya thamani. Halafu atajenga picha wakiwa pamoja wakiwa wanazungmza kwa furaha na bashasha. Mwanamke huona wivu kimwili na hisia.


  Tafiti zinaonesha kwamba, vipigo na vifo vingi dhidi ya wanawake kutoka kwa wapenzi wao hutokana na wivu. Kwa hali hiyo, wivu unaongoza katika kusababisha maumivu ya kimwili na hisia kwa wanawake, na pengine hata kifo .http://kaluse.blogspot.se/
   
 2. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #2
  Aug 28, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  haya mzizimkavu lakini fumanizi usiombe likukute ni aibu ni fedheha na siwezikuelezea kwa hisia maana inauma sana kama mkeo au mmeo unamfumani
   
Loading...