Full Text: Ripoti ya PAC Bungeni kuhusu Tegeta Escrow Account

Kwa nini report ya PAC haijataja wamiliki wa makampuni mbalimbali yaliyohusika na wizi huu? Mimi nilitaka kusikia wamiliki wa PAP

Mkuu nadhani hukusikiliza vizuri, kamati imemtaja mmiliki wa PAP. Hebu nenda ITV faster ngoma ndo inarudiwa sasa ili ujiridhishe.
 
Wakiteuliwa hufanya sherehe za kupongezana kwa sababu wanajua wazi wanapata fursa ya kwenda kuiba ela za umma ili kujitajirisha. Watanzania huu sio wakati wa kuwaachia wanasiasa pekee jambo hili, tusimame wenyewe kuhakikisha kwamba tunatumia nafasi hii kuwatia adabu.
Tukibaki kuwaachia wanasiasa wataishia kubanana kwenye bunge mwisho, livunjwa baraza la Mawaziri na kutuletea wezi wapya ambao baada ya miaka miwili au mitatu wanakuja kutuibia tena huku nchi ikiendelea kuwa masikini kiasi cha kushindwa hata kutibia wananchi wake.
Wameshatuzoea kuwa tunapiga kelele sana jambo linapotokea kisha ukishapita muda fulani basi kila kitu kinasahaulika na maisha yanaendelea, hii tabia lazima tuachane nayo kama tunataka kuleta nidhamu kwa viongozi wetu ambao wengi wao wamejawa na ubinafsi.
Pinda hakuwa wa kusubiriwa ang'atuke kwa kashfa hii, bali ilikuwa aondoke siku nyingi alipotaka wananchi wachukue sheria mkononi dhidi ya wauaji wa walemavu wa ngozi, na bado akasema uogo bungeni juu ya vurugu za Arusha zilizosababisha vifo.
Isitoshe, Pinda huyo huyo ameagiza Polisi wawapige raia. Tulihitaji nini kwa Waziri Mkuu mbovu na asiyejua kutumia mamlaka yake kama huyu? Tujiulize zile sahihi 70 za Zitto Kabwe za kutokuiwa na imani naye ziliishia wapi licha ya kunekana kuungwa mkono na Wabunge wengi wa chama tawala?
Tusimamie hii nchi, hawa viongozi hawana huruma na hii zaidi wako madarakani kutuvizia watubie tu. Jiulize Muhongo ana muda gani tangu awe kwenye ile Wizara? Ona alivyoamua kibabe kugawa vitalu vya gesi kabla ya ruhusa rasmi ya serikali na akawa akileta lugha za kejeli kwa Watanzania kwenye biashara ya gesi, simiani kama hakupewa rushwa.
Leo kangi Lugola anaweka wapi sura yake? Alidhalilisha Wabunge katika Bunge lililopita kuwa nyaraka walizonazo juu ya kashfa hii ni makaratasi tu ya kufungia vitumbua. Alishapewa rushwa, huku akisukumwa na nguvu ya ukabila kwa Muhongo. Akajitoa fahamu na kujiweka upande wa serikali kwa kuwajibu Wabunge.
Tuwatie adabu hawa watu jamani, wanatudharau sana. Usiku na mchana tunahangaika kusaka kipato chetu kwa jasho kwa kusafiri kila pembe ya dunia ili mambo yaende, lakini kuna mijizi imekaa tu kwenye ofisi za serikali inawaza kuiba pesa za umma ili kujitajirisha. Wanakera sana.
Ova
 
JF kwa sasa haina tofauti na CCM kama madai ya Jaji Warioba yana ukweli...kuna JF imani na kuna JF maslahi. Watu wale wale waliotuomba tuvute subira tusubiri ripoti wakidai ni nyeupee na haina chochote, bila hata chembe cha aibu leo wanajitokeza kivingine kuwatetea wezi waliokubuhu ambao ama ni wazazi wao, viongozi wao, wenzi wao, ndugu zao, rafiki zao au washikaji wao kwa kuumbuliwa na hiyo ripoti. Wonders will never cease!
 
