Full Text: Hotuba ya Edward Lowassa aliyotoa katika Uchangiaji wa Saccos ya CWT na Kukusanya 1.27bn

OgwaluMapesa

JF-Expert Member
May 24, 2008
10,943
428
HOTUBA YA WAZIRI MKUU MSTAAFU MHESHIMIWA EDWARDLOWASSA, MB. KATIKA SIKU YA SACCOS YA WALIMU MOSHI VIJIJINI (MOSHI USHIRIKA STADIUM) TAREHE 14 JUNI 2013




Mwenyekiti wa SACCOS ya Walimu Moshi VijijiniMkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Rais wa CWT Taifa,Wawakilishi wa CWT kutoka Mikoa Yote ya Tanzania Bara,Waheshimiwa Wabunge na Waheshimiwa Madiwani,Viongozi wa Serikali na Vyama vya Siasa,Wapendwa Wanachama wa SACCOS ya Walimu Moshi VijijiniWapendwa WanahabariWageni WaaalikwaMabibi na Mabwana Awali ya yote napenda kukushukuru wewe Mwenyekiti nakuwashukuru wanachama wote wa SACCOS ya walimu wa Moshi Vijijini kwa kunialika niwe mgeni rasmi katika tukio hili kubwa na la kihistoria kwa chama chenu.


Nilipoletewa ombi lenu sikusita kulikubali kwa sababu sekta mnayoiendesha na kuisimamia ni sekta iliyo karibu sana na moyo wangu. Bila shaka mnakumbuka kuwa nimekuwa wazi siku zote kwamba njia rahisi ya kuifanya nchi yetu iwe na maendeleo ya haraka ni kwa kuwekeza katika elimu. Mtakumbuka kuwa nilipokuwa Waziri Mkuu tulianza ujenzi wa sekondari katika kata zote za nchi yetu. Kwangu mimi hiyo ilikuwa ni hatua ya kwanza ya kuiletea nchi yetu maendeleo ya haraka na yenye kuleta usawa kwa wengi. Hadi leo naamini kwamba ule ulikuwa ni uamuzi sahihi uliolenga kuwapa vijana wote wa Tanzania elimu kadiri ya uwezo wa kila mmoja wao.Uamuzi huo pia ulikuwa umelenga kuwapunguzia wazazi na wananchi gharama za kusomesha watoto wao kwa kuwa shule za sekondari zilizokuwepo zisingetosha kuendeleza wale waliokuwa wanahitimu na kufaulu katika elimu ya msingi. Natambua kuwa bado kuna changamoto kubwa katika kuboresha shule zetu; lakini huo ni mchakato endelevu na ni wajibu wa serikali, wananchi na wadau wa elimu kwa miaka mingi ijayo.

Ndugu Walimu, Kwa nini nimekuwa nikiweka mkazo sana katika elimu? Tuanze na historia. Katika nchi hii kuna maeneo ambayo wananchi wake walipata elimu enzi za wakoloni kuliko wananchi wa maeneo mengine. Hadi tunapata uhuru maeneo haya yalikuwa mbele kimaendeleo kuliko maeneo ambako mkoloni hakutoa elimu. Kwa maneno mengine, elimu zaidi, maendeleo zaidi, na elimu kidogo, maendeleo kidogo. Ukweli huo unaendelea kubaki kuwa ukweli hadi leo. Tukiweza kutoa elimu bora kwa kila Mtanzania, maendeleo yatamfikia kila Mtanzania, kwa kiwango cha juu na kwa usawa. Elimu bora kwa kila Mtanzania ndiyo njia pekee ya kuondoa tofautiya maendeleo kati ya mtu na mtu na kati ya eneo na eneo ndani yaTaifa letu la Tanzania. Elimu bora itamfanya kila mtanzania aweze kujiamini, kuwasiliana kwa ufasaha, kuwa na maarifa na ujuzi, kuwa na njia za kutatua changamoto,kuwa mbunifu. Vyote hivi vitamsaidia mtanzania kutatua changamoto za kijamii na kiuchumi na hatimae kumsaidia kumletea maendeleo yake binafsi, familia yake, na hatimaye nchi yake. Hiyo ni historia iliyo wazi.

Naomba mniruhusu niende kwenye mifano mingine halisi. Mwaka 1960 nchi ya Korea Kusini ilipata uhuru kutoka kwa Wajapani. Mwaka uliofuata yaani 1961 Tanganyika ikapata uhuru kutoka kwaWaingereza. Mwaka uliofuata wa 1962, Umoja wa Mataifa ukatoa taarifa yake ya Maendeleo ya Mwanadamu (Human Development Report) katika nchi zote zilizokuwa huru wakati huo. Kwa mujibu wakipimo kile, Tanganyika ililingana na Korea Kusini kwa maendeleo. Sote tulikuwa chini kabisa katika jedwali la nchi za dunia wakati ule. Kila nchi ikaanza mikakati yake ya kupambana kuwaletea wananchi wake maendeleo. Tanganyika ambayo sasa ni Tanzania tukawa na mipango mingi sana iliyokuwa inashughulika na sekta zote.

Bajeti yetu ikagawanywa kwa namna ambayo kila sekta ilipewa kipaumbele. Bajeti ya elimu aliyoacha mkoloni ya asilimia 20 ikashuka hadi asilimia 2 kipindi fulani, na japokuwa jitihada mbalimbali zimewekwa kwenye elimu, hatujawahi kuzidi asilimia ishirini kwa mwaka. Kule Korea wao waliamua kutoa kipaumbele kwa sekta moja tu, nayo ni elimu. Elimu ikapewa bajeti kubwa kabisa na ikaboreshwa kuanzia chekechea hadi chuo kikuu bila kushusha bajeti yake. Hili likafanyika bila ubabaishaji na bila kujali utashi wa mwanasisa fulani. Na likafanyika miaka yote, siyo mwaka huu kushusha bajeti akitawala kiongozi asiye na mapenzi katika elimu na kuipandisha mwaka unaofuata akitokea kiongozi anayeipenda elimu.Kitu cha kusikitisha zaidi ni kuwa bajeti kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo ya sekta ya elimu imekuwa tegemezi ya asilimia 70 kwa fedha za Wahisani. Jambo la kusikitisha zaidi wahisani wa maendeleo hawatoi fedha zote wanazoahidi ambapo hutoa asilimia kati ya 40-50 tu ya fedha walizoahidi. Bajeti yetu ya maendeleo ya sekta ya elimu kila mwaka haitekelezeki kwa upungufu wa asilimia 30-35. Kwa hali hii tutapataje maendeleo katika sekta ya elimu?Hapa pia nitoe mfano ambao tunaweza kujifunza toka kwa majirani zetu Kenya na Uganda. Kenya inatumia fedha zake za ndani kwa ajili ya bajeti ya maendeleo ya sekta ya elimu na hii imewezeshakutekeleza bajeti ya maendeleo kwa asilimia 96. Pia Uganda inatumia fedha za ndani kwa Bajeti ya maendeleo ya elimu ya msingi, sekondari na elimu ya juu.

Matokeo ya sera hizi mbili tofauti ni nini? Mwaka 2010, Taarifa ya Maendeleo ya Shirika la Maendeleo laUmoja wa Mataifa (UNDP Report) iliyokuwa imepima kiwango cha maendeleo ya nchi 172 za dunia iliipanga Tanzania kuwa nchi ya 153kati ya nchi hizo 172. Korea Kusini ilipangwa kuwa nchi ya 11 kwa maendeleo duniani kati ya nchi hizo 172. Kwa mfano, wastani wakipato cha Mtanzania mmoja mwaka huo wa 2010 kilikuwa Dola 500 za Kimarekani, wakati wastani wa kipato cha Mkorea mmoja kilikuwaDola 30,000 za Kimarekani, yaani mara 60 ya wastani wa kipato chaMtanzania. Taarifa hiyo iliionesha Tanzania ikiwa imeachwa chini kama ilivyokuwa mwaka 1962, huku Korea Kusini ikichupa na kuainishwa kuwa moja ya nchi tajiri sana duniani. Kabla ya kujiuliza kwa nini nchi hizi zimetofautiana kiasi hiki, tujikumbushe kuwa Tanzania ina madini mengi na ya aina nyingi,wakati Korea Kusini wanayo kidogo sana. Wana gold, coal na chuma ila ni kidogo sana; na uchimbaji wake uko katika low scale. Tanzania ina ardhi kubwa na nzuri ya kilimo, ukilinganisha na Korea Kusini. Tanzania ina vivutio vingi vya utaliii, Korea Kusini hawana. Tanzania ni mdomo bahari kwa nchi saba zinazotegemea bandari zake na ina majirani wanaoishi nao kwa amani, Korea Kusini ni peninsular yenye jirani mmoja tu anayeitishia kiusalama miongo mingi, yaani Korea Kaskazini. Sasa tofauti hii imesababishwa na nini kati ya nchi hizi mbili? Tofauti hii imesababishwa na elimu. Elimu ndiyo imeifanya Korea ikawa mbele zaidi ya Tanzania katika nyanja zote. Elimu bora ya Korea Kusini imelifanya taifa hilo kuwa bora katika karibu kila Nyanja ya maendeleo. Leo hii Korea Kusini ni taifa lenye viwanda na linaiuzia dunia yote magari ya Hyundai na simu za Samsung wakati Tanzania tumebaki kuuza mazao na raslimali ghafi ambazo zina bei duni katika soko la dunia. Kutokana na jeuri ya elimu, Korea Kusini ni kati ya mataifa yanayotoa madaktari bingwa wa ngazi ya kimataifa, tofauti na Tanzania. Tofauti ni kiwango na aina ya elimu tu. Wataalamu wa uchumi wote Duniani wamebainisha wazi kuwa uzalishaji katika jamii yoyote ile, unategemea rasilimali watu na mtaji"Yaani Production is a function of capital and Labour (human capital i.e skilled labour). Hivyo basi ni lazima tutambue kuwa hatuwezi kuwa na uchumi imara bila elimu iliyo bora yenye kutoa wataalamu makini. Ngoja nitoe mfano wa pili. Katikati ya miaka 1990, kiongozi wa Chama cha Labour cha Uingereza Bw. Tony Blair aliulizwa ajenda zake tatu ambazo zingeisaidia nchi ya Uingereza kujikwamua kiuchumi kwani uchumi wake ulikuwa ukiporomoka kwa kasi. Hayo aliulizwa wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu nchini Uingereza. Bwana Blair alijibu kuwa ajenda yake ya kwanza ni elimu, ya pili ni elimu, na ya tatu ni elimu. Alifafanua kuwa kuwekeza kwenye elimu ndiko kungeuinua uchumi wa Uingereza na si kuwekeza katika sekta nyingine yoyote. Alifafanua kuwa elimu bora ndiyo ingeinua sekta za viwanda, kilimo, uvuvi, utalii, mawasiliano, uchukuzi, na teknohama. Waingereza wakamuamini, wakakipa kura Chama cha Labour na Bwana Blair akawa Waziri Mkuu wa Uingereza kuanzia mwaka 1997. Kama mtakumbuka, katika kipindi cha Bwana Blair uchumi wa Uingereza ulipanda kwa kasi na kuyapiku mataifa mengi ya Ulaya yaliyokuwa yameipiku Uingereza wakati wa Uwaziri Mkuu wa Bwana John Major wa Chama cha Conservative.

