Fukuto la Katiba: Wasira azomewa mkutanoni, akasirika na kufunga mkutano ghafla! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fukuto la Katiba: Wasira azomewa mkutanoni, akasirika na kufunga mkutano ghafla!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kiche, Jan 13, 2012.

 1. k

  kiche JF-Expert Member

  #1
  Jan 13, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 456
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Katika hali isiyo ya kawaida juzi katika viwanja vya stendi ya zamani mjini bunda,waziri wasira akiambatana na mbunge wa musoma vijijini ndugu Mkono kwa kile ambacho walikiita mkutano wa elimu katika mchakato wa katiba mpya ambapo walikumbana na zomea zomea hasa wananchi walivyoonyesha kukerwa na sheria inayowabana ya kuelimishana kuhusu katiba kwa madai kuwa kazi hiyo lazima ifanywe na tume tu!!!

  Bila kutarajia wasira alibanwa ni kwanini anatoa elimu hiyo wakati sheria hiyo iliyosainiwa na bosi wake hairuhusu hivyo naye amevunja sheria na ashitakiwe,kutokana na kubanwa huko wasira alisema wananchi hawakuelewa vizuri sheria hiyo lakini wananchi walionyesha kuchachamaa na ndipo wasira alipovunja mkutano huku zomea zomea ikiendelea.

  Swali langu

  Je hivi walipokuwa wakitunga sheria hii ya hovyo hawakujua kwamba hata wao inawabana?au nao ni sehemu ya tume?
  Je inakuwaje mpokea maoni maoni ndiye awe muelemishaji?

  Naomba kuwasilisha wakuu
   
 2. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #2
  Jan 13, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Wassira na Jeshi lake(wabunge wa CCM)wameogopa kufanya Mkutano Musoma Mjini na wakafanya Makutano(nje ya mji)ambapo pia walizomewa na kuamua kuondoka,imebidi wafunge zoezi,hayo yamefanyika huku Chadema ikipasua Anga la Mara na Jeshi la Mtu mmoja(Vincent Nyerere)
   
 3. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #3
  Jan 13, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  siamini kama kweli tukio la namna hii lilitokea,unless mtoa thread anataka tu tujadili uozo/ubovu wa sheria ile
   
 4. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #4
  Jan 13, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,782
  Likes Received: 36,777
  Trophy Points: 280
  ukombozi wa kifikra ni jambo la kuzingatia kabla hata ya swala hili la katiba.
   
 5. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #5
  Jan 13, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,869
  Likes Received: 6,220
  Trophy Points: 280
  kama ni kweli basi mmmmmh maana unapozomewa jimboni mwako ambapo ndo ngome yako ipo mmmmh hatari
   
 6. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #6
  Jan 13, 2012
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hizi sheria zetu hutungwa ili kubana mtu au kikundi cha watu fulani.
   
 7. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #7
  Jan 13, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Na bado ! hizo ni rasharasha tu, mvua zenyewe bado. Pole pole wananchi wanaanza kuchambua mchele na pumba na mwaka 2012 ndio tu umeanza, kaazi kweli kweli.
   
 8. u

  utantambua JF-Expert Member

  #8
  Jan 13, 2012
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 1,373
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Habari ndio hiyo, ichukue ama ipotezee, kazomewa!
   
 9. nashy

  nashy JF-Expert Member

  #9
  Jan 13, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 679
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Safi sana hata mimi ningemzomea, simpendi huyu jamaa kwa pumba zake
   
 10. Bumpkin Billionare

  Bumpkin Billionare JF-Expert Member

  #10
  Jan 13, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 1,336
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Yawezekana wewe ni mwenyeji wa pwani ambako kila mnachoambiwa huitikia 'hewala mzee'. Kule Mara hilo ni tukio dogo tu. Kama hujui muulize Nyangwiri Nyambwene namna alipopolewa na mawe kwa kuleta mambo ya kijinga kama ya Wassira. Halafu kutoamini kwako ni sababu ya kutokujua kwako kuwa kuna Watanzania wanaohoji haki zao tofauti na wewe unayekubali kila kitu.

  Hata Mbeya msafara wa Kikwete ulipigwa na mawe na alizomewa mkutanoni mpk Mark Mwandosya alivyowatuliza, sijui cha ajabu nini hapo kwa kuzomewa huyu Mlala Bungeni.

  Na kama nia ya mtoa uzi ni tujadili uozo wa sheria, njoo basi tujadili badala ya kujitia ufundi wa kubaini nia, kwani hiyo haina marks.
   
 11. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #11
  Jan 13, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  MKUTANO wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu Stephen Wasira, uliofanyika juzi katika viwanja vya stendo ya zamani, ulilazimika kuvunjika baada ya kuzomewa kutokana na kutoa majibu yaliyoonekana kama vitisho kwa wananchi waliokuwa wakimuuliza maswali.

  Chanzo cha zomeazomea hiyo kilitokana na waziri huyo kuwaonya wananchi wasijaribu kuvunja sheria kwa kulazimisha kwa nguvu kufanya mambo yaliyokatazwa wakati huu wa kukusanya maoni na kwamba watakaofanya hivyo watakamatwa na kufungwa au kutozwa faini jambo ambalo liliwachefua wananchi.


  Waziri Wasira, aliyeandamana na wakili maarufu nchini na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Nimrodi Mkono, awali alieleza kuwa wakiwa wabunge wa CCM waliitisha mkutano huo kwa lengo la kutoa elimu juu ya mchakato wa uandikaji wa Katiba mpya na kueleza jinsi walivyoshiriki vema tangu ulipofikishwa bungeni hadi kusainiwa na Rais Kikwete, kauli iliyopingwa na wananchi waliokuwepo uwanjani hapo. Kutokana na kauli hiyo, baadhi ya wananchi walihoji sababu za Wasira akiwa mtumishi wa umma kuingilia kazi ya tume ya kukusanya maoni ya wananchi juu ya uandikaji wa Katiba mpya.


  Wananchi hao walisema kuwa kwa kuwa sheria ni msumemo, basi waziri huyo alipaswa kushtakiwa kwa sababu alikuwa amevunja sheria hiyo iliyosainiwa na Rais. Mmoja wa wanaharakati waliokuwa katika mkutano huo, Frank Kubwera, mkazi wa Bunda, alidai kuwa Wasira na Mkono walivunja sheria Na.2 ya utumishi wa umma ya mwaka 2002 na taratibu za utumishi wa umma ya mwaka 2003. Kubwera alisema kuwa Waziri Wasira kwa kufanya mkutano huo alikuwa amevunja kanuni za kudumu za utumishi wa umma za mwaka 2009 na kwamba kwa pamoja mafungu hayo yanakataza mtumishi yeyote wa umma kujihusisha au kutoa maoni katika mkutano wa vyama vya siasa.


  "Nawashangaa kuwa waziri na mwanasheria mmekuwa wa kwanza kuvunja sheria hii iliyosainiwa na Rais kwa kuwa mmeingilia kazi ya Tume ya Katiba inayosema atakayevunja atalipa faini ya sh milioni 5 hadi 15 au kifungo cha miaka mitatu hadi miaka saba," alisema Kubwera huku akishangiliwa na umati wa watu waliokuwepo. Alifafanua kuwa licha ya Wasira mwenyewe kuwa mtumishi wa umma kwa wadhifa wa uwaziri lakini alishuhudia ofisa tarafa akishiriki kufungua mkutano huo.


  "Jambo la pili mmevunja sheria kwa kumruhusu mtumishi wa umma ambaye ni ofisa tarafa kufungua mkutano wa kichama kuhusu maoni ya Katiba, hivyo kwa kuwa kifungu hicho kinakataza mambo hayo mimi siko tayari kutoa maoni yangu nisije nikafungwa," alisisitiza Kubwera.

  Naye mwananchi mwingine Mongson Kabehu aliomba kipengele cha sheria ya kifungo cha miaka miwili au zaidi kwa kujadili Katiba nje ya tume ya kukusanya maoni ya Katiba ibadilishwe kwa kuwa inawanyima uhuru wananchi kujadili Katiba pamoja bila kuwepo tume.

