KITAULO
JF-Expert Member
- Apr 27, 2018
- 1,926
- 2,776
Wana JamiiForums,
Hamna jambo zito kama kusubiria majibu baada ya kufanya vipimo vya maambukizi ya VVU. Ni kipindi ambacho mtu hujikuta upo kwenye ulimwengu mwingine kiroho na ndo kipindi mwanadamu heweka nadhiri nyingi na Mungu wake endapo tu atamuepusha na hilo dhahama.
Hata mkiwa wengi hamna anayepata nguvu ya kuongea na mwenzake. Kila mtu anazama kwenye dimbwi mawazo kujaribu kutafakari ni wapi anahisi alizingua na kuanza kuevaluate makoloni yake yote aliyopitia.
Hakika hamna kipindi kigumu kama hiki. Pale unaitwa kuchukua majibu yako mwili huwa unapoteza nguvu ndo kipindi tumbo la kuhara hukushika na mapigo ya moyo yanakuwa kwenye speed ya ajabu.
Sasa ukute mshauri ana mbwembwe wakati wa kutoa majibu huwa mtu unahisi kama dunia yote siyo yake tena.
Hakika kusubiri majibu ni kipindi kizito na chenye siri nzito..
Wadau hebu tupeane experience wakati wa kusubiri majibu ya VVU/AIDS