Kagera 0-2 Simba | VPL | Kaitaba Stadium - April 21, 2021

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Bara Vodacom Premier League VPL' kuvurumishwa leo Aprili 21, 2021 ambapo Kagera Sugar wanacheza na Mnyama Mkali Kuliko Wote Mwituni, Mabingwa wa Nchi, Simba SC kwenye uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba.

Kila timu imejiandaa kuweza kushinda na kujikusanyia alama tatu muhimu ili kuweza kujiweka sawa kwenye msimamo wa VPL, ambapo Kagera Sugar wanashika nafasi ya 14 wakiwa na alama 27 huku Simba SC wakishika nafasi ya 2 kwa alama 52.

Kocha wa Kagera Sugar Francis Baraza anasema mchezo utakuwa mgumu lakini anachotaka ni ushindi ili kujinasua nafasi ya chini.

Naye Kocha Didier Gomes amesema anafahamu ushindani utakuwepo katika mechi hiyo kutokana na wapinzani walivyo lakini kwa maandalizi waliofanya wataondoka na alama tatu.

Kumbuka mtanange huu ni kuanzia saa 10: 00 jioni. Usikose Ukasimuliwa

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana

••••

Wakati wowote mpira utaanza. Timu zote mbili zipo uwanjani zikifanyiwa ukaguzi, salamu pamoja na kupiga picha za kumbukumbu.

Naaaam mpira umeanza ni vita vya VPL'

05' Mpira umeanza kwa kasi huku Simba SC wakimiliki zaidi mpira kwa mashambulizi makali ambayo hayakuzaa matunda kuelekea upande wa Kagera Sugar.

10' Kwakweli mpira una kasi huku Simba wakijaribu kupenya lango, na Kagera akijibu kwa kutumia mipira ya kustukiza lango la simba.

12' Miquissone Goooooooooooooaal Gooooal

Luis Miquissone anaipatia Simba SC bao la kwanza akipokea pasi safi kutoka kwa Chama.

Kagera Sugar 0-1 Simba SC

20' Kagera Sugar wanashika dimba, Abdallah Mfuko anapiga shutiiiiii golikipa Manula anadaka bila wasiwasi.

23' Mugalu Goooooooooooooaal Gooooal

Kope Mutshimba Mugalu anaipatia Simba SC bao la pili akipokea pasi safi kutoka kwa Dilunga

Kagera Sugar 0-2 Simba SC

Kasi imepungua hasa kipindi hiki kuelekea kuwa mapumziko, timu zote.

45+2' Anapiga shutiiiiii loooooo golikipa unamngonga na kurudi uwanjani, ilikuwa hatari sana lango la Kagera.


Naaaam mpira ni mapumziko ambapo Simba wapo mbele kwa mabao mawili kwa bila dhidi ya Kagera Sugar

HT, VPL; Kagera Sugar 0-2 Simba SC.

Kipindi cha pili kimeanza uwanja wa Kaitaba.

Kagera Sugar wakifanya mabadiliko, ametoka Abdallah Mfuko na ameingia Mwaterema.

52' Yusuf Mhilu anapiga shutiiiiii linatoka nje ya lango la Simba SC, ilikuwa nafasi bomba kwa Kagera.

59' Mwaterema anaonyesha Kadi ya Njano baada ya kumfanyia madhambi Miquissone.

Ametoka Dilunga na ameingia Rally Bwalya upande wa Simba SC.

Timu zinacheza kwa tahadhari kipindi hiki cha pili. Ametoka Mwalyanzi na ameingia Nanguo upande wa Kagera.

73' Ametoka Mugalu na ameingia Kagere upande wa Simba SC.

83' Kagere kwake Chamaaa loooooo.. golikipa anatema shuti lile na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda

Kagera Sugar 0-2 Simba SC

Ametoka Mzamir na nafasi yake imechukuliwa na Nyoni upande wa Simba SC.

Kadi za njano kwa Taddeo, Miquissone upande wa Simba SC.

90+4' kuelekea kumalizika kwa mchezo huu wa VPL

Naaaam mpira umekwishaaa ambapo Simba SC wanaibuka na ushindi wa mabao mawili kwa bila dhidi ya Kagera Sugar.

FT, VPL: Kagera Sugar 0-2 Simba SC

Ghazwat
 
Kikosi full: dilunga ajitutumue zipatikane 3 goals first half
Screenshot_20210421-151039_Instagram.jpg
 
Timu ya soka ya Kagera leo inaikaribisha Simba uwanja wa Kaitaba, Kagera inaingia kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara utakaoanza saa kumi kamili. Kagera Sugar inaingia mchezo wa leo ikiwa haina ushindi katika michezo mitano iliyopita huku ikiwa nafasi ya tano kutoka mkiani. Ni vita ya kulikwepa daraja dhidi ya vita ya kufukuzia ubingwa. Kuwa nami kukujuza yatakayojiri.

==========
 
Daaah Mugalu awe bora makosa yake yasijirudie tena natumai kajifunza
 
Naaaam mpira umeanza uwanja Kaitaba Vodacom Premier League VPL'

03' Kagera Sugar 0-0 Simba SC
 
Back
Top Bottom