Ndugu Mwenyekiti, Leo hii kila mpenda ukweli atakiri kuwa elimu ya Tanzania iko mahututi kiasi cha kuwakatisha wengi tamaa. Kwa mujibu wa takwimu za benki ya Dunia, hivi sasa hali ya ujinga imeongezeka (illiteracy rate). Mwaka 1992 tulikuwa na watanzania asilimia 15 tu wasiojua kusoma na kuandika ilihali hivi sasa tuna watanzania takribani asilimia 31 wasiojua kusoma na kuandika. Tumeshuhudia mwaka 2011 takribani wanafunzi 5000 waliomaliza darasa la saba walifaulu kujiunga kidato cha kwanza ilihali hawajui kusoma na kuandika. Ufaulu kidato cha nne unazidi kushuka mwaka hadi mwaka. Mwaka 2011 wanafunzi asilimia 43.6 walipata darajasifuri na pia mwaka 2012 asilimia 60.1 walipata daraja sifuri (kabla ya matokeo kufutwa). Shule zetu hazifanyiwi ukaguzi. Wastani wa ukaguzi kwa shule za msingi na sekondari ni asilimia 20 ya shule zote kwa mwaka. Mazingira ya kujifunzia na kufundishia si mazuri na hii yote imesababishwa na uwekezaji mdogo wa fedha za maendeleo kwenye sekta ya elimu, lakini pia uwajibikaji hafifu sana. Bajeti ya maendeleo ya sekta ya elimu ya Tanzania imekuwa katika wastani wa asilimia 9-10 ya bajeti nzima ya sekta ya elimu, huku asilimia 90-91 ya bajeti zikitumika kwa matumizi ya kawaida. Kwa majirani zetu Kenya na Uganda wanawekeza zaidi kwenye maendeleo na si matumizi ya kawaida. Bajeti ya maendeleo katika sekta ya elimu kwa nchi ya Uganda ni asilimia kati ya 23-24, na kwa Kenya ni asilimia kati ya 18-20. Lakini nimesimama hapa kuwasihi msikate tama, licha ya changamoto nyingi katika kazi yenu, kwani kazi yenu ni muhimu sana. Na napenda kuifanya kazi hii kwa kuwarudisha nyuma miaka ya 1960 na kuwakumbusha habari za mwanaharakati aliyekuwa mstari wa mbele kupigania haki za watu weusi nchini Marekani, hayati Dr Martin Luther King (Junior).

Katika hotuba yake aliyoitoa katika kilele cha mateso ya watu weusi mwezi August 1963 mjini Washington, King aliwaambia wasikilizaji wake kuwa alikuwa na ndoto kwamba muda si mrefu mateso ya mtu mweusi katika Amerika yangekuwa historia; kwamba baada ya muda mfupi mtoto mweusi na mtoto mweupe wangepata fursa sawa katika Amerika; na kwamba baada ya kitambo kidogo raia yeyote wa Marekani angehukumiwa kwa kazi au mchango wake katika jamii na siyo kwa kufuata rangi ya ngozi yake. Ingawa Dr King aliuawa miaka mitano baadaye yaani mwaka 1968, ndoto yake ilishaanza kutimia mwaka 1965 watu weusi waliporuhusiwa kupiga kura kwa mara ya kwanza nchini Marekani. Ndoto hii ilifika kileleni mwaka 2008 Barack Obama alipochaguliwa kuwa Rais wa Marekani akiwa mtu mweusi wa kwanza kuukwaa wadhifa huo katika taifa hilo kubwa. Leo nasimama mbele yenu na kuwasimulia ndoto yangu kuhusu elimu ya Tanzania siku zijazo.


Ninayo ndoto kuwa siku si nyingi zijazo, elimu itapewa kipaumbele cha kwanza nchini Tanzania, na namuomba Mwenyezi Mungu asiniondoe duniani kabla sijauona utimilifu wa ndoto hii kama Dr King alivyoondolewa kabla hajaiona ndoto yake ikitimia, bali namuombaanipe muda na nguvu niweze kushiriki katika kuifanya ndoto hiyo iwekweli.

Ninayo ndoto kwamba siku si nyingi Watanzania wote, tukianza na sisi viongozi, tutawajibika kwa vitendo na tutakubali kuwa elimu ndiyo inapaswa kupewa kipaumbele cha kwanza na cha juu kabisa katika nchi yetu; tutakubali kuwa elimu bora ndiyo itatupa kilimo bora;tutakubali kuwa elimu bora ndiyo itatuondolea ujenzi holela wa majengo na barabara zetu; tutakubali kuwa elimu bora ndiyoitatusaidia kuumiliki utalii wetu na kunufaika nao badala ya kuwaachia wageni wanufaike nao huku Watanzania tukiambulia makombo; tutakubali kuwa elimu bora ndiyo itaifanya Tanzania iweze kushindana na wenzetu wa Afrika Mashariki na hata kuongoza kiuchumi katika ukanda huu wa Afrika; tutakubali kuwa elimu bora ndiyo itatusaidia tuweze kuchimba madini yetu na kuyauza kwa faida duniani badala ya kuwaachia wageni wayachimbe na kutuachia faida kidogo huku wao wakipata faida kubwa; na tutakubali kuwa ni elimu bora tu ndiyo itaweza kutufanya Watanzania tuache kuwa wategemezi wa kila kitu kwa wageni wakati tunazo kila sababu za kusimama wenyewe na kusimamia maisha yetu na raslimali zetu kwa faida yetu na ya vizazi vijavyo. Haya yote yanawezekana tukiwa na utashi wa kisiasa (political will) na kuamua kwa makusudi kabisa kuwajibika kufanya hali iwe hivyo.

Ninayo ndoto kuwa siku si nyingi, shule za Tanzania zitakuwa na zana bora kabisa za kufundishia, ikiwa ni pamoja na maabara za kisasa na vifaa vyake na mabweni kwa shule zote za sekondari, hatazile za kata. Hii itawafanya watoto wetu wa sekondari watulie shuleni badala ya kutumia nusu ya muda wao wakitembea au kuwinda daladala kwenda shuleni na kurudi nyumbani. Ninayo ndoto kuwa siku si nyingi shule zetu zitakuwa na walimu wa kutosha ambapo uwiano wa mwalimu kwa wanafunzi utakuwa mwalimu 1 wanafunzi 40,uwiano wa darasa kwa wanafunzi utakuwa darasa 1 wanafunzi 40, kila mwanafunzi kukaa kwenye dawati kwa wanafunzi 3 kwa kila dawati,kila mwanafunzi kuwa na kitabu kwa masomo yote, kila shule kuwa na maktaba yenye vitabu.

Lakini ninayo ndoto pia siku moja walimu wote watatambua wajibu na umuhimu wao katika kutoa elimu bora kwa watoto wetu wa kitanzania.

Ninayo Ndoto Sikumoja katika Nchii Hii,hakuna Mtoto wa Kitanzania atakaeshindwa kupata Elimu Bora kwa Sababu Mzazi wake Hana kipato,watoto wote bila kujali vipato AMA vyeo vya wazazi wao watapata Elimu ilyo bora na ubora sawa.Ninaota Siku Moja Shule zote kuwa na Nishati ya uhakika ya Umeme Kama nyenzo muhimu ya kusomea na kufundishia,kwa Umeme wa jua AMA Gridi ya Taifa.Ninaota Shule zote kuwa na maabara za komputa kama nyenzo muhimu ya kufundishia na kusomea na kejenga msingi bora wa kuwa na Dira ya Elimu ya Kujitegemea,ninaota Kama mimi na wenzangu tulivopewa fursa ya kupata elimu Kama huduma muhimu na Taifa hili iliyobora bila wazazi wetu kuwa na Vipato,vivyo hivyo ni Ndoto yangu elimu kuwa ni haki ya Kila mtu Kama ilivyo haki ya kuishi na kuwapatia mazingira bora,nyenzo bora stahiki bora wanaotoa na kufundisha watoto wetu.

