Fukwe (Beach) za Tanzania na hatma yake

Game Theory

Platinum Member
Sep 5, 2006
8,545
835
Nchi inaelekea pabaya waTANZANIA sasa wapigwa marufuku COCO BEACH!

Kuna taarifa kuwa baada ya kutumia pesa za walipa kodi, WATANZANIA sasa wamepigwa MARUFUKU kwenda ufukweni na serikali kupitia halmashauri ya jiji

Jamani haya yanatokea TANZANIA ya mwaka 2007 na siyo 1957
 
Nooo way!
Haya ndiyo yaliyowakuta Jamaica miaka ya 80! na haya haya ndiyo yaliyoangusha serikali iliyokuwa madarakani!...viongozi wetu wanayaona kuwa madogo basi yatakuja watokea puani.
 
Suala la Coco Beach ni suala pana, kama munafuatilia, hao watu wa Jiji/Manispaa wamekua wakisuasua na tenda waliyoipenyeza kinyemela kutaka kuuza sehemu kubwa ya ukanda wa pwani ya Oysterbay ikiwamo Coco Beach na nyinginezo kwa mwekezaji mwenye asili ya kiasia. Baada ya mambo kuwekwa hadharani katika gazeti moja, wakaahirisha na kukaa kimya. Sasa wanafanya mambo kimya kimya na mutasikia simu moja hata yale majengo na vibanda vya pale Coco beach kwenyewe yanavunjwa na matingatinga ya Manispaa/Jiji, kabla ya kuanza kuona makandarasi wakijenga kwa haraka majengo ama vitega uchumi ili muwe mukitaka kwenda beach mulipie ama tena iwe ni beach ya watalii toka nje ya Tanzania na kina sie tuendelee kwenda kula upepo pale juu Manzese Darajani. TUWE MACHO, Tusikubali
 
I also overheard this Coco beach issue and was well handled by Jumanne Magembe.
 
Pamoja na Waziri Jumanne Maghembe, wa Maliasili na Utalii kuzungumzia, na Adam Kimbisa (Meya wa Jiji la Dar es Sakaam) bado kuna vibao vya Manispaa kuzuia watu kufanya shughuli. Lakini Jumamosi hii nilikuta watu chini ya kibao "Marufuku kufanya shughuli hapa" wakivinjari na bibi na bwana harusi wao huku wakipiga picha na wauza madafu na ice cream wakiendelea na biashara zao. Nasikia watu wameapa, "Mgambo wa Jiji athubutu kufukuza watu ataona cha mtema kuni" tutarajie vurugu kubwa pinda nguvu itakapotumika
 
ama kweli waTANZANIA wavumilivu

I cant imagine issue hiii ingekuwa nchi kama NIGERIA hali ingekuwaje

Hivi hata hakuna wanafunzi wa chuo kikuuu wanaofanya PROBONO ambao wanaweza kuchukua hii issue na kutengeneza majina ili hali bado wako University?
 
ama kweli waTANZANIA wavumilivu

I cant imagine issue hiii ingekuwa nchi kama NIGERIA hali ingekuwaje

Hivi hata hakuna wanafunzi wa chuo kikuuu wanaofanya PROBONO ambao wanaweza kuchukua hii issue na kutengeneza majina ili hali bado wako University?


Ilikuwa zamani. Wanafunzi wa siku hizi wana deal na allowance. Wakipata vihela vyao basi, wanafikiri dunia imeisha wanaenda kulewa!
 
kweli

hivi katika wanasiasa ni yupi ambaye yuko makini kusikiliza watu ?

maana hiali ishakuwa ya desperation

hii ni back door apartheid
 
DrWHO

Hivi hata hakuna wanafunzi wa chuo kikuuu wanaofanya PROBONO ambao wanaweza kuchukua hii issue na kutengeneza majina ili hali bado wako University?


Naona wewe sasa umelowea huku, mambo ya UK unataka yafanyike pale Bongo, hao wanafunzi wakuifanya hii kesi wako kwenye level ipi? Vile vile kumbuka hii sio mara ya kwanza kwa Coco beach kutaka kuchukuliwa kama nakumbuka vizuri enzi ya mzee ruksa kulikuwa na kitu kama hiki lakini kilizimwa. Kwa hiyo jamaa safari hii wamejiandaa na unavyojua sasa hivi ni watu wawili tu muungwana na rafiki yake ukiwaweka hao mfukoni mambo yamekwisha.
 
Halisi,
Huyo Kimbisa ni ndumiakuwili. Anashiriki pia katika mpango wa kutaka kujaza mchanga pale Selenda Bridge ili mwekezaji ajenge nyumba za magorofa, licha ya kwamba Meya wa zamani alipinga mipango hiyo kwa sababu za kimazingira.
 
haya mambo saa nyingine inapendeza kutoyajua, that way utaishi kwa amani kabisa. Kila rasilimali tumeibiwa sasa hata kupunga upepo wa Mungu napo tunanyimwa! mh, labda ndo sikio la kufa..inaweza kuwa ndo kifo cha CCM kilichotabiriwa...yetu macho
 
Kuna hajan ya kubeba panga hapa na kuwakata hawajinga hadharani tunyongwe maana lugha ya u civil ni msamiati kwao .
 
Lunyungu nilikuwa naogopa kutamka hivyo ila tayari nilikuwa na wazo hilo,kwa kweli akili yangu imechafuka sana kiasi naamini hiyo ya mapanga inaweza saidia as last solution. Hii amani wanayotuimbia kila siku ni mfuniko na kinga wanayoitumia ili waendelee kutu-skin tukiwa hai.Kama ni amani wao ndo wanaivunja na wakati hauko mbali.
 
haya mambo saa nyingine inapendeza kutoyajua, that way utaishi kwa amani kabisa. Kila rasilimali tumeibiwa sasa hata kupunga upepo wa Mungu napo tunanyimwa! mh, labda ndo sikio la kufa..inaweza kuwa ndo kifo cha CCM kilichotabiriwa...yetu macho

nimeamua kuchukua ushauri wako

kwani yananipa depression
 
Wanabodi,

Haya maswala sasa hivi yanakwenda mbali sanaa. TUMECHOKA kuburutwa!

Mimi binafsi na familia yangu yametukuta makubwa.. Huko Mwanza tuna uwanja mkubwa sana sehemu za Pasiansi karibu kabisa na lake Nyanza. habari nilizozipata ati serikali imeamua kuichukua sehemu hiyo na ndugu zangu kupewa uhamisho sehemu nyingineyo...
Hawa viongozi wetu wenyewe wamegoma kabisa kuhamia Dodoma lakini wao wanaona rahisi mtu kuondoka sehemu ambayo mababu zako walizaliwa hapo na kuna makaburi yao leo mnatuchukua mzobemzobe utafikiri tunaanzisha upya vijiji vya Ujamaa. Fidia yenyewe inakadiriwa na wao sio sisi kwa sababu tu serikali ndio yenye ardhi!...je, serikali ni nani? hatuna jibu.
Tuliomba kujenga Hotel ya kitalii (kwa sababu sehemu hiyo ni karibu na Uwanja wa ndege) tukazimwa kwa miaka baada ya kugundua kuwa kiwanja hicho hicho kulitakiwa na mhindi. Zaidi ya miaka kumi kumekuwa na mvutano bila suluhu, leo tunaambiwa ati serikali inataka kujenga bwawa la maji machafu na taka...LAZIMA wananchi wahame!..
Come on guys, karibu na uwanja wa ndege ambao unakusudiwa kuwa wa kimataifa? Hizi taka zimeanza jana kuwepo kiasi kwamba hakuna sehemu nje kabisa ila sehemu karibu na ziwa.
 
kila mtu kashachoka

saa mtu ukirudi Tanzania ukiwa na ngozi nyeusi huwezi kwenda COCO BEACH

yaani nchi imekuwa kama ALABAMA 1959
 
rawisi%2022.JPG


RAIS Jakaya Kikwete akiteta na mgeni wake, Naibu Mtawala wa Ras AL Khaimah, Sheikh Saud Saqr AL Qasimi, IKulu, mjini Dar es Salaam, jana ambaye yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu. (Picha na Freddy Maro).

Michuzi blog Waziri wa Viwanda Biashara na Masoko B. Mramba akiwabrif paparazi juu ya ujio wa Shaik saud bin Saqr al qasimi ambaye ni mtawala wa rs al Khaiman ambayo ni mojawapo ya nchi saba zinazounda imarat. Mgeni huyu atatembelea sehemu mbalimbali ambazo nchi yake imeonyesha nia ya kuwekeza ikiwa ni pamoja na fukwe za Dar pamoja na daraja la Kigamboni. atatembelea Zenj na kwenda kuangalia wanyama kule grumet.

Sasa yale maswali ya ufukweni huyu ndie anakuja kwa mgongo wa wakubwa kuwekeza. Je sheria zetu za ardhi ndio siku hizi zimekufa? Kiasi gani anawekeza na kina nani ni share holders? Je ni hii amani tuliyoiendekeza kuweka hii mikataba siri?
 
Back
Top Bottom