Fukuzafukuza CHADEMA: Josephine kama Mama Ruksa enzi hizo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fukuzafukuza CHADEMA: Josephine kama Mama Ruksa enzi hizo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by GHOST RYDER, Oct 2, 2012.

 1. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #1
  Oct 2, 2012
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  · Yadaiwa ana Ushawishi Mkubwa katika Maamuzi ya Chama
  · Wakati mwingine kwa Utashi hata kuliko Kanuni na Maadili ya Uongozi
  · Wanaoitwa Pandikizi wadai hofu ni Urais 2015
  · Walaani kutumiwa jina Rais kwa Katibu Mkuu katika safari za M4C kuwa ni chanzo cha migogoro mingi ndani ya CDM

  M2 ni Zaidi ya Anavyofikirika

  SOMA KWA MAKINI UZI HUU HALAFU TUKUTANE BAADA YA PRESS CONFERENCE:

  Mabingwa wa misamiati na nahau wanaamini kabisa ''Kila matokeo ya mafanikio au kuporomoka kwa mwanamume nyuma yake kuna mkono wa mwanamke''.


  Ni dhahiri kama mama ni nguli wa kupanga, kuamua na kuongoza njia sahihi hapana shaka matokeo ya tunu hizo yataakisiwa na mafanikio katika familia hiyo, na akiwa bingwa wa kutaka makuu, mbwembwe na daima awe juu faraka na sintofahamu hujenga makazi katika familia hii.

  Siku chache baada ya kufukuzwa uanachama kwa waliokuwa madiwani wa CDM huko Igoma kumeibuka malalamiko mazito juu ya mwenendo wa Maamuzi yanayochukuliwa na Katibu Mkuu wa CDM kwamba hufanyika kwa ushauri mkubwa ubavu wake.

  Madai haya ambayo hakuna hata kiongozi mmoja tuliyeongea naye jana aliyekubali kuyathibitisha huku kila mmoja akirusha mpira kwa mwenzie yanadaiwa kuongeza hali ya ujoto wa kisiasa na vuguvugu la kutoaminiana kwa madereva ndani ya CDM huku mzimu wa mkasa wa timuatimua makao makuu zama za Mwigamba hadi Arusha, Mbeya na mapokezi ya Mama Josephine hadi sakata hili la Mwanza na mengine mengi yakiongeza ufa katika uimara wa chama.

  Kwa afya ya Chama naomba nisiandike mengine zaidi katika kulibaini hili ili kutoa nafasi kwa viongozi wangu kulishughulikia hili na kusisitiza katika misingi na maadili ya uongozi huku wakizingatia ukomo wa fikra mbadala katika maamuzi mazito ya kichama.

  Huku haya yakitajwa kama ni moja ya Agenda inayokusudiwa kusambazwa rasmi kwa umma kupitia mikutano ya hadhara kwa kundi linaloonekana kuwekwa pembeni ndani ya CHADEMA wanachagizwa na madai kuwa kutumiwa kwa jina Rais kwa baadhi ya wanachama katika ziara za M4C mikoani kwa Katibu Mkuu zimemtia wingu katika fikara zake na kuamini kuwa yeyote ndani ya chama anayedaiwa kuwa na nia na nafasi hiyo kuwa dhihaka kwake na mtovu wa nidhamu kwani kote apitapo wanachama tayari wanamtambua yeye kama Rais.

  Jina hili ambalo linasemekana chimbuko lake ni muda mfupi baada ya uchaguzi mkuu ambapo kinadharia chama kiliamini kupokwa nafasi hiyo kwa mchezo mchafu wa tume mgombea kiti hicho na katibu Mkuu alikuwa akishangiliwa kama Rais katika mikutano yake ya hadhara kama ishara ya kuonyesha uungwaji mkono wa wanachama licha ya unaodaiwa kuwa udhalimu wa Tume kepeleka mambo kama watakavyo.

  Kibwagizo hicho cha Rais, Rais, Rais kila asimamapo katibu Mkuu katika mikutano yake mingi kimedaiwa kunasa katika fikara za mashabiki wa CDM mpaka sasa na kumhakikishia usultani huo ambao kamwe anaelekea kuamini hakuna Rais tena 2015 ndani ya CDM zaidi yake.

  Kwa mintarafu hiyo hata migongano na nyuzi nyingi hapa Jamvini za kumpima ubavu na ZZK zinatokana na ukweli huu kwamba hutakiwi kusikika ndani ya chama mwanaCDM mwingine unawaza kuikwaa nafasi hiyo. Hang over hiyo imepelekea kuibuka hofu hewa ya kuwepo kwa mapandikizi wa ZZK ambao wanadaiwa kumuunga mkono na kwamba watakuwa tatizo kubwa katika vikao vikuu vya chama wakati wa mchakato wa kumpitisha mgombea wa Urais, wanafanywaje sasa? Jibu ni kwamba watengenezewe mazingira ya kuonekana watovu wa Nidhamu kisha fukuza wote kusafisha chama.

  Inadaiwa Orodha bado ni ndefu na wote watakwenda mmoja baada ya mwingine ili kuhakikisha kwamba 2015 mambo saafi. Hii siyo CDM inayokusudiwa hayumkini kuna tatizo la msingi hapa.

  Wengi wameaminishwa kuwa ZZK ni pandikizi wa Chama fulani na amekuwa mmoja wa Viongozi wanaoyumbisha maamuzi CDM na wanaojitenga katika harakati nyingi kumbe anaepukwa yeye kuwepo katika maeneo hayo kwa makusidi kabisa ili kumtengenezea chuki mbaya na wanaCDM hii ni hatari sana bila shaka.

  Moja ya udhaifu mkubwa unaotajwa katika muendelezo huu ni kuchukuliwa kwa maamuzi bila kufanya tafiti za kutosha kuhusu kushutumiana huko na pia kutekeleza malengo kwa hasira na jazba bilakujali matokeo yake ya muda mrefu na taswira ya chama kwa jamii.

  Licha ya madai haya M/Kiti anatajwa kama Icon muhimu sana isiyofungamana na upande wowote katika shutuma hizi na hivyo kumpa nafasi kubwa ya kuendelea kuimarisha chama na kuondosha matabaka haya yanayokomaa sasa.


  My Take:

  Muarobaini wa tatizo hili upo na moja ni kuhakikisha ule usultani wa Mama kuamua mambo mazito alioupinga hata Baba wa Taifa pale Kilimanjaro Hotel enzi za Uhai wake unapunguzwa makali nakuwekwa mbele ustawi wa chama badala ya Urais ambao unaelekea kuwa binafsi badala ya taasisi.

  Adhabu mbadala kwa viongozi na wanachama zipo ila kama ililazimika kufukuza pia si vibaya lakini tukubali kuteswa na mizimu ya kama ya akina Malema na ANC.

  ADIOS
   
 2. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #2
  Oct 2, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Mkuu unataka kutuambia Dr Slaa, alivyowafukuza Madiwani wa Mwanza, Matata na Chagulani, ni amri kutoka kwa mama Junior Josephine, mbona Mbowe anaendesha siasa zake peke yake, Dr Slaa jifunze kwa Mbowe unaingamiza Chadema.
   
 3. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #3
  Oct 2, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mkuu nakuheshimu sana lakini nasikitishwa na jinsi unavyotaka kiupotosha jamii!hivyi wale madiwani walifukuzwa na kamati kuu ya CHADEMA au Dr slaa?
   
 4. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #4
  Oct 2, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,748
  Likes Received: 12,842
  Trophy Points: 280
  Eti kwa uhai wa chama nisiandike mengine, hivi uliyoyaandika yana leta uhai kwa chama?

  Maneno mengi kumbe
  Nia ni kumhusisha josephine,.
  Unafiki ni kitu kibaya sana!

  Chanzo cha habari sijui kiko wapi? Na hayo ni matokeo ya habari za kutunga!

  Hatuwezi kufuga nyoka ndani kwa kuogopa majirani.

  Cdm hatuto gombana kwaajili ya urais-ZITTO
   
 5. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #5
  Oct 2, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Mkuu mie utanionea bure mleta huu uzi ndio kasema mengi.
   
 6. Arushaone

  Arushaone JF-Expert Member

  #6
  Oct 2, 2012
  Joined: Mar 31, 2012
  Messages: 14,373
  Likes Received: 640
  Trophy Points: 280
  Kwa maoni yangu binafsi kama mwanaCHADEMA, naomba kama kuna tatizo huko ngazi za juu ifanyiwe marekebisho ASAP. Nawasihi wachangiaji wenzangu tusitoleane lugha isiyopendeza kwani wewe unaamini hivi na mwingine vile, na ndio MAANA ya DEMOKRASIA.
   
