Fujo za Iramba: Waliofanya fujo wanatoka Dar (soma majina)

MADORO

Senior Member
Nov 12, 2011
198
117
Watanzania, serikali yetu na Chama cha Mapinduzi wamezidi kutudharau, kutuonea, kutunyanyasa na kufanya hila za kila namna.

Hii ni aibu kubwa, kati ya Vijana waliofikishwa mahakamani leo ambao polisi wamefanikiwa kuwafikisha mahakamani ni 12. Vijana watatu ni wa Ndago, Josia Israel (Katibu wa CHADEMA), na wenzake Abel Paulo wa Ndago, na Athumani Husein wa Ndago. (hao kwa mujibu wa maelezo ni Wafuasi wa CHADEMA), ni wakaazi wa ndago na wamedhaminiwa leo wapo nje kwa dhamana.

Kizungumkuti ni kuwa VIJANA wengine Saba, walioletwa kwa kusababisha fujo ni wakaazi wa Dar. Hawa ndio wanasadikiwa kuwa kundi la vijana waliopata mafunzo yakutesa watu pale Ulemo, Jimbo la Iramba Magharibi, siku chache kabla ya Uchaguzi wa Igunga, na waliendesha vitendo vya Kikatili katika Uchaguzi wa Arumeru. Hao wamekosa dhamana, vijana wa Singida wameogopa kuwadhamini kwanza kwa kuwa hawafahamiki, na ni wa Dar je wasiporudi siku ya kesi itakuwaje?.

Hata hivyo hawa vijana wamejitambulisha katika hati ya Mashtaka kuwa ni Abdala Mbwana Kingwande, (Mndengereko), ana Miaka 36, Mwislamu, Mfanyabiashara na Mkaazi wa Segerea Dar es Salaam.

Wa Pili Ni Nasri Salehe (Mnyamwezi), ana umri 28, Mwislamu, anakaa karikaoo, na ni mfanyabiashara. Wa tatu ni Laizimu Njama, ni MMakua, ana miaka 42, Mwislamu, anatokea Tandika/Temeke Dar es salaam. Wa Nne ni Mohamedi Abdalaa, Mluguru, ana miaka 34, Mwislamu, anakaa Kibamba Dar es Salaam, wa Tano ni Rudoviki Muganyizi, Mhaya, ana miaka 32, Mkristo, Ni Injinia. Wa Sita ni Justini Sangu, Mfipa, ana miaka 40, Mkristo anakaa Dar na ni mfanyabiashara. Wa Saba ni Salumu Ali Rashidi, ni Mmwela, ana miaka 26, Mwislamu, ni Mkaazi wa Tandika Jijijini Dar.

Maswali magumu ni haya: Tumetoka Mahakamani viongozi wa CCM wanahaha kuwadhamini hao vijana saba toka Dar. Je hao vijana, wafanyabiashara na injia wana Uhusiano gani na CCM? Je kama ni kweli ni wafanya biashara wa mazao kama walivyojitambulisha ilikuwaje waje kwenye Mkutano wa CHADEMA, ilhali Mkutano wa CHADEMA ulikuwa ni wa sera za chama na hakuna Dalali wamazao katika Mikutano ya Chadema?. Muda wote wamehudumiwa na viongozi wa CCM je CCM ilikuwa na maslahi gani na wafanyabiashara hao?

Ninaacha wazi wanafalsafa mjiulize maswali, na majibu muweke ninyi. Ila Mwigulu Nchemba, amehonga vijana shs 10,000/- wamefanya fujo na kusababisha kifo cha mwenzao.
 
mmmh kuhonga watu ili wafanye fujo..ni tuhuma nzito hizi aise
 
Mkuu Madoro,
Me sijakuelewa unaposema Vijana hao Wanahudumiwa na CCM wakati TBCCM imetangaza waliokamatwa na kufikishwa mahakamani ni CDM!?
 
salale haya sasa na kule kuomba muongozo bungeni sasa mwigulu umeumbuka uje ujibu tuhuma hapa. wenzio wameeleza ukweli wote kuwa wewe uliwasafarisha na kuwagharimia kila kitu. aibu yenu nyinyiem
 
kama ni kweli jeshi la polisi lifanye kazi bila upendeleo hao vijana wahojiwe ili ukweli upatikane.
 
Maswali:

1. Hao vijana waliingia lini Singida? na walipanga kuondoka lini?

. Walisafiri pamoja? Na wanajuana? kama ndio kwa muda gani?

3. Walishafika Singida kabla? Kama jibu ndiyo, lini na kwa shughuli gani? Walikuwa wote?

4. Dar es Salaam wanafanya biashara pamoja, na eneo lao la biashara liko mahali gani?

5. Walisikia toka kwa nani kwamba CHADEMA walikuwa na mkutano? na waliambiwa no viongozi gani watahutubia?

6. Mbali na kuhudhuria mkutano wa CHADEMA, walifanya nini kingine siku/kabla ya mkutano huo?

7. Wanamjua Mwigulu Nchemba? au walishasikia hilo jina? na wanafikiri ni nani?

8. Wametembelea sehemu gani nyingine ndani na nje ya Tanzania kwa miezi 12 iliyopita?

9. Mbali na mkoa wa Singida ni mkoa gani mwingine huwa wananunua mazao, na lini mara ya mwisho wamenunua huko?

10.Wanaweza kusema huu ni msimu wa mazao gani Singida? Na mkoa gani unazalisha nafaka kwa wingi zaidi hapa Tanzania?
 
Imekuwa ni taabia yao kuchukua vijana kutoka sehemu moja kwenda kufanya fujo sehemu nyingine kwa ujira mbuzi hii yote katika kuonyesha kuwa kundi flani ni wafanyafujo ila Mungu siku zote akiamua liwe litakuwa lakini siyo binadamu.Mahakama inapogeuzwa kwama Chimbo la kuficha uozo!Shame!
 
Fikirieni ccm inashinda uchaguzi 2015 na Rais huyo mpya anamteua MWIGULU NCHEMBA kua waziri wa mambo ya ndani...hee mbona tutakua tunacharazwa bakora mtaani..maana huyu jamaa anaonekana ana roho ya kikatili,kijambazi na ni wa kuogopwa mno
 
Mkuu Madoro,
Me sijakuelewa unaposema Vijana hao Wanahudumiwa na CCM wakati TBCCM imetangaza waliokamatwa na kufikishwa mahakamani ni CDM!?
TBCCM ni full propaganda, very unprofessional! ndiyo tatizo la kukumbatia unshuled people, wanaunga unga tu huku wanakimbizana na madili machafu harafu wanaanza kudharau wanaosotea taaluma kwa miaka mingi tena kwa kuvumilia shida na mateso shuleni na vyuoni.
 
Mkuu Madoro,
Me sijakuelewa unaposema Vijana hao Wanahudumiwa na CCM wakati TBCCM imetangaza waliokamatwa na kufikishwa mahakamani ni CDM!?

Ndiyo ujiongoze mwenyewe kama CCM wanaweza kuwapelekea chai mahabusu wa CDM
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom