Hechinodemata
JF-Expert Member
- Sep 16, 2016
- 1,467
- 3,228
Tropical Storm Jobo LIVE Images and Tracker | Zoom Earth
LIVE updates, satellite images and tracking maps of Tropical Storm Jobo 2021. Current wind speed 75km/h. Max 100km/h.
zoom.earth
Fungua link hapo kujua kinachoendea juu kimbunga jobo ili kuchua tahadhari madhubuti, Yatupasa kuomba mungu sana atuepushe na janga hili ili kunusuru uharibifu mkubwa wa mali na maisha ya waliopo kwenyw mkondo huo. Tuombe mungu speed izidi kupungua kadri kimbunga kicho kinavyozidi kusogea mchini kwetu
Utabiri unaonesha kimbunga kitatua Dar es salaam kuanzia wakati wa usiku wa saa 9 ukikiwa na speed ya 55km/hr.
Hii ni speed kubwa sana na kinaweza kuacha uharibifu mkubwa. Tunategemea kuwa na ukinzani wa upepo wa baharini utakao punguza zaid speed hiyo ya kimbunga ila itategemea na hali ya hewa baharini kwa wakati huo.
Tahadhar mbalimbali zimetolewa na mamlaka ya hali ya hewa pia na balozi za nchi tofauti zilizoko tanzania juu ya kimbunga hicho. Tahadhari hizo ni pamoja na
1. Usafir wa majini kufuatilia kwa makin hali ya hewa au kutoendesha vyombo baharini
2. Shughuli zote za baharini kutokuwepo kwa wakati huo
3. Wakazi walio maeneo yaliyo ainishwa yatapata adhar ya kimbunga kuchukua tahadhari zote ikiwa ni pamoja na kutoka maeneo hatarishi.
4. Wakazi wa mabondeni na sehemu zenye mafuriko kutoka hayo maeneo, ikimbukwe kimbunga hicho kinaweza ambatana na mvua kubwa.
5. Balozi mbalimbali zimeenda mbali zaidi kuwataka raia wake kutulia majumbani na kuwa mahitaji yote muhimu
6. Wasiendeshe magari siku husika
7. Wafuatilie kwa umakini taarifa zote muhimu watakazo yoa juu ya kimbunga hicho. e.t.c
UTANISAMEHE MIMI SIO MUANDISHI MZURI.