JamiiForums
JF Official Account
- Nov 9, 2006
- 6,227
- 5,270
Sekta za Afya na Elimu ndizo sekta zinazobeba uhai wa Taifa... Taifa la watu dhoofu haliwezi kuzalisha vyema na kufanya shughuli zake za maendeleo kwa ufanisi, vivyo hivyo taifa la wajinga haliwezi kufikia malengo ya kiuchumi kwa kuwa elimu ndio ufunguo wa kila kitu katika dunia ya sasa.
Ijumaa ya tarehe 27 Mei 2016, Benki ya Dunia itawasilisha Ripoti yake kuhusu hali ya Utoaji Huduma ya Afya na Elimu (Service Delivery Indicators) ilivyo nchini Tanzania.
Endelea kufuatilia kwenye uzi huu ili uweze kufahamu ni wapi tumeweza, wapi tunahitaji kuongeza mkazo na wapi pa kujiboresha ili tuweze kufikia malengo ya Afya na Elimu Bora kwa kila Mtanzania..
Team ya JamiiForums itakuletea updates za uwasilishwaji wa ripoti hii siku ya uzinduzi hatua kwa hatua kutoka Hyatt Regency Hotel, Dar es salaam..
Tafadhali kuwa nasi kwa ukaribu..