Ninayo ndoto kuwa miaka michache ijayo, badala ya watoto waKitanzania kupelekwa nje kuitafuta elimu katika nchi jirani na nyingine duniani, kwa kisingizio kuwa elimu yao ni bora kuliko ya kwetu, watoto wa nchi jirani nasi, wataletwa Tanzania kunufaika na elimu bora itakayokuwa inatolewa hapa Tanzania. Naam, naota kuwa kuna siku hata wazazi kutoka nchi zilizoendelea watawaleta watoto wao Tanzania kusoma kwani suala halitakuwa tena ubora wa elimu, ila labda mambo kama umbali kutoka huko hadi hapa. Ndugu Mwenyekiti, Kuota ni rahisi kuliko kuifanya ndoto iwe na uhalisia. Ili ndoto nzuri iwe halisi sharti iwepo mikakati na nia ya dhati ya kuifanyia ndoto hiyo kazi. Kila ninapoitafakari ndoto yangu hii huwa najiuliza: Itatekelezekaje? Na kwa hatua zipi? Katika tafakuri yangu nimegundua kuwa ukitaka yote haya yafanikiwe, hatua ya kwanza ni kumjali mwalimu. Narudia: hatua ya kwanza ni kumjali mwalimu. Mwalimu mwenye motisha, hata kama anafundisha katika mazingira magumu, ana uwezo wa kufaulisha wanafunzi kuliko mwalimu aliyekata tamaa na anayefundisha katikamazingira mazuri. Kwa sababu hiyo, natoa wito kwetu sisi sote viongozi na Watanzania wote tuanze kuwajali walimu na maslahi yao kama hatua ya kwanza ya kuifanya nchi hii iwe na elimu bora itakayoleta maisha bora. Mimi naamini kuwa tunaweza kutengeneza sera na mitaala bora kabisa nakuunda tume nyingi, lakini kama hatutawajali walimu, elimu bora itaendelea kubaki ndoto Tanzania.


Kuwajali walimu ni pamoja na kuwapa mafunzo kazini. Waweze kujifunza mbinu mbadala za kufundishia, wajue namna mbalimbali za kuwahamasisha wanafunzi kupenda masomo; pia watambue kwa wakati mabadiliko katika jamii zetu na nyanja za kiteknolojia-ili watoe mwanga na ubunifu huo kwa wanafunzi. Ifike mahala sasa turejesheheshima ya mwalimu. Lakini ifike mahali, nanyi walimu muoneshekwa vitendo kuwa taifa hili lina wajibu wa kuwapa heshima hiyo.

Ndugu Mwenyekiti, Si nia yangu kuwachosha na hotuba ndefu, lakini ni muhimu kuanza na historia ili muelewe ni kwa nini leimu ni jambo muhimu sana kwa taifa lolote duniani linalotaka maendeleo. Ni kwa sababu hiyo,naamini kuwa maslahi bora kwa walimu ndio mwanzo wa kuiboresha elimu ya Tanzania, ndiyo maana niko hapa kwenye tukio hili la kuichangia SACCOs hii. Niwapongeze sana wanachama wa SACCOs hii ambao badala ya kulalamika, mmetekeleza kwa vitendo wito alioutoa Rais mmoja kijana wa Marekani aitwaye John Kennedy. Katika hotuba aliyoitoa siku ya kuapishwa kwake tarehe 20 Januari 1961, Kennedy aliwaambia Wamarekani wenzake, na hapa nanukuu: "Ask not what your country can do for you; ask what you can do for your country" Hakika nyie badala ya kuweka nguvu nyingi kuidai nchi iwaboreshee maisha, mmeamua kuweka nguvu zenu zaidi katika kuisaidia nchiyenu.



Na kwa tukio la leo, mmewaonesha walimu wengine nchini kwamba walimu kwa umoja wenu mnao uwezo wa kuifanyia Tanzania yetu jambo la maana mkiamua. Mmeonesha kuwa walimu kwa wingi wenu na umoja wenu mnaweza kuboresha maisha yenu na kuibadili Tanzania. Nawaomba wawakilishi wa walimu mliopo hapa mlipeleke wazo hili zuri kwa walimu wote nchini ili kila wilaya iwe na SACCOS ya walimu wa wilaya hiyo. Mwalimu ni kioo,hufundisha ndani na nje ya darasa, nanyi mmedhihirisha hivyo kwa jitihada hii ya kutafuta njia mbadala ya kuniua kipato chenu badala ya kuridhika na hali ya umskini. Mnatumia kidogo mpatacho kuwekeza katika njia endelevu na ya kuleta tija kwa manufaa ya yenu na familia zenu.Kwa upande wa viongozi wenzangu mliojumuika nami hapa nawaomba sote tuoneshe kuwajali walimu wetu hawa kwa kuanza kuchangia tukio la leo kwa moyo mkuu.



