Full time: Robo fainali Klabu Bingwa Afrika: Simba SC 3-0 Kaizer Chiefs | Benjamin Mkapa National Stadium - Mei 22, 2021

Joseverest

JF-Expert Member
Sep 25, 2013
51,937
69,220
Naaaaaaam Barabara kabisa...

Karibuni wapendwa wanamichezo katika mpambano wa kukata na shoka kati ya Simba ya Tanzania dhidi ya Kaizer chiefs ya Afrika Kusini, mechi hii ni ya mkondo wa pili baada ya ile ya kwanza kuchezwa Afrika kusini jumamosi iliopita 15/5/2021 ambapo Matokeo yalikuwa Kaizer chiefs 4 Simba 0, Kimahesabu Simba ili afuzu anatakiwa ashinde goal 5 bila ili afuzu

Muda wa mechi ni Saa 10 jioni kwa saa za Tanzania na saa 9 alasiri kwa Saa za Africa kusini.. Dimba ni pale "Kwa Mkapa Taifa"

Je Simba atapindua meza kibabe? Au Kaizer Chiefs watafanya Remix tena na kusonga mbele? Au ngoma itakuwa droo?

*Uzi huu utakuwa updated (Utahuishwa) kadiri muda unavyoenda na matukio yanayotokea

Updates:i)COVID 19 PROTOCOLS Mashabiki wameambiwa ni lazima kuingia na Barakoa, pia kuwe na Social distancing kukaa kwenye viti nafasi wazi ya viti vitatu iachwe, wakati huohuo wameambiwa wawahi tiketi mapema kuepusha usumbufu

Idadi ya mashabiki ni 10,000 tu ndio walioruhusiwa

ii) Televisheni za kuonesha mpira huu
ZBC 2 kupitia kisimbuzi/king'amuzi cha Azam Tv
KBC TV kupitia kisimbuzi cha DSTV channel namba 270


===================================================

VIKOSI VYA TIMU ZOTE/ Starting XI/Lineups

Simba SC

1. Manula Aishi
2. Kapombe Shomari
3. Hussein Mohamed Zimbwe Jr
4. Onyango Joash
5. Wawa Paschal Sergi
6. Lwanga Thadeo
7. Chama Cleotus
8. Mzamiru Yasin
9. Bocco John (Captain)
10. Mugalu Kope Chris
11. Miquissone Luis

Reserve/Sub: B.Kakolanya E. Nyoni, Kennedy J., S.Ndemla, B.Morisson, A.Miraji, M.Kagere, R.Bwalya Kahata F.

Head Coach: Didier Gomes DaRosa


KAIZER CHIEFS Starting XI/Lineup

Kaizer Chiefs lineup:

1.Bruce Bvuma (GK)
2.Siyabonga Ngezana
3.Daniel Cardoso
4.Erick Mathoho
5.Philani Zulu
6.Njabulo Blom
7.Reeve Frosler
8.Lebogang Manyama
9.Bernard Parker (C)
10.Samir Nurkovic
11.Leonardo Castro

#TotalCAFCL #SSCKCFC

SUBs: Akpeyi, Mphahlele, Agay, Baccus, Kambole, Katsande, Ngcobo, Mashiane, Sasman

Head Coach: Gavin Hunt


-----------------------------------------------------------------------------------------------
*FOR ENGLISH AUDIENCE, THIS IS A SHORT PREVIEW

CAF CHAMPIONS LEAGUE, QUARTER FINAL SECOND LEG

SIMBA VS. KAIZER CHIEFS

The battle to secure a spot in the last four of Africa's premier club competition resumes between Amakhosi and the Reds of Msimbazi

Kaizer Chiefs will be looking to complete their march into the Caf Champions League semi-finals while Simba SC are keen to perform a big comeback when the two sides meet in a quarter-final, second leg match at Benjamin Mkapa National Stadium on Saturday.

Following Chiefs 4-0 victory in the first leg seven days ago, they carry a huge advantage going into this clash in Dar es Salaam.

But Simba have previously overturned a 4-0 deficit in this competition and would be confident of doing that again.

Chiefs are seeking to continue making history in this competition by getting into the semi-finals for the first time ever while Simba reached the last four of the 1974 edition when the tournament was still known as the African Cup of Champions Clubs.
Game Simba SC vs Kaizer Chiefs
Date Saturday, May 22-2021
Time 15:00 SA Time

TV Channel, Live Score & How To Watch

Online StreamingTV Channelhttps://www.facebook.com/CAFCLCC

Squads & Team News

Simba will be without midfielder Jonas Mkude who has been given permission by coach Didier Gomes Da Rosa to deal with private matters.
No Simba player is suspended for Saturday's match. Da Rosa would be banking on the likes of Cletous Chama, John Bocco, Erasto Nyoni, Luis Miquissone and veteran attacker Medie Kagere to lead a huge comeback.

Amakhosi welcome back goalkeeper Itumeleng Khune who has recovered from a shoulder injury which saw him miss the last four matches across all competitions.
Khune's return completes their goalkeeping department which was hit by injuries in recent games.
The Soweto giants traveled to Tanzania without Dumisani Zuma who was injured in the first leg against Simba.
He lasted 35 minutes of the match at FNB Stadium and was replaced by Leonardo Castro who went on to score one of Chiefs' four goals.
Zimbabwean attacker Khama Billiat remains out injured with a fractured leg which could see him fail to recover before the end of the season.

Match Preview

It will be the first time for Chiefs to play a match inside a stadium with fans since March 2020.
That makes Simba bank on their supporters to create an intimidating atmosphere which could contribute to Chiefs crumbling.
The Tanzanians have not lost at home in the Champions League this season and they have put to the sword the likes of Al Ahly and AS Vita at Benjamin Mkapa.
In five games they have played in Dar es Salaam since the preliminary round this term, Simba have scored 12 goals and conceded just once.
On two occasions, they scored four goals when they beat Zimbabwean champions FC Platinum 4-0, before thrashing AS Vita 4-1 and those results might be worrisome for Chiefs.
That could give Simba confidence of a successful comeback as they need to win 4-0 and force the contest into a penalty shootout, or a 5-0 victory.
They have previously overturned a 4-0 defeat in this competition and it still stands as a 42-year comeback record in the Champions League.
The Reds of Msimbazi lost 4-0 away at Mufulira Wanderers in Zambia in the 1979 first round, first leg but turned the tables with a 5-0 victory in the home leg to progress to the second round.
Chiefs will be trying to avoid this as they return to East Africa to play a Champions League match for the first time since 1993.

Article continues below

The last time they were in this part of the continent in this competition was when they visited Rwandan club Kiyovu Sports in Kigali in March 1993.

Full Time results: Simba 3 Kaizer Chiefs 0
Bocco
Chama

----------------------------------------------------------------------------------------------

Kuwa nami kuanzia mwanzo mpaka mwishoView attachment 1793902
kcfcofficial-20210522-0001.jpg


00' +1 Mpira umeanza kwa kasi, Simba wanashambulia goli wanapata kona inaokolewa. Simba wanapata kona ya mapema lakini inashindwa kuzaa matokeo

03' Muzamiru Yassin anaachia mkwaju lakini unapaa juuuu


05' Simba wanapata kona tena inadakwa na kipa huku


07' Konde Boy anajaribu lakini mpira unakuwa hauna madhara

08' Kaizer Chiefs wanashambulia hapa ila mpira unakuwa mkuuubwa nje.

10'Castro anawekwa chini na Lwanga Thadeo..anaumia

13,Shomari kapombe anafanya juhudi binafsi paleee aaah inadakwa


16' Mugalu anawahadaa mabeki pale anapiga shuti linapaa nje huko

22' Kona kwa Kaizer Chiefs.. inapigwa na Parker... john bocco anaokoa

23' Goooooooaaaal John bocco anafunga kwa Simba


25' Mpira umechangamka... morison anaingia kuchukua nafasi ya Mzamiru


30'Simba wanashambulia hapa ila Miquissone anatoa nje inakuwa Goal Kick, wakati hùo Onyango,Lwanga, Nurkovic wako chini mpira umesimama

35' Sub kwa Simba Thadeo Lwanga out Erasto Nyoni In

37' Sub tena kwa Simba Joash Onyango Out Kennedy Juma In

40' Miquissone anashambulia hapa nini pale... Simba wanakosa goli la wazi kabisa aaaah

