Fujo za Iramba: Waliofanya fujo wanatoka Dar (soma majina)

Kwa kweli, suala la kwenda kurusha mawe katika mikutano ya watu wengine, liangaliwe kwa makini. tunakwenda 2014 - 15, kila mtu yuko hatarini, bila kujali chama. Kama kuna watu wanachochea haya, hawatutakii mema hata kidogo.
 
[h=2]Nukuu ya maandishi ya jumbe za simu za kutishwa kuuawa alizotumiwa Mwigulu Nchemba [/h] 18/07/2012
0 Comments

Baadhi ya wabunge wa CHADEMA, wamehusishwa na mauaji ya Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wa Kata ya Ndago wilayani Iramba mkoani Singida, Yohana Mpinga (30).

Akizungumza bungeni jana, Mbunge wa Iramba Magharibi (CCM), Mwigulu Nchemba alisema kabla ya mauaji hayo anayoona yalipangwa, alitishiwa kuuawa kwa kutumiwa ujumbe mfupi wa simu na wabunge hao kutokana na mijadala yake bungeni.

Nchemba alitoa madai hayo alipoomba Mwongozo wa Spika akitumia Kanuni ya Bunge ya 47 inayohusu kusitishwa kwa shughuli za Bunge ili kujadili jambo la dharura la Taifa.

Sehemu ya ujumbe huo ambao Spika wa Bunge, Anne Makinda alimzuia kuusoma, unamtaka Mwigulu asijifanye anajua, kwani mwenzake Chacha Wangwe (Marehemu Mbunge wa Tarime) alijifanya anajua na “sasa yuko wapi?” Ujumbe mwingine ulimwambia kuwa skafu ya Bendera ya Taifa anayovaa shingoni, itageuka sanda yake.

Akiomba Mwongozo huo, Nchemba alisema kutokana na tukio la kinyama lililotokea jimboni mwake juzi la kuuawa kwa Mpinga na watu wanaodaiwa kuwa wafuasi wa CHADEMA, aliomba Bunge liahirishwe ili suala hilo lijadiliwe kwa kina.

“Naomba tuahirishe Bunge tujadili suala hili, kwa kuwa inaonesha kilichotokea kilipangwa, nilipokea SMS (ujumbe mfupi) katika simu yangu za kunitishia kuuawa kutokana na mijadala ninayochangia bungeni na namba za walionitumia SMS zimebainika kuwa ni za wabunge wa CHADEMA,” alisema Mwigulu.

Alisema namba za simu zilizokuwa zikitumika kumtumia ujumbe huo mfupi alizipeleka Polisi na tayari wabunge hao waliomtishia maisha wamebainika majina yao na hatua zaidi zitachukuliwa.

Pamoja na kukataa kutaja majina ya wabunge hao, Nchemba nje ya Bunge alionesha ujumbe mfupi aliotumiwa ambao unasema:

  1. “Hivi wewe unajiamini nini? Kwa nini unatusonga hivyo? Unadhani nchi hii ni ya CCM milele? “Utajutia kimbele mbele chako. Unadhani ni wewe tu unayejua sana? Ukabila kwenye chama chetu unakuhusu nini, hata kama ni kweli, kwa nini kututia aibu?”
  2. “Hata ufanyeje, 2015 tunaingia Ikulu na mjengoni tutajaa, Wangwe alijifanya kujua kama wewe leo yuko wapi?”
  3. “Bendera unayovaa kila siku shingoni itageuka sanda yako. Kila mtu ana haki ya kuvutia kwake, lakini wewe umezidi. Hatuwezi kuitema keki tuliyokwishaionja”.
  4. “Fahari yako leo, itageuka kilio kwako. Utatutambua.”

Hata hivyo, Spika Anne Makinda alimkatisha Nchemba asiwataje kwa majina wabunge hao waliomtumia ujumbe mfupi wa kutishia kumwua na kumtaka aiachie Polisi ishughulike na jambo hilo, ambapo pia aliukataa Mwongozo wa kuahirisha kikao.
 
Watanzania, serikali yetu na Chama cha Mapinduzi wamezidi kutudharau, kutuonea, kutunyanyasa na kufanya hila za kila namna.

Hii ni aibu kubwa, kati ya Vijana waliofikishwa mahakamani leo ambao polisi wamefanikiwa kuwafikisha mahakamani ni 12. Vijana watatu ni wa Ndago, Josia Israel (Katibu wa CHADEMA), na wenzake Abel Paulo wa Ndago, na Athumani Husein wa Ndago. (hao kwa mujibu wa maelezo ni Wafuasi wa CHADEMA), ni wakaazi wa ndago na wamedhaminiwa leo wapo nje kwa dhamana.

Kizungumkuti ni kuwa VIJANA wengine Saba, walioletwa kwa kusababisha fujo ni wakaazi wa Dar. Hawa ndio wanasadikiwa kuwa kundi la vijana waliopata mafunzo yakutesa watu pale Ulemo, Jimbo la Iramba Magharibi, siku chache kabla ya Uchaguzi wa Igunga, na waliendesha vitendo vya Kikatili katika Uchaguzi wa Arumeru. Hao wamekosa dhamana, vijana wa Singida wameogopa kuwadhamini kwanza kwa kuwa hawafahamiki, na ni wa Dar je wasiporudi siku ya kesi itakuwaje?.

Hata hivyo hawa vijana wamejitambulisha katika hati ya Mashtaka kuwa ni Abdala Mbwana Kingwande, (Mndengereko), ana Miaka 36, Mwislamu, Mfanyabiashara na Mkaazi wa Segerea Dar es Salaam.

Wa Pili Ni Nasri Salehe (Mnyamwezi), ana umri 28, Mwislamu, anakaa karikaoo, na ni mfanyabiashara. Wa tatu ni Laizimu Njama, ni MMakua, ana miaka 42, Mwislamu, anatokea Tandika/Temeke Dar es salaam. Wa Nne ni Mohamedi Abdalaa, Mluguru, ana miaka 34, Mwislamu, anakaa Kibamba Dar es Salaam, wa Tano ni Rudoviki Muganyizi, Mhaya, ana miaka 32, Mkristo, Ni Injinia. Wa Sita ni Justini Sangu, Mfipa, ana miaka 40, Mkristo anakaa Dar na ni mfanyabiashara. Wa Saba ni Salumu Ali Rashidi, ni Mmwela, ana miaka 26, Mwislamu, ni Mkaazi wa Tandika Jijijini Dar.

Maswali magumu ni haya: Tumetoka Mahakamani viongozi wa CCM wanahaha kuwadhamini hao vijana saba toka Dar. Je hao vijana, wafanyabiashara na injia wana Uhusiano gani na CCM? Je kama ni kweli ni wafanya biashara wa mazao kama walivyojitambulisha ilikuwaje waje kwenye Mkutano wa CHADEMA, ilhali Mkutano wa CHADEMA ulikuwa ni wa sera za chama na hakuna Dalali wamazao katika Mikutano ya Chadema?. Muda wote wamehudumiwa na viongozi wa CCM je CCM ilikuwa na maslahi gani na wafanyabiashara hao?

Ninaacha wazi wanafalsafa mjiulize maswali, na majibu muweke ninyi. Ila Mwigulu Nchemba, amehonga vijana shs 10,000/- wamefanya fujo na kusababisha kifo cha mwenzao.
Hivi ukiwa umesafiri kwenye shughuli zako na kuna mkusanyiko wa watu na ukaona ni chama fulani kinamwaga sera huruhusiwi kusikiliza kwasababu si mkazi wa eneo hilo?Ngoja nikupe mkasa miaka fulani nilikuwa napita maeneo ya magomeni sokoni polisi wa jiji walikuwa wanakamata wafanyabiashara wanaouza bidhaa nje ya soko walitukamata mimi na ndugu yangu na tulikuwa hatuhusiki na tulifikishwa polisi na mahakamani na kusomewa mashitaka ambayo hakuna hata moja lituhusu na dhamana ikataka kufungwa.Hivyo haimanishi kila anayekamatwa kwenye mkusanyiko wenye fujo na vyombo vya dola na kutuhumiwa ni kweli anahusika.
 
kimsingi Mwigulu huongoza umwagaji damu ili kulinda maslahi yake ndani ya chama,alifanya hivyo Igunga,Arumeru na sasa jimboni kwake akidhani kwa kufanya hivyo angeichafua CDM.
 
Nimeshaanza kuona hatari ya hawa jamaa ifikapo 2015. Inavyooneka wako tayari kufanya lolote ilimradi wabaki madarakani. kwao wao kuachia madaraka kwa kukubali kushindwa itakuwa kama kukubali uwe mwisho wa dunia. hii ni kutokana na vimbwanga wanavyovifanya.
 
Sisiem sasa mbona mnachoka vibaya!!!? Heb tuuze sera kwa wananchi wanunue wenyewe si kwa kuhonga jamaniii!!!!!
 
[h=6]TAARIFA RASMI MBUNGE 1 WA CHADEMA AMUOMBA RADHI MWIGULU KWA KUMTUMIA MSG HIZI mwigulu ampa sharti la kutoa ufafanuzi kwa watanzania,,,mbunge huyo akasema viongozi wa chama chake wamekataa yeye kuomba radhi hadharani" hasira za kichaga:
1. 'Hivi wewe unajiamini nini? Kwa nini unatuzonga hivyo? Unadhani nchi hii ni ya ccm milele? Utajutia kimbelembele chako. Unadhani ni wewe tu unayejua sana? Ukabila kwenye chama chetu unakuhusu nini hata kama kweli kwa nini kututia aibu? Hata ufanyeje 2015 tunaingia ikulu na mjengoni tutajaa, Wangwe alijifanya kujua kama wewe leo yuko wapi?'