Pili nawaomba popote pale mtakapoenda baada ya tukio la leotuanze kufikiria na kudhamiria kuyaboresha maisha ya walimu wetu kama hatua ya kwanza ya kuiinua sekta ya elimu Tanzania. Viongozi tujiulize kwa nini mwalimu anayeanza kazi leo hapewi chombo cha usafiri lakini bwana shamba anapewa? Tujiulize kwa nini walimuwengi hawapewi nyumba za kuishi lakini wafanyakazi wengine wenye elimu inayolingana nao wanapewa nyumba za kuishi? Tujiulize kwa nini maofisa mbalimbali wa serikali wanapata posho mbalimbali lakini walimu wanaambulia posho wakati wa uchaguzi au sensa tu, na tenasi walimu wote? Tukishajiuliza maswali hayo tusiishie hapo.



Tuchukue hatua ya kuirekebisha hii hali; ili watu wenye uwezo mkubwa kitaaluma nao wavutiwe kuwa walimu. Kazi ya ualimu iweze kupiganiwa na watu wenye ufaulu wa juu kama udaktari na sheria, na ipewe heshima hiyo inayostahili. Sasa natambua kuwa wapo viongozi wenye hofu kuwa kuyaboresha mazingira ya kazi ya walimu si jambo rahisi eti kwa sababu ya wingi wao. Kwa viongozi au watu wanaofikiri hivyo napenda niwakumbushe msemo wa mwanafalsafa mmoja aitwaye Socrates aliyeishi miaka mingi kabla ya Kristo. Yeye aliwashauri viongozi wa taifa lake la Ugiriki waliokuwa wanapata taabu kugawa sehemu ya utajiri wao kuwasaidia raia wao waliokuwa maskini, akiwaambia wasipojitahidi kuyaboresha maisha ya raia wao wengi waliokuwa wanateseka kiuchumi, wao viongozi wachache wasingeweza kufurahia utajiri wao mkubwa kwa sababu hali hiyo ya mgawanyiko wa kiuchumi ilikuwa sawa na bomu lililokuwa linasubiri kulipuka. Kwa maneno yake Plato: "If a free society can not help the many who are poor, it can not save the few who are rich" Naamini kuwa sisi viongozi na Taifa kwa jumla tunapaswa kuiona hiyo kama changamoto, na kujipa wajibu wa kupambana hadi tuishinde changamoto hii ya kuyainua maisha ya walimu wetu. Na ili tuishinde changamoto hii lazima tuondokane na woga. Kila zama,viongozi duniani hupambana na changamoto za aina moja au nyingine, na wanaoweka historia ni wale wanaoamua kuushinda woga.




Niwakumbushe changamoto moja aliyoipata Rais Franklin Roosevelt wa Marekani. Tarehe 8 Desemba 1941 Rais Roosevelt alilazimika kuiingiza Marekani katika Vita Kuu ya Pili ya Dunia baada ya Ujapani kuuvamia mji wao mmoja uitwao Pearl Harbour huko Hawaii. Rais huyu alipambana na baadhi ya Wamarekani waliokuwa na hofu kuwa Marekani na marafiki zake wasingeshinda vita ile kwa sababu ya nguvu kubwa ya maadui zao yaani Ujerumani, Ujapani, naUitaliano. Akiutuliza woga huo, Rais Roosevelt alisema, na hapanamnukuu: "The only thing we have to fear is fear itself" Nami leo nasema sisi Watanzania tunapaswa kuuogopa woga unaotufanya tuone kuwa pamoja na madini yetu, gesi yetu, mbuga nyingi za wanyama, na ardhi nzuri ya kilimo, eti hatuwezi kusimamia raslimali hizi na kupata mapato makubwa yatakayotuwezesha kuwalipa walimu wetu vizuri; eti hatuwezi kuuza madini na gesi yetu ili kuwajengea walimu wetu nyumba za kuishi zenye hadhi inayolingana na mchango wao kwa Taifa letu; na eti hatuwezi kuwarahisishia mazingira yao ya kufanya kazi kwa kuwapatia vitendea kazi bora ili watoe elimu iliyo bora kwa maendeleo ya taifa letu.



Tunapaswa kuuogopa woga unaotufanya tuone kuwa hatuna uwezo wa kuwajengea watoto wetu maabara nzuri na mabweni mazuri ya kulala, wakati tunazo kumbukumbu kuwa tulipoamua kujenga sekondari za kata tuliweza kuutekeleza uamuzi huo ndani ya miaka miwili tu, na wananchi walichangia kuliko walivyowahi kuchangia jambo jingine hapo kabla Tunapaswa kuuogopa woga unaotufanya tuone kuwa hatuwezi kuwasomesha walimu wetu kwa kiwango cha juu kabisa na kuwapa fursa wanaopenda kupanda madaraja nafasi ya kurejea darasani. Mimi nina imani kuwa tukiamua kwa dhati na tukashikamanatutaishinda vita hii. Nina imani nanyi walimu wote mlioko hapa na walimu wote nchini Tanzania.