Simba 1 Kaiser Chief 0

43' Simba wanashambulia pale tena..Chama anatoa nje mpira ule kwa kukosa umakini


45' Dakika 6 za nyongeza kuelekea Halftime

45+2' Simba wanapata kona, inapigwa inaokolewa Simba wanaipata tena.. Erasto Nyoni anabutua nje kule Goalkick

45+4' Kaizer Chiefa wanaonana hapa Parker anaingiza ndani kule lango la Simba hamna mtu pale daah

45+5' Morisson anashambulia pale, nini pale anajiangusha refa anakataa, Yellow card kwa Benard Morisson

45+6' Halftime Simba 1 Kaizer Chiefs 0


Second Half inaanza

45' Sub kwa Kaizer ChiefYagaan Saasman kaingia Philan Zulu Nje...

46' Morisson anashambulia anaingiza mpira kule Mugalu anacheza faulo

47' Castro anakosa goli hapa mpira unaenda nje


48' Mugalu anapiga shuti pale kipa Bvuma anadaka...anatoa mpira nje kuashiria ameumia...

50' Kadi ya njano kwa kipa wa Kaizer chief Bruce Bvuma

52' Offside Simba wanazidi langoni mwa Kaizer Chiefs

53' Nurkovic yupo chini , Erasto Nyoni kadi ya Njano

54' Simba wanapata kona, inaingizwa ndani tena... Kona... Chama anapiga shuti kuuubwa nje


56' Goaaaaal John Bocco tena anaifungia simba

57' Sub kwa kai Willard Katsabde ndani Nurkovic nje

Antony Akumu ndani, Manyama nje


60' Mpira umechangamka hapa , Kaizer chiefs wanatoa mpira nje ..inakuwa wa kurusha

65' simba wanashambulia lango la Kaizer Chiefs Kapombe anamwaga maji pale ila Bocco anacheza faulo

67' Kaizer Chief wanapata nafasi pale wanashindwa kuitumia...wakati huo Blom yuko chini


68' Simba wanapata kona inapigwa ila haina madhara...

71' Sub kwa Kaizer Chiefs Kerin Baccus, Njabulo Blom nje

73' Mugalu anapiga mpira laini pale Goalkeeper anaudaka

75' Kaizer Chiefs wanashambulia lango la Simba... Kona pale inapigwa na Parker... inapigwa shuti paleee nje

77' Kona kwa Kaizer Chiefs, Parker anaingiza kona inaokolewa inakuwa kona Dotto. Kona tena inaingizwa ndani...Kona ya tatu wanapata inaingizwa wanaokoa..Morisson anakimbiliaaa anaupiga lakini kipa anadaka

Simba 2 Kaizer Chief 0 Dakika 33 kipindi cha pili

80' Simba wanapiga shuti inagongwa mwamba pale.daaaah

Morisson anapiga pale kona.. inaokolewa inakuwa kona ingine... inapigwa kona tena.. Wawa.. anashambulia pale kipa anadaka hatari pale


85' Timu zinashambuliana kwa zamu hapa, Kaizer Chiefs wamerudi nyuma hapa


86. GOAAAAAAL CHAMA ANAFUNGA

88' Anaingia Ramalwe Mfalele anatoka Davido Castro

SIMBA 3 KAIZER CHIEFS 0

90' Dakika 5 za nyongeza

90+1' Simba wanapaisha Shuti kuuuubwa nje

90+3'Offside John Bocco


90+5' Mpira umeishaaaaaaaaaaa

FT: SIMBA 3 KAIZER CHIEFS O

AGGREGATE SCORE Simba 3 - Kaizer Chiefs 4

Kaizer Chiefs wanafuzu nuzu fainali ya Klabu Bingwa barani Africa


Simba anatoka katika hatua ya Robo fainali pamoja na kushinda 3 bila
 

Chiefs One Foot In The Semifinals | Tso Vilakazi Predictions


Second leg of CAF champion league match in Dar es Salaam, Tanzania between Simba SC vs Kaizer Chiefs
iDisk TV
 
Back
Top Bottom