  Mongson Kabehu na Frank Kubwera ni miongoni mwa wananchi kutoka wilayani Bunda walioshiriki katika mdahalo wa wazi kuhusu mswada wa Katiba iliyosaniwa na Rais kuwa sheria ya ukusanyaji wa maoni juu ya uandikaji wa Katiba mpya uliofanyika mwezi Aprili mwaka jana mjini Dodoma.

  Hoja hizo zilimfanya Wasira aamue kukatisha ghafla maswali na maoni ya wananchi na kuamrisha mkutano ufungwe huku akisema kuwa watu hao wamenukuu vibaya sheria hizo na kwamba sheria ya utumishi wa umma iliyotajwa inazuia tu mtumishi wa umma kutofanya kazi za chama cha siasa na sio kwenye mkutano kama huo.

  Wasira alisema kazi ya kutoa elimu ni kwa vyama vyote vya siasa na sio CCM tu na kwamba hata wabunge wa vyama vingine watafanya hivyo.
  Kwa upande wake Mkono ambaye katika mkutano huo alivaa sare za CCM pamoja na mambo mengine alidai kuwa wananchi hao hawakutafsiri vizuri maneno hayo ya kisheria kwa kuwa yaliandikwa kwa lugha ya Kiingereza.

  Kuahirishwa ghafla kwa mkutano huo kulizua mtafaruku uwanjani hapo huku umati huo ukiwataka wabunge hao kutoa ufafanuzi zaidi.
  Mkutano huo ulitawanyika huku wananchi wakizomea jambo lililofanya wabunge hao na viongozi waliokuwepo kuondoka kila mmoja kwa njia yake.

  Tanzania daima

   
 12. only83

  only83 JF-Expert Member

  #12
  Jan 13, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Tusubirie mengi wakati wa kukusanya maoni...ngumi lazima zipigwa kwa style hii ya magamba kuendesha mambo kihuni....
   
 13. The FaMa

  The FaMa Senior Member

  #13
  Jan 13, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 125
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Lakini huyu Wassira huko Bunda si ndiyo nyumbani kwao/jimboni kwake?!! Au nimechanganya, sasa anazomewa kwao, je akienda Arusha au Nyamagana-Mwanza itakuwaje? Kazi ipo.
   
 14. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #14
  Jan 13, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Kweli sheria ni msumeno, imeanza kwa kumkata aliyeishabikia ipitishwe bungeni. Hadi katiba itakapopatikana patakuwa pamechimbika sana.
   
 15. m

  mama kubwa JF-Expert Member

  #15
  Jan 13, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 2,408
  Likes Received: 1,965
  Trophy Points: 280
  Wanafikiri wananchi hawakuusikiliza mjadala ule bungeni waanze kuweka yao, wakati huo umepita kila mtu anajua ubabe waliotumia ccm kwenye mjadala huo kwa manufaa yao. Sasa wameshaanza kupata malipo na bado.
   
 16. T

  Tata JF-Expert Member

  #16
  Jan 13, 2012
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,730
  Likes Received: 646
  Trophy Points: 280
  Wewe subiria tu wenzako ndio wanakusanya maoni hivyo. Ukija kushtuka "wameshahuisha" katiba kukidhi matakwa yao.
   
 17. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #17
  Jan 13, 2012
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Wasira asijidai kupotezea, sheria wameipitisha wenyewe kwa ubabe wao wa Ki-ccm sasa wananchii wamegundua janja ya nyani.
   
 18. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #18
  Jan 13, 2012
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Wazee waliochoka akili kama Wasira huwa wananitia kichefuchefu sana.
   
 19. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #19
  Jan 13, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  i hope ningekua eneo la tukio ningecheka mpaka nichanganyikiwe cause I HATE THIS OLD MEN.
   
 20. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #20
  Jan 13, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Utawezaje kuamini wakati habari hii haijatoka gazeti la Uhuru? Ila habari hii ni kweli hata kwenye magazeti tunayoyaamini (sio wewe) imetoka.
   
Loading...