Fuatilia kisa hiki kuhusu simu zetu.Ni jambo la kheri kujua ubaya wa mwenzio ili uishi naye kwa taha


Kkimondoa

Kkimondoa

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2014
Messages
4,473
Likes
4,844
Points
280
Kkimondoa

Kkimondoa

JF-Expert Member
Joined May 31, 2014
4,473 4,844 280
Ni jambo la kheri kujua ubaya wa mwenzio ili uishi naye kwa tahadhari au mkarekebisha ili mjenge familia bora kumbuka kuna hatari ya mmoja akalichuma mkala wote nakuwaacha watoto wakiwa yatima, ngoja nitoe mfano hapa.

Kuna jamaa mmoja alikuwa na mke mzuri kweli kweli, lakin pia bwana huyo alikuwa na rafiki yake waliye kuwa wakifanya kazi pamoja ofisin na ailikuwa rafiki yake kweli kweli kwa maana kwanza alikuwa ni bosi wake hapo kazini

Sasa kumbe yule bosi wake alikuwa akimpenda sana mke wa rafiki yake na alijitahidi sana apate mwanya wa kukutana naye angalau apewe namba ya simu,

Siku moja mume akiwa kazi bosi akatembelea nyumban kwa rafikiye kwa lengo la kufanya namna ya kupata namba ya simu na kweli alifika nyumban kwa bahati akamkuta mlinzi alipo muuliza mama yupo akamwambia hayupo akamwambia naweza pata mawasiliano yake nina shida naye mlinzi akamwambia alisha zuia kutoa namba yake bila ridhaa yake.

Basi bosi akamwambia sasa fanya hivi nipe namba halafu usiseme kwamba nimepita hapa wala umenipa namba ili isije onekana nimeipata kwako kuna maswala ya kiofisi nahitaji niongee naye shemeji .

Basi mlizi akatoa namba kwa vile aliahidiwa pia kupewa hela ya chai baada ya kukamilisha hilo,

Basi bosi akaanza mawasiliano na shemeji yake na kusisitiza yawe ya siri na alianza kwa kurusha tsh. Laki 5 kwenye simu ya shemejie ila akajifanya amekosea lakin akamwambia kuwa ukipenda shemeji yangu hata kama nimekoseaa naweza kukuachia tu kwani vibaya?? Kama tunavo jua wanawake pesa ndio kilevi chao kuwalewesha akaingia kingi baada ya story mbili tatu na shuhuli ikaanzia hapo.

Tukirudi nyuma kidogo huyu bosi alikuwa na tatizo ambalo alilificha sana sababu alikuwa HIV + siri ambayo aliye ijua ni dereva wake pekee na si mwingine sababu ndiye aliye kuwa akimpeleka kupata dawa ya dozi inayo fahamika

Lakini kupitia hilo boss huyu alikuwa anafanya dhambi kubwa sana ya kusambaza ugonjwa huo kwa makusudi kwa kulipa kisasi kwa sababu na yeye aliupata katika mazingira ya kulipizwa kisasi

lakin pia dereva alikuwa karibu sana na mume wa yule dada hivyo alimshirikisha kuhusu hilo hivyo naye alilijua pia kwa undani

Mume alikuwa na tendency ya kupitia pitia simu ya mkewe kwa siri bila mke kujua ndipo siku moja alipo kuta sms mbali mbali ikiwepo na ya mihadi ya kukutana sehemu fulani na bosi akiahidi kumpa mume kajisafari ka siku tatu nne hivi ili wapate nafasi ya kuvunja amri ya sita

Kizuri ni kwamba mume alikuwa mstaarabu na hekima kubwa sana alikaa na mkewe kwa utulivu akamwambia mkewe nashukuru mungu nimelijua hili kabla na naamini mungu yu pamoja na ndoa hii ingawa shetani anataka kutia mkono wake .

Mke akastaajabu akauliza kwa nini baba**** unasema hivyo ??

Mume akamwambia mama ***** tuna watoto wawili pekee na hatuujui mwisho wa maisha yetu nilini, twaweza fikiri tutaishi sana kumbe tukaish kidogo lakin pia twaweza dhani tutaishi kidogo kumbe tutaishi sana na kuishi sana ndio furaha yetu maana tutafaidi matunda ya watoto wetu na kucheza na wajukuu zetu

Mungu ndiye hupanga kifo lakini kipo cha hiyari ambacho mwanadamu hukitafuta mwenyewe na kipo kilicho pangwa na mungu

Akaendelea ''mke wangu tusikitafute kifo cha hiyari bali tukisubiri kifo kilicho pangwa kwa ajili yetu.''

