Nampongeza Mheshimiwa Rais na uongozi wa serikali kuu mkoa wa Daressalaam na NEMC kuingilia kati kwa wakati muafaka na kusitisha ujenzi wa structures kwenye eneo la fukwe pwani ya Oysterbay na Masaki.
Mwanzoni nilipoona kuna bulldozers zinafyeka eneo hilo niliamini kuwa kuna wawekezaji ambao wameamua kuwekeza kwenye eno hilo kwa madhumuni na maslahi ya Watumiaji wote wa fukwe.
Inasikitisha kuona kuwa Halmashauri za Mkoa wa DSM kupitia idara yake ya mipango miji na Kamati ya madiwani wa mipango miji, haielewi kitu kingine zaidi ya kutoa vibali vya ujenzi wa majengo tu. Na majengo yenyewe yawe yale yanayojengwa na watu wenye nia ya kujenga kwa nia ya kupangisha majengo ya nyumba za kuishi au maduka. Masuala ya kupendezesha fukwe na mazingira haimo kabisa kwenye agenda zake. So sad indeed.
Hebu fikiria kwa nini eneo la fukwe kuanzia Seacliff hotel urudi mpaka Golden Tulip hotel halafu uanzie nje ya Police mess uje hadi kibandani Coco beach moja kwa moja mpaka light house karibu na kasri ya Agakhan wasipatengeneze kwa kuweka pavements za na walkways ambapo wangeweka taa za usiku. Eneo lote hilo wangepanda maua na miti ikawa park ambapo watu wangeweza kufan ya mazoezi yajogging, ya kutembea au hata kukaa na kula upepo wa bahari. Na wale vijana wanaojinasisha kwenye daladala au malori wakati wana roller skates zao, wangeweza kucheza michezo yao kwenye pavements hizi.
Ninamuunga mkono pia mheshimiwa Janet Zebedayo Mbene Mwenyekiti wa mtaa wa Masaki na sasa mbunge wa kuteuliwa, kwa kuwa mstari wa mbele kupinga zoezi hilo la kujenga ati maeneo ya recreation. Well done Mheshimiwa.