2. 'Bendera unayovaa kila siku shingoni itageuka sanda yako. Kila mtu ana haki ya kuvutia kwake lakini wewe umezidi. Hatuwezi kuitema keki tuliyokwishaionja'

3. 'Fahari yako itageuka kilio kwako. Utatutambua'

SOURCE: Tanzania Daima July 17, 2012.

masikini CHACHA WANGWE kumbe hawa jamaa walikuua!!
[/h]
 
SOURCE: Tanzania Daima July 17, 2012.

masikini CHACHA WANGWE kumbe hawa jamaa walikuua!!

Mh!naona umemkumbuka Chacha Wangwe!
Naomba pia uwakumbuke hawa:
(1) Imran Komba
(2)Horace Kolimba
(3)Edward Moringe Sokoine
(4)Kasim Hanga(Alizikwa wapi?)
(5)Gilman Rutihinda
(6)Steven Kibona
(7)Daudi Balali
 
anayeipenda ccm anatakiwa kupimwa akili,je anaipenda kwa dhati?au kuna maslahi,je anajua ccm wanachokifanya? chadema endeleni kutoa elimu ya raia.
 
Watanzania, serikali yetu na Chama cha Mapinduzi wamezidi kutudharau, kutuonea, kutunyanyasa na kufanya hila za kila namna.

Hii ni aibu kubwa, kati ya Vijana waliofikishwa mahakamani leo ambao polisi wamefanikiwa kuwafikisha mahakamani ni 12. Vijana watatu ni wa Ndago, Josia Israel (Katibu wa CHADEMA), na wenzake Abel Paulo wa Ndago, na Athumani Husein wa Ndago. (hao kwa mujibu wa maelezo ni Wafuasi wa CHADEMA), ni wakaazi wa ndago na wamedhaminiwa leo wapo nje kwa dhamana.

Kizungumkuti ni kuwa VIJANA wengine Saba, walioletwa kwa kusababisha fujo ni wakaazi wa Dar. Hawa ndio wanasadikiwa kuwa kundi la vijana waliopata mafunzo yakutesa watu pale Ulemo, Jimbo la Iramba Magharibi, siku chache kabla ya Uchaguzi wa Igunga, na waliendesha vitendo vya Kikatili katika Uchaguzi wa Arumeru. Hao wamekosa dhamana, vijana wa Singida wameogopa kuwadhamini kwanza kwa kuwa hawafahamiki, na ni wa Dar je wasiporudi siku ya kesi itakuwaje?.

Hata hivyo hawa vijana wamejitambulisha katika hati ya Mashtaka kuwa ni Abdala Mbwana Kingwande, (Mndengereko), ana Miaka 36, Mwislamu, Mfanyabiashara na Mkaazi wa Segerea Dar es Salaam.

Wa Pili Ni Nasri Salehe (Mnyamwezi), ana umri 28, Mwislamu, anakaa karikaoo, na ni mfanyabiashara. Wa tatu ni Laizimu Njama, ni MMakua, ana miaka 42, Mwislamu, anatokea Tandika/Temeke Dar es salaam. Wa Nne ni Mohamedi Abdalaa, Mluguru, ana miaka 34, Mwislamu, anakaa Kibamba Dar es Salaam, wa Tano ni Rudoviki Muganyizi, Mhaya, ana miaka 32, Mkristo, Ni Injinia. Wa Sita ni Justini Sangu, Mfipa, ana miaka 40, Mkristo anakaa Dar na ni mfanyabiashara. Wa Saba ni Salumu Ali Rashidi, ni Mmwela, ana miaka 26, Mwislamu, ni Mkaazi wa Tandika Jijijini Dar.

Maswali magumu ni haya: Tumetoka Mahakamani viongozi wa CCM wanahaha kuwadhamini hao vijana saba toka Dar. Je hao vijana, wafanyabiashara na injia wana Uhusiano gani na CCM? Je kama ni kweli ni wafanya biashara wa mazao kama walivyojitambulisha ilikuwaje waje kwenye Mkutano wa CHADEMA, ilhali Mkutano wa CHADEMA ulikuwa ni wa sera za chama na hakuna Dalali wamazao katika Mikutano ya Chadema?. Muda wote wamehudumiwa na viongozi wa CCM je CCM ilikuwa na maslahi gani na wafanyabiashara hao?

Ninaacha wazi wanafalsafa mjiulize maswali, na majibu muweke ninyi. Ila Mwigulu Nchemba, amehonga vijana shs 10,000/- wamefanya fujo na kusababisha kifo cha mwenzao.

Relax; hakuna kamba ndefu isiyokuwa na ncha; Penye ukweli uongo hujitenga, freedom is comming tomorrow; kabati lao la ujanjaujanja linakaribia kukauka, relax.
 
Mh!naona umemkumbuka Chacha Wangwe!
Naomba pia uwakumbuke hawa:
(1) Imran KombE
(2)Horace Kolimba
(3)Edward Moringe Sokoine
(4)Kasim Hanga(Alizikwa wapi?)
(5)Gilman Rutihinda
(6)Steven Kibona
(7)Daudi Balali
Gibons Mwaikambo
 
Back
Top Bottom