Fumanizi-mwanaume anapokuwa Kijogoo na mwanamke kahaba……….! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fumanizi-mwanaume anapokuwa Kijogoo na mwanamke kahaba……….!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Mar 5, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Mar 5, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Wanaume wengi huwachukulia wanawake kama mali zao, ambazo ni wao tu wanaotakiwa kuzimiliki kwa namna fulani. Mali yako ni mali yako, ikitumiwa na mtu mwingine, huumiza hisia. Lakini, mali hii inayoitwa mwanamke, mbona ina utambuzi wake? Kila wakati ukisoma kuhusu mauaji ya wivu wa kimapenzi, wanawake ndio ambao wanauawa zaidi. Lakini ukija kusoma takwimu za wanaotoka nje, wanaume ndio wanaotoka kwa kiwango cha juu sana. Kama ni kuuawa, bila shaka wanawake wangekuwa wanawaua wanaume kila siku. Hata ukiangalia kwenye fumanizi nyingi, utashangaa kuona nguvu inapelekwa kwa wanawake, badala ya wote waliofumaniwa.

  Inaonekana kama anayefumaniwa ni mwanamke, yeye ndiye ambaye ametia aibu, na huonekana kama kahaba. Mwanaume ni mara chache sana kukumbana na misukosuko ya fumanizi, hasa kutoka kwa jamii, kwa sababu huonekana kijogoo.

  Kwa nini unadhani hali iko hivyo, wakati mwanaume ndiye mtokaji nje mzuri?

  Ni kwa sababu wanaume hujawa na wivu zaidi pale suala linapohusu mwili kuliko hisia. Wataalamu wanasema, mwanaume anapofikiria kuhusu kumfumania mke au mpenzi wake, picha zinazoenda kwenye mawazo yake ni zile zenye kuhusu mwili. Atatengeneza picha za mkewe au mpenzi wake na huyo mwanaume wakiwa pamoja kwenye tendo. Ataona kila kitu ambacho hufanya na mkewe kikiwa kinafanywa na mtu huyo na pengine ataona ziada. Lakini, picha zote zitakuwa zinahusu shughuli za kimwili.Lakini kwa mwanamke picha zitakuwa ni za mwili, lakini pia za kujali.

  Mwanamke atafikiria au kujenga picha kwamba, mumewe au mpenzi wake ameenda shopping na huyo hawara na anamnunulia vitu vya thamani. Halafu atajenga picha wakiwa pamoja wakiwa wanazungmza kwa furaha na bashasha. Mwanamke huona wivu kimwili na hisia.

  Tafiti zinaonesha kwamba, vipigo na vifo vingi dhidi ya wanawake kutoka kwa wapenzi wao hutokana na wivu. Kwa hali hiyo, wivu unaongoza katika kusababisha maumivu ya kimwili na hisia kwa wanawake, na pengine hata kifo………………...
   
 2. Analogia Malenga

  Analogia Malenga JF-Expert Member

  #2
  Mar 5, 2012
  Joined: Feb 24, 2012
  Messages: 1,093
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  mwanamke kaolewa let her be used. Prove me wrong
   
 3. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #3
  Mar 5, 2012
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Dah na si kuoana?
   
 4. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #4
  Mar 5, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Loh! asara yako usojua thamani ya mwanamke.
   
 5. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #5
  Mar 5, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Unko nimekuelewa sana hapo na ujumbe umefika...
   
 6. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #6
  Mar 5, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Unachosema ni kweli, ila kwa kuongezea ni kwamba kwa hali ya sasa ilivyo hata wanawake pia huona wivu kama wanaume na pengine zaidi ya wanaume. Kwa miaka ya karibuni, tumeshuhudia wanawake kadhaa wakiwauwa wanaume baada ya kuwafumania na wengine, tena wenye ndoa wamediriki kuua mpaka hawala wa hawala yake!
  Kama unakumbuka vzr kuna mada nyingi tu zimepostiwa humu jamvini kuhusiana na mambo haya.

  Ila kwa maoni binafsi, kufumania kunaumiza sana na wala hakuna mtu duniani popote ambaye angependa kuona anasalitiwa. Cha msingi kwa sasa ni kujitahidi kuwa wakweli na waaminifu kwa wenzetu ila kuondoa picha hizi mbaya ndani ya Jamii.

  Ni mtazamo tu nawawakilishia ndugu zangu.

  HP
   
Loading...