Fujo mashuleni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fujo mashuleni

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by MotoYaMbongo, Aug 22, 2008.

 1. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #1
  Aug 22, 2008
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,859
  Likes Received: 200
  Trophy Points: 160
  Jamani mi naona sasa serikali imezika kabisa elimu nchini. Tunapenda sana kuiga ya wazungu wakati sisi ni waafrika. Tabia za watoto wetu tunazijua vizuri. Hivi kweli fimbo mashuleni zifutwe hizi shule zitaenda? Watoto adabu hawana, nataka viboko vifutwe halafu viongozi waje waendeshe hizi shule japo kwa mwezi mmoja tu ili waone mziki wake. Hakyanani watakimbia. Adhabu za kawaida watoto wanaona kama kazi wanazofanya kwao sa sijui mwl afanyeje wakati fimbo haziruhusiwi? Wanafunzi nawashauri mchome tu haya mashule ili wajenge mengine. Halafu mpumbavu mmoja akasema kuwa eti ikitokea fujo shuleni wakuu watafukuzwa. Sasa Ruvuma leo wamesimamishwa masomo wanafunzi kuanzia form one, je na hilo nalo ni kosa la walimu? Wanafunzi wamepiga hadi wananchi, tena ktk kilabu cha pombe. Siku fimbo zikifutwa rasmi walimu nawashauri muangalie maslahi tu, wakivuta bangi waacheni, wakinywa pombe acheni, wakikataa kusafisha mazingira yote acheni tu, halafu mpumbavu ataekuja kukagua mumwachie yeye aoneshe mfano kwa kuiendesha shule japo wiki moja bila kutumia fimbo na mazingira yawe masafi. akiweza basi awafundishe mbinu alizotumia kumuendesha mtoto wa kiafrika bila kiboko na akaenda ktk mstari.
   
 2. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #2
  Aug 22, 2008
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,859
  Likes Received: 200
  Trophy Points: 160
  Ndo maana hata spika Six amemwambia JK kwamba haki za binadam zinaendana na mazingira sometimes. Haki ya binadam kwa watoto wetu zinataka kuvuka mipaka. Sasa tujiandae kupigwa mawe, kutukanwa, na kudhalilishwa kutokana na hizi HAKI ELIMU.
   
Loading...