CHADEMA kaeni chini na Zitto mzungumze yaishe!!Makosa yake yanazungumzika mbona?

Kuivua nguo serikali kiasi hiki na kulinda ripoti yao isiibiwe usiku kucha sio jambo rahisi!!Zitto ni MWANAMAPINDUZI
Zitto ni mwizi,tapeli,msaliti na majina yote mabaya unaweza kumwita.
 
Mwandosya confirmed kutoka kwa Mtu wa Ndani wa Jumba Jeupe Magogoni!,ndo Waziri Mkuu Mpya kuanzia kesho Rasmi
 
mtu anauliza kuna tofauti gani kati ya mwizi, kibaka na jambazi! ndg zangu kuhonga ni kuhonga tu alie honga ndege, nyumba, gari na alie honga voucher ya mia tano wote ni WAHONGAJI.
yote mijizi hiyo from nowhere mtu akupe 1.6kindugu tuu! bwana kigumu nae kama jina lake kavuta 80m sasa sijui kwa niaba au mpunga wote wake.
 
Hivi weeeewe nini hujaelewa hapa? Muhongo ndio alikuwa kuwadi

We umeelewa vizuri au unafuata ngoma usiyoijua?

ngoja nikusaidie, Ni hivi dada, Muhongo kaingia Wizara ya Nishati na Madini kakuta kuna mivutano isiyoisha kati ya Tanesco na IPTL, na IPTL na VIP, kabla ya mzigo wa ESCROW kutoka watu walikuwa wanapiga hela kila siku Hapo Tanesco mara body, mara vikao, mara kesi, Na wakili Mkono ndio alikuwa anapigia Pesa hapo, Muhingo kama waziri akaamua asafishe uchafu Tanesco ikiwa ni pamoja na kuzimaliza kesi zote
Na hili kuzimaliza kesi zote ilibidi IPTL na VIP wakutane, na Muhongo ndio alifacilitate hao wakutane na wamalize tofauti zao ili Tanesco iwe free

sasa hapo tatizo la Muhingo liko wapi? Katika list uliyonayo Muhongo kapiga ngapi?
 
We kilaza umeniquote hapo juu nikimcheka bibi mwenzako Faizafoxy alivokuwa anakejeli watu Wanataka Umeme wa bure, huajnielewa kilaza ukadhani nasapoti wizi wenu, Boya ww

Huelewi kuwa Zitto katia nchi mkenge, malipo sasa mara mbili au zaidi.

subiri uone.
 
Furaha yangu haijatimilika mpaka Mtoto Wa mkulima na wenzake wawajibishwe na kupelekwa mahakamani.Teh teh teh wapi Msalani.

Msalani hawezi kuja hapa leo. Hata Mwanakijiji, Pasco, Salary Slip wameingia mitini.
Wamebaki roho za paka tu kina Faizafoxy na Ritz lakini nao wapowapo tu tia maji tia maji.
 
Bila shaka ulipokuwa shule ulikuwa unapigwa sana kwa uelewa wako mdogo na bado ulimaliza miaka yako ya kuwa shule bado ukiwa na uelewa mdogo. Unastahili uendelee kuchapwa viboko sana ili ubongo wako uamke.

Ungenielewesha kuliko kuniattack..kama wewe umeelewa..basi nipe ufafanuzi..its just that simple. Hapa mie naona kuna yaliyojificha na sisi tunashabikia tusichokijua
 
Gemu mbichi sana kesho watoto wa kiume ndiyo wanashuka uwanjani leo walikuwa wanazungumza wavulana kesho ndiyo wanaongea wanaume sasa.

Afadhali km mmejiandaa kiakili kuwa game bado mbichi.Kesho Wanaume Halisi wanaingia mzigoni,maccm lazima mkae!Mnaowalamba miguu lazima tuwafurushe,wakafuge nyuki na kuchunga ng'ombe!
 
Habari za jioni watanzania wenzangu!
Poleni na siku nzima ya leo ambayo kama taifa tumepitia wakati mgumu sanaaa!
Napenda kuwapongeza wale wote walioiibua hii kashfa ya escrow,pia pongezi ziende kwa kafulila kwan alisimama kkidete pale bungeni ili kudai pesa hizi zirudishwe! Kamati ya PAC pongezi nyingi sana mmefanya kazi nzito mbarikiwe na tumetambua mchango wenu! Kulinda ripoti kwa usiku mzima pale bungeni si kazi ndogo,kizazi cha wazalendo kitawakumbuka daima!
Mm binafsi nimesikitishwa sanaa na yote niliyoyasikia kutoka kwenye kamati ya PAC! Hivi kweli nchi hii ina uongozi wa kidemokrasia?kweli watu wanagawana pesa kama wanagawana peremende?hivi kweli watu wamekosa uzalendo kiasi hiki?nimetokwa na machozi kweli kabisa! Lkn mm najiuliza hivi kweli hakuna alielijua hili na kuchukua hatua mpaka lipigiwe kelele bungeni?nina maswali mengi mnoo lkn labda majibu yatapatikana kesho ripoti hii itakapojadiliwa bungeni!
Mm naomba kama taifa kuna haja ya kujua wajibu wetu! Na ni wakati muafaka wa viongozi woote kujitathmin kama kweli wanastahili kuendelea kushikilia nyadhifa zao!
Nataman kusema mengi lkn nina uchungu mnoo naona nitaandika hata yasiyofaa! Mm kama mwananchi mzalendo kabisa na ambae nataka kuhakikisha kuwa mafisadi hawaendelei kuitesa nchi yetu,basi naanza kuchukua hatua kwanza kwa kujiandikisha ili nichague kiongozi wangu wa serikali ya mtaa anaefaa,pia panapo majaliwa hapo mwakani nitaonyesha uzalendo wangu kwa kupiga kura kuwachagua viongozi wasio na chembe ya ufisadi! Tutaonana kwenye karatasi ya kupigia kura! Lkn pia nitakuwa mjumbe mwema wa kuwakataa wazi wazi mafisadi na wanyonyaji wa nchi yetu!
 
We umeelewa vizuri au unafuata ngoma usiyoijua?

ngoja nikusaidie, Ni hivi dada, Muhongo kaingia Wizara ya Nishati na Madini kakuta kuna mivutano isiyoisha kati ya Tanesco na IPTL, na IPTL na VIP, kabla ya mzigo wa ESCROW kutoka watu walikuwa wanapiga hela kila siku Hapo Tanesco mara body, mara vikao, mara kesi, Na wakili Mkono ndio alikuwa anapigia Pesa hapo, Muhingo kama waziri akaamua asafishe uchafu Tanesco ikiwa ni pamoja na kuzimaliza kesi zote
Na hili kuzimaliza kesi zote ilibidi IPTL na VIP wakutane, na Muhongo ndio alifacilitate hao wakutane na wamalize tofauti zao ili Tanesco iwe free

sasa hapo tatizo la Muhingo liko wapi? Katika list uliyonayo Muhongo kapiga ngapi?

Muhongo ndo tapeli namba wani kwa kumleta singa singa bila kuwa na ushahidi kuwa singasinga ndo kweli mmiliki halali wa IPTL. Muhongo alijua kila kitu ndo maana siku zote yeye aligeuka PR wa singa singa kwa kutetea kuwa fedha ya escrow ni private money. Kuna mambo mengine kuyarudia rudia ni ujinga tu. Nadhani huo utetezi mtautoa mahakamani sababu si mmenunua majaji eee. Mtaenda kupambana na ma - auditor waliokagua huko mahakamani. Hapa mtuache tukusanye vipande vya nchi yetu vilivyobaki baada ya ninyi na magenge yenu kutaka kuisambaratisha!
 
Back
Top Bottom