Basi mke akapigwa na butwaa kwa nini leo baba *** anaongea haya ,ndipo mume akaamua kumueleza mkewe kuwa nimeona una mawasiliano ya kimapenzi ma bosi wangu nakuomba uache mara moja najua umeshawishiwa na fedha zake mke wangu kama umeona sina maana kwako chukua kilicho chako sasahivi uniache nilee wanangu kwa amani bila mashaka wala hofu ya kifo unayo taka kuniletea humu ndani.

Basi mke akaelewa vyema kinacho ongelewa na akamueleza mume wake hali ilivyo kuwa tangu mwanzo hadi walipo fikia na kumuhakikishia mumewe kuwa hato rudia tena kosa kama hilo na wakakubaliana kuwa ili mume asiharibu kazi mke umueleze boss kwamba amefikiria ameona hawezi kumsaliti mume wake na pesa zile azzirudishe kwa kuzirusha kwa njia ya mttandao na akafanya hivyo na ndoa ikabaki salama kabisa lakin boss hakujua kama mwenye mke kazipata taarifa hizo maana walitumia busara ya hali ya juu sana wanandoa hao kulitatua hilo bila kuzalisha tatizo jipya.

Hivyo kuna kaumuhumi kwa kiasi fulani kufuatilia nyendo za mwanandoa mwenzi maana huenda kwa kufanya hivyo kunaweza kukuokoa hata wewe pia kwa sehemu fulani na familia kwa sehemu nyingine

Kupitia pitia simu ya mwanandoa mwenzio kwa kiasi hujenga hofu ya heshima ya ndoa ingawa si kwa asilimia nyingi lakin inasaidia maana wandoa hao watakuwa na hofu kugawa gawa namba kwa mahawala ni tofaauti na uhuru ulio pitiliza kiasi kwamba mume au mke anaweza kupigiwa simu na mahawala zake mkiwa wote hapo hapo pamoja kitu ambacho ni dharau iliyo kithiri kwenye ndoa

Ndoa iliyo imara kabisa na isiyo na mashaka wala aina yeyote ya uhuni na ujanja ujanja hakuna sababu ya kuwa na siri kubwa kwenye simu zenu unless mnafanya magendo.

Ikumbukwe simu imekuwa ndio chanzo cha migogoro kwenye ndoa kwa 75% maana kupitia simu ndipo waweza kufanya mambo mengi maovu maana simu mdio kiunganishi kikuu na cha haraka sana.

Na mtu yeyote anaye ona mke au mume hana mamlaka na simu ya mwenzie hasa wanandoa sio wapenzi, ni dhahiri mume au mke huyo anashiriki katika vitendo viovu mke au mume ndiye mtu wa karibu sana haiingii akilini hawala yako anakuwa na mamlaka ya kushika na kukagua simu yako hadi sms za manung'uniko ya mkeo au mumeo juu yako anayasoma hawala yako halafu mke au mume wako unamuwekea mashart makali ni lazima hapa parekebishwe tusihalalishe uovu kwa sababu tu ya kutetea tamaa za wakati mfupi.

Maana hapa walio wengi wanalikataa hili si kwa sababu za maswala ya kiofisi la hasha 85% wanatetea mambo yao ya sirini tena maovu yasionwe na wanandoa wenzao ndio maana wengi wameshupaza shingo kujifanya haitakiwi kupitia pitia simu ya mwenza wako.

Lakin sasa pamoja na hayo isiwe kutwa kucha upo na simu ya mume au mke wako hiyo itakuwa too much na ni kero pia ingawa kwa ndoa iliyo imara yenye mke/mume mwenye hekima na busara hakuna cha kumficha labda kama ndio wahe au wame hawa wa kuokoteza mitaani wasio na malezi bora.

Lakin ikumbukwe kupitia simu hizi hizi baba mmoja alijua kumbe analea mtoto asiye wake baada ya kufuma sms kwenye simu ya mke wake ambaye anawatoto nae watatu na huyo wa tatu ndiye asiye wake huku mama huyo akiwa anachati na baba halisi wa mtoto na anatumiwa pesa ya matumizi bila mume wake kujua hadi alipo zifuma sms hizo.

SIMU HIZI ZINASAIDIA KWA SEHEMU KUJUA YALIYO JIFICHA AMBAYO KWA SEHEMU YAOKOA JAHAZI.
 
Kkimondoa

Kkimondoa

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2014
Messages
4,473
Likes
4,844
Points
280
Kkimondoa

Kkimondoa

JF-Expert Member
Joined May 31, 2014
4,473 4,844 280
Mods naomba mnirekebishie kichwa cha habari hapo juu sahihi ni FUATILIA na sio DUATILIA.
 
B

Bhampupile

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2015
Messages
814
Likes
626
Points
180
B

Bhampupile

JF-Expert Member
Joined Jul 6, 2015
814 626 180
Sawa mkuu umeeleweka vzr sn .Wengi wametengana na wapendwa wao kwa sbb ya hz simu wameacha watoto wakihangaika kwa kukosa kalezi bora ya mama na baba.
 
M

msafiri2017

Senior Member
Joined
Dec 6, 2016
Messages
128
Likes
94
Points
45
Age
48
M

msafiri2017

Senior Member
Joined Dec 6, 2016
128 94 45
Ni vyema mleta huu uzi,umesema ukweli katika maisha,maana kumbuka mlikua wachumba mlikua hamfichani jambo maana mlipendana kwa dhati sana na ikawa hakuna anaye michael mwenzie lkn mm naomba kuongeza kitu hapo,kabla ya haya mambo yote mtangulize Kwanza MUNGU ndio namba moja hii ni katika kumpata aliye wako wa ukweli,maana bila hivyo mnaweza mkaoana kwasababu ya tamaa ya mwili tuu,na hii ni mbaya kuliko,hapo ndio shida inapoanzia,ni vizuri pia kuwa muwazi sana kwa mweni wako kwasababu kua mwili mmoja sio mchezo sio lele mama,Mtangulizeni Mungu kwanza awape ulinzi na zaidi aongoze akili na mawazo yenu,msiamue,kwa kuitumia akili zenu lah mtaharibu, huyo Baba aliongozwa na Roho wa Mungu kuliwa wazi hilo jambo kwa upole na utashi mkubwa bila ugomvi,inaonyesha jinsi Mungu alivyochukua nafasi katika Ndoa hiyo labda pasina huyo Baba kujua au alimkabidhi Mungu mambo yake kabla ya kuliendea jambo
 
Domhome

Domhome

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2010
Messages
2,212
Likes
1,410
Points
280
Domhome

Domhome

JF-Expert Member
Joined Jun 28, 2010
2,212 1,410 280
Ni jambo la kheri kujua ubaya wa mwenzio ili uishi naye kwa tahadhari au mkarekebisha ili mjenge familia bora kumbuka kuna hatari ya mmoja akalichuma mkala wote nakuwaacha watoto wakiwa yatima, ngoja nitoe mfano hapa.

Lakin sasa pamoja na hayo isiwe kutwa kucha upo na simu ya mume au mke wako hiyo itakuwa too much na ni kero pia ingawa kwa ndoa iliyo imara yenye mke/mume mwenye hekima na busara hakuna cha kumficha labda kama ndio wahe au wame hawa wa kuokoteza mitaani wasio na malezi bora.

Lakin ikumbukwe kupitia simu hizi hizi baba mmoja alijua kumbe analea mtoto asiye wake baada ya kufuma sms kwenye simu ya mke wake ambaye anawatoto nae watatu na huyo wa tatu ndiye asiye wake huku mama huyo akiwa anachati na baba halisi wa mtoto na anatumiwa pesa ya matumizi bila mume wake kujua hadi alipo zifuma sms hizo.

SIMU HIZI ZINASAIDIA KWA SEHEMU KUJUA YALIYO JIFICHA AMBAYO KWA SEHEMU YAOKOA JAHAZI.
...NDO MAANA SULEIMANI ALIPO AMBIWA NA MUNGU AOMBE LOLOTE ATAPEWA, YEYE ALIAMUA KUOMBA "APEWE HEKIMA"......MUNGU AKAAMUA KUMUONGEZEA NA UTAJIRI..
 
Job K

Job K

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2010
Messages
8,286
Likes
4,446
Points
280
Job K

Job K

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2010
8,286 4,446 280
Hii mi mods ya humu nayo unakera sana, imeombwa muda mrefu na mleta mada kwamba imrekebishie heading imebuma tu! imekalia kupiga watu ban tu, hapa ukimtukana kidogo tu Lizaboni utaona itakavyokufurumusha na ban! Wacheni hizo bwana mnakera!!
 
Duduwasha

Duduwasha

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2010
Messages
5,323
Likes
2,467
Points
280
Duduwasha

Duduwasha

JF-Expert Member
Joined Nov 3, 2010
5,323 2,467 280
Mods naomba mnirekebishie kichwa cha habari hapo juu sahihi ni FUATILIA na sio DUATILIA.
duatilia kisa hiki kuhusu simu zetu.Ni jambo la kheri kujua ubaya wa mwenzio ili uishi naye kwa taha
 
Kkimondoa

Kkimondoa

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2014
Messages
4,473
Likes
4,844
Points
280
Kkimondoa

Kkimondoa

JF-Expert Member
Joined May 31, 2014
4,473 4,844 280
duatilia kisa hiki kuhusu simu zetu.Ni jambo la kheri kujua ubaya wa mwenzio ili uishi naye kwa taha
Kuna shida ilijitokeza nadhan katika kupost ika copy mstari wa kwanza sijajua nini shida maana hapo kichwa kilikuwa hivi"FUATILIA KISA HIKI KUHUSU SIMU ZETU" sasa hayo mengine sijui yaliingiaje hapo ambayo yapo kwenye mstari wa kwanza nadhani mods watanisaidia kurekebisha. Ucjali ni matatizo ya hizi smartphones zetu.
 
IMERN

IMERN

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2013
Messages
498
Likes
551
Points
180
IMERN

IMERN

JF-Expert Member
Joined Sep 6, 2013
498 551 180
Ahsante mkuu,.ujumbe mzuri sana huu.
 
M

msafiri2017

Senior Member
Joined
Dec 6, 2016
Messages
128
Likes
94
Points
45
Age
48
M

msafiri2017

Senior Member
Joined Dec 6, 2016
128 94 45
Kuwa Mwaminifu katika Ndoa ni jambo jema sana na hasa ukimshirikisha Mungu akuongoze uishi maisha ya furaha na zaidi sana sio kwa kumpendezesha mtu mwingine zaidi yako wewe Mume/Mke na Mungu tuu!!Tamaa hua zipo lakini Ukiwa Mtiifu kumwachia Mungu Njia zako hakika atakupa njia ya kutokea bila hivyo usifikiri utaweza kwa akili zako.unapokua Mwaminifu kwa kila jambo amani hutawala ndani ya nyumba lkn ukiwa muongo hakika yule mshika ki wako atakua anakutunmia sana.simaanishi kua mwaminifu kwa jambo moja tuu la ndoa,lah,bali bali mwaminifu kwa kila jambo ndani ya nyumba yenu.kwenye ndoa ni jambo moja pana sana na yamkini nikiweka uzi huo hapa nadhani kila mwenye ndoa atachukua mwenzake atakaporejea nyumbani hivyo kuwa tuu Mtiifu na mwaminifu mmoja kwa mwingine UKIMWI au mgonjwa yatakua ni historia kwako
 
M

msafiri2017

Senior Member
Joined
Dec 6, 2016
Messages
128
Likes
94
Points
45
Age
48
M

msafiri2017

Senior Member
Joined Dec 6, 2016
128 94 45
Ulietoa hii mada hebu nenda mbali zaidi nakushauri pia uwe una weka na shuhuda ambazo ni za kweli lkn kwa kutomtaja mtu jina na hata dini yake weka iwe ni kwa manufaa ya wale waliko katika Ndoa na zaidi sana kwa wale wanao subiri kuingia kwenye ndoa
 
Evelyn Salt

Evelyn Salt

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2012
Messages
48,331
Likes
40,113
Points
280
Evelyn Salt

Evelyn Salt

JF-Expert Member
Joined Jan 5, 2012
48,331 40,113 280
Maisha ya sasa ni kuishi kama unaoga nje....
 
Possibles

Possibles

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2011
Messages
1,394
Likes
624
Points
280
Possibles

Possibles

JF-Expert Member
Joined Sep 22, 2011
1,394 624 280
Umenena vyema ingawa ni lazima tutambue kama una mwenza muhuni hakuna namna utamzuia.Ukiikagua simu yake atatafuta namna ya kukukwepa na madhara yatakuja yaleyale. Wakati mwingine MUNGU tu huamua kutulinda.
 
VAN HEIST

VAN HEIST

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2014
Messages
1,437
Likes
154
Points
160
VAN HEIST

VAN HEIST

JF-Expert Member
Joined Aug 26, 2014
1,437 154 160
Huu udukuzi wa simu ya mupenzi ulinitokea puani hadi sasa sitamani hata mupenzi tena
 

Forum statistics

Threads 1,274,855
Members 490,833
Posts 30,526,029