Fujo za kisiasa ni zipi?

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,603
8,741
Watanzania wengi wanachanganywa sana na wanasiasa wanatumia maneno bila kuyaelezea vizuri au kutoa ushahidi. Polisi, CCM na Rais wa Tanzania kwa wao mkutano wa aina yeyote kama wa katiba au kuita Watanzania kujadili kitu chochote kama sio CCM wanaita fujo! au uvunjaji wa amani!. Yaani umeita Watanzania kuongea hoja sehemu hata kwenye kumbi za ndani bado inaitwa fujo au uvunjifu wa amani.

Serikali inavyosema baaada ya uchanguzi mikutano hairuhusiwi zaidi ya ile ya chama ni ujinga wa ajabu maaama vyama vimewekwa ili kuwakilisha wananchi sio kufanya mikutano ya kuongea wenyewe. Yaani ikitokea kitu hawakipendi au kama wanataka maoni ya wananchi wataongea nao wapi! huwezi kusema mambo yanayotokea sasa kwa maisha wa watu wasubiri mpaka uchaguzi kuyajadili wakati ni mambo ambayo wananchi yanawahusu kwa muda huu. Huwezi kusubiri miaka 5 kuongelea mambo ya mwaka huu mfano Corona miaka mitano inaweza isiwepo sasa wanachama na wananchi kwa ujumla wataweza kujadili vipi vitu vya kila siku.

Lakini Rais samia amekuwa anapotosha si kweli kwamba nchi za nje kama US hakuna mikutano baada ya uchaguzi! Trump ameshidwa na anafanya mikutano mingi tu na wala sio mgombea na uchaguzi umemalizika mwaka jana tu. Sasa Rais Samia anavyotaka kumuiga Magu kwa kudanganya au kupotosha Watanzania kama vile hawajui kitu hawezi kufanikiwa kwenye hili.

Tupende tusipende Tanzania sio nchi ya Chama kimoja. Hebu tutoe mfano kwa Chadema wanachama waliojiandikisha ni zaidi ya milion 7 ina maana ukiweka na familia na watu wa karibu unaweza ukawa na watu milioni 20 kati ya milioni 60 wanao unga mkono hiki chama hii ni 30% bado ATC ....... Sasa tukiwa na mfumo wa kufikiri kwamba asilimia 40% au zaidi hawana umuhimu au mawazo na watakuwa wapongezaji tu sio ukweli na haitawezekana. Hivyo usalama utatokana na haki sio maendeleo kama wanavyofikiria maana kuna wananchi ambao wataona mapungufu hata tuwe na nini. Dunia ni kujilinganisha na nchi nyingine sio kusema nimefanya hiki au kile



 
Sheria zifuatwe, na sio matamko ya ajabu ajabu kwa fikra za mtu mmoja.

Watu waachwe wafanye siasa kwa mujibu wa sheria.
 
Wanaouliza kwa nini Mbowe amekamatwa sasa na si vinginevyo wanasahau kuwa Mbowe, Lema, Meya wa zamani Ubungo Boniface walikamatwa mara baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu kutangazwa na kabla Rais hajaapishwa kwa kuchochea maandamano yasiyo na kikomo kupinga matokeo. Mambosasa alihojiwa na vituo vya ITV na TBC na kutoa madai hayo hayo ya ugaidi.
 
Back
Top Bottom