Full Text: Hotuba ya Mch. Msigwa; maliasili na utalii - Upinzani

Kwa mwendo huu, bunge la bajeti lijalo 2012/13 litakuwa tofauti sana. Na hakika ccm/serikali hawakutegemea kibano cha kambi ya upinzani (CHADEMA) kingekuwa kikubwa hivi. Hata yale makelele ya kuwaponda naona nguvu zimeisha maana CHADEMA wameamua kukomaa kwa kuwamwagia data. Na mungu alivyo mkubwa wauza mafuta nao wameiacha serikali na ccm uchi mchana kweupe.

Wamashukuru sana Waziri Mkuu Pinda amejitahidi sana kuwalainisha wabunge wa ccm ili waipe TAFU bajeti za wizara. Lakini mwakani sidhani kama watakubali maana wananchi wameshaamka.
 
Hotuba makini kama hii hata waziri akitolea majibu marahisi kama kawaida yao itabaki kumbukumbu kwa watanzania watakaosoma na kusikiliza. Wajue jinsi nchi inavyoingizwa kwenye umaskini wa kujitakia na viongozi wabovu, wabinafsi na wenye kutanguliza maslahi yao mbele
 
“The value of our dignity in this World will never be determined by what we have accumulated, but rather for what we have contributed."


Well said Mch. Msigwa, Magamba hawalijui hili, wanashindana ku-accumulate....hahahaahhaaa
 
Hotuba haina mbele wala nyuma
Aisee! Naamin kwa mjibu wako hotuba zenye mbele na nyuma ni zili zenye kuwa na maneno kama haya

"...Tuko mbioni,...Tupo kwenye michakato ....Serikali inalichukulia kwa uzito mkubwa suala hili,....mikakati inaendelea kuandaliwa,.... Tumeunda kikosi kazi. Ha ha ha ha safi hiyo. etc
 
Kwakweli hotuba ya mch.msigwa na nyinginezo za Kambi ya upinzani zinaweza kukutoa machozi jamaa wanaonesha umakini mkubwa na uzalendo wa hali ya juu, wanaongea kwa data, hivi watz tunataka nini kama wakombozi wameisha jitokeza.

Jamani lets pray for CHADEMA wachukue nchi mayb watatukomboa kwenye hili dimbwi la umaskini tulionao watz wengi. Mimi nashangaa mtu anayeng'ang'ania ushabki wakati tupo kwenye hali mbaya ya kiuchumi shilingi inazidi kuporomoko zidi ya USD tunaenda wapi jamani, tuache ushabiki tuwe kitu kimoja katika vita ya kuwatoa hawa wanyonyaji MAGAMBAZI.
 
Mchungaji msigwa akitoka huko mjengoni mi ningependa pia atueleze hata kwa kifupi cc wapiga kura wake tangu alivyochukua jimbo japo kwa kipindi kifupi! Amefanya nini?sababu mi binafsi sioni kipya jimboni kwangu!
 
Aisee! Naamin kwa mjibu wako hotuba zenye mbele na nyuma ni zili zenye kuwa na maneno kama haya

"...Tuko mbioni,...Tupo kwenye michakato ....Serikali inalichukulia kwa uzito mkubwa suala hili,....mikakati inaendelea kuandaliwa,.... Tumeunda kikosi kazi. Ha ha ha ha safi hiyo. etc

La kuvunda halina ubani
 
Back
Top Bottom