Bila nyie ndoto niliyoisimulia hapo juu haitakuwa ya ukweli. Lakini nina mwarobaini wa matatizo yenu.Jibu langu ni "inategemea." Inategemea kama na nyie mna maono kama niliyo nayo juu ya elimu ya Tanzania. Lakini bado wajibu wa walimu kujikomboa unaanza na nyie wenyewe walimu. Walimu wa Moshi Vijijini mmeonesha njia, shime walimu wote tambueni wajibu wa kwanza unaanza na nyie wenyewe, na sisi tutawaunga mkono daima. Ahsanteni sana kwa kunisikiliza. Tuko pamoja
 
Kuna barua ya aliyekuwa msaidizi wa Baba wa Taifa inayo elezea aliyoyasema babna wa taifa kuhusu Lowassa kuwa na pesa kuliko Rais (Baba wa Taifa) bila kuelezea alizipata wapi?
Hivi raisi anayegawa mali alizozipata kwa hila ndiye tunayemtaka?Je akifilisika? Sijawahi akimuongelea mtu wa kawaida wa Tanzania vile wakulima na ardhi katika Tanzania tunayoihitaji.
Tutafakari. Ni rais wa namna gani tunamhitaji ili atuvushe? Huyu rafiki yake Rostam Azizi au................?
 
KANYANGO
Kuna barua ya aliyekuwa msaidizi wa Baba wa Taifa inayo elezea aliyoyasema babna wa taifa kuhusu Lowassa kuwa na pesa kuliko Rais (Baba wa Taifa) bila kuelezea alizipata wapi?
Hivi raisi anayegawa mali alizozipata kwa hila ndiye tunayemtaka?Je akifilisika? Sijawahi akimuongelea mtu wa kawaida wa Tanzania vile wakulima na ardhi katika Tanzania tunayoihitaji.
Tutafakari. Ni rais wa namna gani tunamhitaji ili atuvushe? Huyu rafiki yake Rostam Azizi au................?​


Nyie midimu a.ka. vijana wa mzee wa kung'oa kucha mna stres lowasa aingii ikulu kutapanya kilichopo kama bosi wenu hana njaa na aingii ikulu ili akaamishie watoto wake ikulu...eti msaidi wa nyerere alileta hotuba huyo si kipaza sauti cha kna sita wanampa buku 7 kutokana na kuganga njaa kama wale vijana wa nape eti Nyerere kwani nyerere alkuwa Mungu nchi hii kiongoz imara alkuwa sokoine na waltofautiana sana na nyerere cz nyerere alkuwa hashaurki na aliona sokoine anamzd uwezo sokoine alshajiuzulu zaid ya mara 2 nyerere akamuomba arudi so nyerere si Mungu ni bnadamu na kzazi kpya tunataka maendeleo na watu strong kama lowasa si wanaolialia kama kna membe na sita, pia nyerere altofautiana na karume pia na mzee mtei muasisi wa chadema, nyerere alkuwa hashaurki na alkuwa aksema lowasa ni kijana mkorofi...lowasa ni jembe na ni mtu anayeweza kuwavusha watanzania kwenda kwenye neema kwa sababu ni jasri na anasimamia anachokiamn pia anataman maendeleo kwa kila mtu
 
MAISHA POPOTE; This is Lowassa,he talk as the President,move as the president and indeed act like a president....
Hahahahahaha ngumu kumesa yerooo ila midimu imese hivyohvyo ma presdent is LOWASA
 
Kajiuzuru kwa ufisadi, sasa anaonekana makini kuliko kikwete! siku hizi wenye akili hawataki kuwa viongozi, viongozi wako kwenye kubabaisha
 
Hivi Lowassa anadhani ataiendesha hii nchi kwa harambee? Anaweza kuwa Ombaomba kuliko Kikwete huyu...

Harambee is ombaomba wewe...yaani wananchi kujituma ktk kugharamia mamb yao wenyewe ni kuomba?tatizo la Lowasa ni kuiga ya CDM kwa kiasi cha kuibomoa CCM.Hapo ndipo nilipopapenda.
 
Amenena vema E.L , ni vema tukajadili hoja zilizobeba hotuba yake na wala si kumjadili yeye, hatuwezi kufanikikiwa na tutakuwa tunapofusha fikra zetu kujadili personalities badala ya hoja, Ukereketwa wa Lowassa katika sekta ya Elimu ni jambo lisilo na mjadala,
 
Dah!! Huyu Bwana ameongea Mambo mengi Mazuri na yenye Matumaini.Lakini si huyu Lowasa ambaye yupo Serikalini kwa Miongo Kadhaa sasa?Si huyu ndio yupo kwenye vyombo vya juu vya Maamuzi vya CCM?Kwa nini Ushauri huu Mzuri asiutoe huko ili uje kama Tamko rasmi la Serikali?Kama wanapinga Mawazo yake atuambie hadharani.Tofauti na hapo ni yaleyale ya kutaka kujitia Kondoo kumbe ni Mbwamwitu.
 
Nyie midimu a.ka. vijana wa mzee wa kung'oa kucha mna stres lowasa aingii ikulu kutapanya kilichopo kama bosi wenu hana njaa na aingii ikulu ili akaamishie watoto wake ikulu...eti msaidi wa nyerere alileta hotuba huyo si kipaza sauti cha kna sita wanampa buku 7 kutokana na kuganga njaa kama wale vijana wa nape eti Nyerere kwani nyerere alkuwa Mungu nchi hii kiongoz imara alkuwa sokoine na waltofautiana sana na nyerere cz nyerere alkuwa hashaurki na aliona sokoine anamzd uwezo sokoine alshajiuzulu zaid ya mara 2 nyerere akamuomba arudi so nyerere si Mungu ni bnadamu na kzazi kpya tunataka maendeleo na watu strong kama lowasa si wanaolialia kama kna membe na sita, pia nyerere altofautiana na karume pia na mzee mtei muasisi wa chadema, nyerere alkuwa hashaurki na alkuwa aksema lowasa ni kijana mkorofi...lowasa ni jembe na ni mtu anayeweza kuwavusha watanzania kwenda kwenye neema kwa sababu ni jasri na anasimamia anachokiamn pia anataman maendeleo kwa kila mtu


Watu type yako ndo wananifaa, mwaga ya moyoni fastafasta, me pia nadhani EL akikwea magogoni hana njaa kivile kama JMK, so atawasaidia wananchi, (labda ikute anazikopa)
hapo ndo tungeumia. Otherwise namsapot.
 
Niwakumbushe changamoto moja aliyoipata Rais Franklin Roosevelt wa Marekani. Tarehe 8 Desemba 1941 Rais Roosevelt alilazimika kuiingiza Marekani katika Vita Kuu ya Pili ya Dunia baada ya Ujapani kuuvamia mji wao mmoja uitwao Pearl Harbour huko Hawaii. Rais huyu alipambana na baadhi ya Wamarekani waliokuwa na hofu kuwa Marekani na marafiki zake wasingeshinda vita ile kwa sababu ya nguvu kubwa ya maadui zao yaani Ujerumani, Ujapani, naUitaliano. Akiutuliza woga huo, Rais Roosevelt alisema, na hapanamnukuu: "The only thing we have to fear is fear itself" Nami leo nasema sisi Watanzania tunapaswa kuuogopa woga unaotufanya tuone kuwa pamoja na madini yetu, gesi yetu, mbuga nyingi za wanyama, na ardhi nzuri ya kilimo, eti hatuwezi kusimamia raslimali hizi na kupata mapato makubwa yatakayotuwezesha kuwalipa walimu wetu vizuri; eti hatuwezi kuuza madini na gesi yetu ili kuwajengea walimu wetu nyumba za kuishi zenye hadhi inayolingana na mchango wao kwa Taifa letu; na eti hatuwezi kuwarahisishia mazingira yao ya kufanya kazi kwa kuwapatia vitendea kazi bora ili watoe elimu iliyo bora kwa maendeleo ya taifa letu.

Apo ndipo ninapomkubali lowasa yupo strong kutetea anachokiamini na si kigeugeu au mpma upepo kama wenzake...ma presdent 2015 is LOWASA Kwa kweli silaha nakukubali sana lakini ili jembe lowasa tulipe nafasi kwanza
 
Mleta mada nakusahihisha, E.L ni waziri mkuu ALIYEJIUZURU na sio mstaafu. call a spade a spade.
 
MASANILO Hakuna cha maana ni Fisadi tu huyo.

Ni mawazo yako tunayaheshmu kwa sababu kila mtu na haki ya kutoa maoni yake ila kura yako ni moja na sisi tunamkubali lowasa na 2015 tutampa kura za yes kwenda ikulu kwa sababu yupo strong kutetea anachokiamini...nikuulize swali ni mgombea urais gani ndani ya ccm mwenye ubavu wa kuanika uozo wa serkali kama anavyofanya lowasa...si sita,wala membe wote wanalamba viatu vya JK ....lowasa anatoa tatzo na kutoa solution..ana mifano hai shule za kata alizjenga within 2yrs na stage two ilikuwa ni kuziwezesha kwa kuzpa waalimu bora...toka lowasa aondoke ktk uwazri mkuu nchi hii ni bora liende amna kpya kilichofanyka kilmo kwanza watu waliishia kula pesa za ruzuku wzaran...na lowasa aliwashaur kabla wawekeze ktk elimu hzo fedha zilipie wanafunzi mikopo wote vyuo vkuu na sekondar ziwe bure na walimu walpiwe na gvment bt wakamkatalia...mm kura yangu ipo kwa lowasa either kuptia chama chochote au akiwa kama mgombea bnafs.
 
Lowassa is a visionary and charismatic leader. Sumaye was boring as much as Pinda!
 
Kajiuzuru kwa ufisadi, sasa anaonekana makini kuliko kikwete! siku hizi wenye akili hawataki kuwa viongozi, viongozi wako kwenye kubabaisha

Mazingira ya kuondoka kwenye U-PM kwa huyu jamaa kunatofautianaje na kufukuzwa?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom