Full mapicha picha

onyx

JF-Expert Member
Mar 17, 2016
1,587
1,316
Wakuu heshima zenu,

Kusema kweli nchi inapoelekea wala sielewi. Moja haikai, mbili haikai. Vijana tunazidi kuharibikiwa na siasa, sio kama zamani wazee wetu walikuwa na mijadala mirefu ya kujenga nchi.

Leo hii ukiingia kwenye mitandao ya kijamii ni aibu tupu, vijiweni hapafai, makazini hapafai. Mbaya zaidi hata majumbani hapafai. Kila nikitafakari kesho yetu hata sielewi.

Kwanini tumekubali kuwa na Taifa la namna hii, na wapi tulipojikwaa. Mara huyu kamsema yule, yule kamsema huyu full tafrani.

Tuelekezeni nguvu zetu kwenye ujenzi wa Taifa. Najua wengi hatujui pa kuanzia, wala hatuna mitaji,lakini hii hali isitukatishe tamaa.Tunaweza kujiunga huko huko kwenye magroup yetu ya whatsapp na tukaweza kuanzisha jambo la maana.

Sio kila siku ukiamka,huyu hivi,yule hivi, hatujengi bali tunabomoa. Kwanza kama binaadamu tufahamu kila mtu kapewa kipawa chake, kwanini tusiviunganishe lipatikane jambo la maana.

Kwa mfano tunakesha kwenye mitandao kuchafuana, hivi mimi nikichafuka wewe utakuwa umeongezekewa na kitu gani.

Tuacheni mambo hayo bana, tutafakari ni namna gani kama taifa tutajikwamua kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Hizi tabia tujaribu kuziacha, maana hali ni mbaya full mapicha picha

Onyx
 
Tatizo siyo sisi vijana tatizo ni wao,kwa kuanzia tu mkulu kasema anapenda kipindi cha shilawadu na sisi kwetu viongozi ni kioo chetu tunafuata wanayofanya, kingine kutwa kucha mara Makonda kafanya hivi, mara Gwajima kasema yale na kikubwa kinachonifanya mm binafsi nishinde mtandaoni ni KUDANGANYWA KUWA NITAPEWA AJIRA NDANI YA MIEZI MIWILI LAKINI SIZIONI
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom