Fuata haya kulinda mahusiano na watu wenye pesa au hadhi zaidi yako

1. Ukitaka kuzoeana na watu wenye pesa zao kamwe USIWAZOWEE

2. Usije kumpigia simu kumsalimia kila baada ya siku kadhaa ikawa ndo desturi yako, acha hiyo atakuwa hapokei simu zako.

Kumbuka thamani ya salamu ni pale tunapowasalimia watu ambao wanaona umuhimu wetu na sio ambao tunaona umuhimu wao"

3. Ukitaka kumtembelea usimpe taarifa kama unaenda, wewe nenda ukimkuta piga stori kama hujamkuta aga ondoka.

4. Ikiwa umemkuta ulipomtembelea chonde chonde chonde usijaribu kukaa muda mwingi; kaa muda mchache zaidi ujifanye una haraka ulipita mara moja tu.

Usije ukala chakula baada ya kwenda ghafla, labda iwe walikualika

Kumbuka "kuwatembelea matajiri ni kama kuwatembelea wagonjwa" kwa maana hawataki usumbufu

5. Kama kakuita kwa shida fulani nyumbani kwake hakikisha unaifanya kwa ucheshi na bashasha na kuipenda kazi hiyo lakini ukimaliza usikae tena ondoka hapo.

6. Ukitaka matajiri wakuheshimu basi jifanye huna muda nao.

7. Hakikisha kabla ya kuonana nae uwe na mambo ya msingi ya kuongea nae, sio unaonana nae mara mnakaa kimya alafu wewe ndo umemfuata na hajakuita, unampotezea muda wake.

8. Usije kumlalamikia shida yoyote ile hata kama huna nia ya kumuomba,kwa maana usilalamikie chochote mbele yake yeye atahisi unamuomba kijanja atakuona mzushi hufai kuwa karibu nae.

acha yeye ndo ajue shida yako kupitia yeye mwenyewe kuona au asimuliwe na wengine kwamba wewe una shida.

Kulalamika shida mbele ya tajiri ni mwiko!

9. Usiwe unakubali vipesa anavyokupa kwa kumsaidia kazi ambazo hazina utaalamu kama vile kusukuma gari,kumsaidia kuingiza mzigo ndani n.k

Akikupa chochote mwambie usijali mkuu kawaida tu kusaidiana sisi wanadamu.

Hapo kiakili ataona na yeye ana deni la kukusaidia wewe kwa wema unaomfanyia hivyo inaweza kumpa fikra akupe mchongo fulani wa pesa na mambo mengine.

Ataona kwamba mali sio ishu kubwa kwako na kumbuka matajiri hawapendi watu wanaopenda mali zao,wanapenda watu wasiojali mali zao matajiri.

10. Usimhoji kabisa kuhusu mali zake kazipata vipi ili na wewe upite njia hizo, usimhoji usimhoji usimhoji!

Kufanya kinyume na haya ni kutaka kuonekana msumbufu na atakuepuka alafu utapoteza malengo yako kama ulitaka kupata connection ama msaada wake.
Uzi mzr ila mm siwez kwa kwel
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom