Fueling the parallel economy: Kutumia benki sasa ni hatari?

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
15,314
24,173
Wadau JF,

Mnalionaje hili, sasa hivi kuweka pesa yako benki unajitakia umaskini.

Jamaa wa TRA kiulaini wanakuja kuichota kama vile ukakasi wowote ni mali yao.

Kutumia benki kwa malipo halali sasa ni hatari.

Matokeo ya dhahiri ni aidha watu kutopeleka kabisa fedha benki zetu au kudai malipo kwa huduma au bidhaa mbadala(Barter Trade).

Hii italeta parallel economy ambapo serikali itakosa kabisa mapato.

TRA mumo humu tupeni maoni.
 
Na benki kwanini waruhusu pesa za mteja A zichukuliwe na mteja B?

Kama hii inafanyika bila kufuata utaratibu wa kisheria (mahakama) kuamuru fedha za mteja fulani zitaifishwe, basi benki husika na aliyechukua wanakuwa na makosa/hatia.

Nenda mahakamani washitaki na utarudishiwa fedha yako yote na riba juu!
 
Ndio maana mliambiwa msajili simu zenu na vitambulisho ili wakifatilia hizo transaction zenu humo kwenye simu, kwisha mchezo hapo
unatumiwa makadirio ya kulipa kodi 🤣
 
TRA wana uwezo kisheria kuchukua pesa katika account
Na benki kwanini waruhusu pesa za mteja A zichukuliwe na mteja B?

Kama hii inafanyika bila kufuata utaratibu wa kisheria (mahakama) kuamuru fedha za mteja fulani zitaifishwe, basi benki husika na aliyechukua wanakuwa na makosa/hatia.

Nenda mahakamani washitaki na utarudishiwa fedha yako yote na riba juu!
 
TRA wana uwezo kisheria kuchukua pesa katika account

Siyo TRA tu, hata wewe unaweza kwenda kuchukua pesa ya mtu mwingine kwenye Bank Account take huyo mtu/taasisi/kampuni ILA NI PALE TU unapokuwa umefuata utaratibu wa kisheria kupata ruhusa hiyo...!

Kwa hiyo tusidanyane hapa kuwa TRA wana mamlaka yao tu bila kupitia mahakamani. Kwa kifupi, hakuna mamlaka hayo ya kienyeji tu...
 
  • Thanks
Reactions: _ID
Na benki kwanini waruhusu pesa za mteja A zichukuliwe na mteja B?

Kama hii inafanyika bila kufuata utaratibu wa kisheria (mahakama) kuamuru fedha za mteja fulani zitaifishwe, basi benki husika na aliyechukua wanakuwa na makosa/hatia.

Nenda mahakamani washitaki na utarudishiwa fedha yako yote na riba juu!

Benki inakuwa imeshirikiana na wezi kuiba pesa ya mteja wao.

Mtu unakwenda mahakamani na Benki inakuwa ni shahidi.
 
Na bodi ya mkopo wananoa panga waende kuzikata huko huko kwenye benki
IMG_20201206_071929.jpg
 
Back
Top Bottom