 7. N

  Naytsory JF-Expert Member

  #7
  Oct 2, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,593
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Mleta mada, Toka lini familia ya Dr. Slaa inaunda kamati kuu ya chama? Acheni kupotosha watu.
   
 8. K

  Kuntakint JF-Expert Member

  #8
  Oct 2, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 1,112
  Likes Received: 470
  Trophy Points: 180
  Hivi ww viongozi wote ndani ya ccmafisi ni wazuri. Mbona hata siku moja uwezi hata kuwasema isipokuwa ukisikia cdm ni kama unawashwa vile. Umbea utakuua unaacha kwako kunawaka moto unakimbilia kuyasema ya jirani.
   
 9. Capt Tamar

  Capt Tamar JF-Expert Member

  #9
  Oct 2, 2012
  Joined: Dec 15, 2011
  Messages: 6,663
  Likes Received: 3,316
  Trophy Points: 280
  Na wewe pia unakosea!

  Kama una imani na demokrasia inakupasa kuamini ndani ya mipaka ya demokrasia,kama huyu mtoa mada angekuwa na nia ya kweli ya kusahihisha mfumo wa ki uongozi ndani ya chama asingekwepa ukweli anao ufahamu dhahiri kuwa adhabu ama hatua zichukuliwazo dhidi ya VIONGOZI wa chama waliopotoka hutolewa na chama kupitia vikao halali huku mtuhumiwa akipata haki yake ya kujieleza/kujitetea, hiyo inaonyesha jinsi ambavyo mtoa mada alijipanga kuelekeza mashambulizi kona fulani tu, huku akijaribu kukwepa ukweli.
   
 10. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #10
  Oct 2, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,534
  Likes Received: 5,685
  Trophy Points: 280
  Kama CHADEMA yote, akiwemo Mbowe, Zitto, Mkumbo, Lissu, Mnyika, Prof Baregu, Prof Safari, Marando, Lema, Wenje, Sugu n.k wameletewa madai yoyote kama sehemu ya utawala mkuu wa CDM wakashindwa kutoa maamuzi sahihi ikimaanisha Mama Josephine Slaa akawazidi akili hadi sheria na kanuni za chama zikapindishwa basi hata Dovutwa atakuwa Rais wa Tanzania.

  G.R mkuu wangu this is too low kutoka kwako! Sijawahi kuona unaandika kitu poor kama hiki toka nimeijua JF!
   
 11. kbosho

  kbosho JF-Expert Member

  #11
  Oct 2, 2012
  Joined: Jun 4, 2012
  Messages: 12,505
  Likes Received: 3,314
  Trophy Points: 280
  nyie kweli hamnazo!...chadema sio viongoz chadema ni wananch.
   
 12. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #12
  Oct 2, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,534
  Likes Received: 5,685
  Trophy Points: 280
  Alafu G.R tunaolalamikia mapandikizi ndani ya CDM ni akina sisi huku mitandaoni na mitaani maana tunalalamikia matendo ya hao watu! Sijawahi kusikia Dr Slaa wala Mbowe wakilalama juu ya hili! Mimi binafsi viongozi wote wawili hata sifahamiani nao lakini ni mfuatiliaji tu wa siasa zetu hizi.

  Chuki zipandikizwe na nani wakati wahusika wanaharibu mchana kweupe? Alafu Dr Slaa kuitwa Rais si mapenzi yake ni watu wenyewe mkuu wangu hata mimi binafsi hupenda kumuita hivyo!!!

  Muacheni mzee wetu afanye kazi jamani,kuendesha chama cha upinzani Afrika hususani Tanzania na Chama kikafikia kilipo Chadema si kazi ndogo! Dr Slaa ananyima usingizi Serikali na chama tawala kuliko wakati wowote toka nchi hii ipate uhuru.

  Majungu kwa Dr Slaa yamezidi sana tena siku hizi mnamtukana kupitia mke wake si jambo jema kwa wapenda maendeleo.tuacheni tuhukumu matendo yake na yenu na si kulialia humu kwa vujisababu vya kupika.

  Kama upo ushahidi wa Josephine kushinikiza watu fulani wafukuzwe weka hapa acha kuzunguka Mbuyu CDM si CCM wanakolindana.
   
 13. k

  kimboka one JF-Expert Member

  #13
  Oct 2, 2012
  Joined: Jan 23, 2010
  Messages: 734
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Mtoa mada umefanya vizuri japo unakera sana mashabiki wasiopenda kujenga kwa kuona ufa ulipo, wao huamini cdm kinaongozwa na malaika.

  Lazima mjuwe Dr ni kikwazo cha mafisadi kufanya kazi zao hivyo ni rahisi kumtumia wake zake kufanikisha mambo yao, sasa CHADEMA tunatakiwa kuwa makini wameshajua udhaifu wa kiongozi upo kwa wakina mama.

  Mtu anaposema msimbeze hawa mashemeji wetu watatuweka vibaya tuwe nao makini.
   
 14. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #14
  Oct 2, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,534
  Likes Received: 5,685
  Trophy Points: 280
  Tatizo walalamikaji wote hawana ushahidi! mwisho wa siku wanaanza kumtukana Dr Slaa na mke wake kihuni kabisa.Leteni nondo hapa tuhukumu na si kututaka tujadili mtizamo tu wa mtu mwenye chuki binafsi!

  Tumeomba wenyewe chama kisafishwe na fagio ndio hilo linapita sasa hata Shibuda akilalamika tuseme ni Josephine? Mnafikiri CDM hakuna mapandikizi ya CCM? Acheni masihara na siasa za nchi hii msidhani mambo mnavyoona yanakwenda akina Dr Slaa wanalala kwa amani kama just a CEO of certain company!
   
 15. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #15
  Oct 2, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  Hii taarifa ni ya ukweli 100%, ninaiamini na sina shaka nayo.

  Ni hayo tu kwa leo.
   
 16. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #16
  Oct 2, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,632
  Trophy Points: 280
  GR, unaleta ukosoaji wa mama Chadema humu kwa kumsingizia 1STL2BE!?. We subiri tuu, utapata habari yako!.

  NB, by the way, siku nazungumza na Dr aliponieleza msimamo wake (off the record) kama atagombea urais 2015 au laa, Ubavu wake, Mama Chadema, alikuwepo na alisema ...(off the record)!.
   
 17. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #17
  Oct 2, 2012
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135

  Mkuu take my words, its a matter of Time. Jaribu kufanya utafiti wako binafsi utayabaini haya. Usiridhike na uzuri wa kitabu kwa kurasa yake ya juu. Tuna tatizo kubwa ndani ya CDM bila kulikemea tunakwenda kubaya.

  CCM mwanza wametumia udhaifu wetu kujiimarisha na wamefanikiwa, tukishinda ubunge Mza 2015 itakuwa kwa mbinde hasa, leo CUF kaona ombwe jingine Arusha kapiga kambi huko.

  Mapande yanazidi na uimla unamarika, ni hatari kwa chama cha siasa
   
 18. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #18
  Oct 2, 2012
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Pasco,

  Najua leo watanishangaa wengi sana Mkuu, ila hili ni kwa ithibati yangu binafsi na juhudi za kina, Kwa mabadiliko thabiti hakika wakuu watanivumilia tu leo, mwarobaini mchungu ila dawa.
  Kuna tatizo ndani CDM lisipotolewa mapema mashabiki wengi watapoteza imani.
   
 19. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #19
  Oct 2, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,280
  Trophy Points: 280
  Mimi nadhani sasa ni wakati wangu muhafaka wa kuomba uanachama wa Chadema ili kuwakabili waganga njaa wote akiwemo huyu mleta thread ili wajuwe tunapaswa kufanya siasa baada ya shughuli zetu zingine halali zinazotuingizia kipato.

  Njaa na akili hata siku moja haviwezi kukaa pamoja, mbona hamuendi kwenye chama cha Dovutwa kwenda kuleta migogoro? Yaani mnaona ng'ombe amenona mnadhani sasa ni wakati wa kukamuwa tu na mvune kile msichopanda?
   
 20. b

  bariadi2015 Member

  #20
  Oct 2, 2012
  Joined: Sep 26, 2012
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwanini hujui ni kwanini walifukuzwa? Mfundishe dhaifu mwenzio kwani kahaikisha familia yake wanapita bila kupingwa, ukipinga tu, huna ulaji tena
   
Loading...