Fuel consumptions katika Neutral (N) na Drive (D)

DOKEZO

Member
Jan 17, 2014
82
125
Habari,

Naomba kuuliza
Je,ni kweli wakati gari Toyota wish unapokuwa kwenye mteremko na ukaweka Neutral inakuwa NO FUEL CONSUMPTIONS kwa muda ule gari inatembea ikiwa kwenye neutral??

Je ni kweli unapokuwa umeiweka kwenye Drive (D) bila kukanyaga accelerator huku gari inaendelea kutembea barabara tambarare of coz mwendo unakuwa mdogo napo pia kunakuwa NO FUEL CONSUMPTIONS kwa muda ule??
 

Davooo

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
486
1,000
Mkuu ,hata Mimi (sio fundi)lakini naamini gari ikiwa neutral mafuta hayaliki(hili nalifanya sana kama kuna mtetemko)
Kuhusu drive hata kama upo tambarare mafuta yanaenda kwakuwa umehusisha system
 

Hazchem plate

JF-Expert Member
Feb 25, 2011
9,779
2,000
Aliwadanganya nani kuwa mafuta hayaliki gari ikiwa neutral??? Kama hayaliki kwann usiwe unaliacha gari neutral usiku kucha wakati unalala.
As long as Engine ina run basi jua mafuta yanatumika whether ni neutral au ipo kwenye D.

Utofauti ni kwamba gari ikiwa neutral, Gear box na Prime mover ambayo ni engine vinakuwa dis engaged. Kwa maana hiyo gari litakuwa jepesi ukiwa upo mtermkoni. Na incase ukiwa umeweka D gari itakuwa nzito. Maana gari inashuka mlima kwa kutegemea inclination ya surface at the same time D peke yake bila kukanyaga mafuta gari inakuwa na mwendo wa tratibu.
 

Eminentia

JF-Expert Member
Jun 5, 2014
2,330
2,000
hata ikiwa neutral yanatumika yale ya kuifanya gari iwe silence.....kama tachometer inafanya kazi we jua kama mshale hauko kwenye 0 basi mafuta yanatumika
 

concious mind

JF-Expert Member
Jun 27, 2012
817
500
kimsingi kwenye mtelemko kama gari ipo kwenye N inakula zaidi mafuta kuliko gari ikiwa kwenye D ukiacha kukanyaga mafuta, ikiwa unashuka kwenye mtelemko gari ipo D matairi yanaendesha engine hivyo haivuti mafuta, ikiwa ipo N itahitaji mafuta kuzungusha engine .
 

That Gentleman

JF-Expert Member
Dec 16, 2016
574
1,000
Mafuta hulika pote, katika N na D.
Ili engine i-run inahitaji mafuta yaingie kwenye combustion chamber
 

Hardbody

JF-Expert Member
Jan 25, 2017
2,222
2,000
Mafuta hulika lakini kidogo ukiweka kwenye N (neutral) na ikiwa kwenye D (drive) mafuta hulika kwa kiasi kikubwa zaidi
 

pipikijiti

JF-Expert Member
Apr 25, 2017
309
500
Nimefuatilia comments zenu wote, kila mtu jibu analikaribia jibu ngoja tuwekane sawa hapa kwanza jua kwamba injini ikisha washwa mafuta ni lazima yatumike hata kama ni kwa kiasi kidogo lakini ni lazima ya tumike

Kuhusu kwenye D na N,,hapo kwenye ulaji ni lazima utofautiane ijapokuwa ni kwa kiwango kidogo sana,gari ikiwa kwenye N maana yake ni injini tu inayozunguka kwahiyo gari itakuwa na mzigo wa kuzungusha injini tu
- ila gari ikiwa kwenye D au Drive maana yake injine imeshakuwa connected na difu ya gari maaana yake hapa sasa gari itakuwa na kazi mbili za kufanya yani kuzungusha injini pamoja na matairi yake kwahyo ni lazima compression kwenye injini iongezeke ili kuzungusha difu ndo results ya matairi kuzunguka kwa maana hiyo ni lazima ulaji wa mafuta kwenye D uwetofauti na wa N

Huku ninapoishi kuna kampuni flani ya usafirishaji wa mizigo na baadhi ya madereva ni rafiki zangu katika stori stori huwa wanasema kabisa ukitembelea mara nyingi N safarini lazima upate mafuta mengi yanayobaki na hivyo jamaa huwa wanayatoa na kuuza na huwa wanapata hadi elf 70 hadi 50 kwenye mafuta tu per root

