Ubungoubungo
JF-Expert Member
- Jul 28, 2008
- 2,502
- 739
Jamani, kulikuwa na hotuba ya kikwete nimeona kwenye itv leo jioni, sijui ilikuwa imerecodiwa lini, ila alichosema pamoja na mambo mengine, kabla ya kumaliza ni kwamba, SISI WATZ HATUNA UBAVU KUINGIA VITANI SASAIVI KAMA ZILIVYO NCHI ZINGINE...hii ni kauli toka kwa rais wa nchi kubwa kama tz....hakuna rais ambaye nilishawahi kumsikia tangu nizaliwa, akisema kuwa nchi yake haina nguvu kijeshi au jeshi la nchi yake halina nguvu....au halina uwezo kuingia vitani...hata rais banda mwanamke wa malawi hajawai sema hivyo....wenzangu mlimsikia? yawezekana ni kweli tunaye rais dhaifu aisee...pamoja na kwamba alikuwa na nia nzuri na aliongea hotuba nzuri, lakini hakuridhika pale mwishoni akajikuta ameonyesha jinsi alivyo, dhaifu...akakiri kwamba tz hatuna ubavu kuingia vitani na malawi kama zilivyo nchi zingine.