Ingawa kitalaamu,watalaam wameonya usipende kutembelea N mara kwa mara,gearbox inaweza pata itirafu.asanteni
 

Negrodemus

JF-Expert Member
Dec 30, 2010
2,310
2,000
Mkuu ,hata Mimi (sio fundi)lakini naamini gari ikiwa neutral mafuta hayaliki(hili nalifanya sana kama kuna mtetemko)
Kuhusu drive hata kama upo tambarare mafuta yanaenda kwakuwa umehusisha system
Ushauri wangu usirudie kuweka N wakati unashuka miteremko angalia aina ya mlima kuna D 2 na L tumia hizo gia. Kufunga break ili upunguze mwendo wakat gari ipo kwenye D ni tofaut na wakati gar ipo kwenye N kwenye N gari inakua nyepesi as hakuna muunganiko wa injini na dif via gia box asilimia za break kufail au gari kuzima ni mkubwa.
 

J33

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
1,509
2,000
Mkuu ,hata Mimi (sio fundi)lakini naamini gari ikiwa neutral mafuta hayaliki(hili nalifanya sana kama kuna mtetemko)
Kuhusu drive hata kama upo tambarare mafuta yanaenda kwakuwa umehusisha system
Ukiwasha gar bila kutembea yanalika itakuwa ikiwa kwenye mwendo!? Labda uzime iserereke kama mkokoteni.
 

Negrodemus

JF-Expert Member
Dec 30, 2010
2,310
2,000
Habari,

Naomba kuuliza
Je,ni kweli wakati gari Toyota wish unapokuwa kwenye mteremko na ukaweka Neutral inakuwa NO FUEL CONSUMPTIONS kwa muda ule gari inatembea ikiwa kwenye neutral??

Je ni kweli unapokuwa umeiweka kwenye Drive (D) bila kukanyaga accelerator huku gari inaendelea kutembea barabara tambarare of coz mwendo unakuwa mdogo napo pia kunakuwa NO FUEL CONSUMPTIONS kwa muda ule??
Tumia N kama gari inavutwa
Ukitumia N ratio inakuwa chini ukiweka D inatumia mafuta mengi kufikia ratio ua mwendo unaotaka ikiwa kwenye D tayar inakua ime regulate matumiz ya mafuta hata ukisimama kwenye folen inaweza rudi namba mbili au tatu ukiweka N ukarudisha D jua unaanza na namba moja na itatumia mafuta mengi mpaka kufikia ratio ya gia ya mwendo unaoutaka
 

J33

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
1,509
2,000
Ila na huu udereva wa kutumia N kwenye mteremko ili kupunguza mafuta sijui tunajifunzia WAP. Na huu ujinga bora uufanye kwenye gar manual vinginevyo IPO siku.
 

brightoscar

JF-Expert Member
Dec 29, 2013
244
250
Kama umenunua gari nunua mafuta kama unataka kubana matumizi ya Mafuta tumia public transports
 

Hazchem plate

JF-Expert Member
Feb 25, 2011
9,779
2,000
Haishauriwi kuanza kufanya hizo sarakasi za N na D wakati unaendesha gari, utaharibu gari kwa kusave mafuta ambayo hayana kipimo.

Labda kama foleni ni kubwa sana japo pia wadadisi wanasema P na N ni yale yale.
P na N ni tofauti mkuu. Gari ikiwa P inakuwa kwenye brake while ikiwa kweny N inakuwa free so unaweza hata isukuma ikaenda. Kwenye folleni unatakiwa uweke P ili gar isije ikarud nyuma kama kuna kamuinuko. Na kama ukiweka N basi kanyaga na brake au weka hand brake.
 

From Sir With Love

JF-Expert Member
Sep 13, 2010
1,937
2,000
P na N ni tofauti mkuu. Gari ikiwa P inakuwa kwenye brake while ikiwa kweny N inakuwa free so unaweza hata isukuma ikaenda. Kwenye folleni unatakiwa uweke P ili gar isije ikarud nyuma kama kuna kamuinuko. Na kama ukiweka N basi kanyaga na brake au weka hand brake.
Hazchem, sina ubishi na hilo.

Issue ilikuwa ni ulaji wa mafuta kwenye hizo category mbili wakati gari ipo on.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom