Fuata haya kulinda mahusiano na watu wenye pesa au hadhi zaidi yako

1. Ukitaka kuzoeana na watu wenye pesa zao kamwe usiwazowee.

2.usije kumpigia simu kumsalimia kila baada ya siku kadhaa ikawa ndo desturi yako,acha hiyo atakuwa hapokei simu zako.

Kumbuka thamani ya salamu ni pale tunapowasalimia watu ambao wanaona umuhimu wetu na sio ambao tunaona umuhimu wao"

3.ukitaka kumtembelea usimpe taarifa kama unaenda,wewe nenda ukimkuta piga stori kama hujamkuta aga ondoka.

4.ikiwa umemkuta ulipomtembelea chonde chonde chonde usijaribu kukaa muda mwingi kaa muda mchache zaidi ujifanye una haraka ulipita mara moja tu.

Usije ukala chakula baada ya kuenda ghafla,labda iwe walikualika

Kumbuka "kuwatembelea matajiri ni kama kuwatembelea wagonjwa" kwa maana hawataki usumbufu

5.kama kakuita kwa shida fulani nyumbani kwake hakikisha unaifanya kwa ucheshi na bashasha na kuipenda kazi hiyo lakini ukimaliza usikae tena ondoka hapo.


6.ukitaka matajiri wakuheshimu basi jifanye huna muda nao.


7.hakikisha kabla ya kuonana nae uwe na mambo ya msingi ya kuongea nae.sio unaonana nae mara mnakaa kimya alafu wewe ndo umemfuata na hajakuita,unampotezea muda wake.


8. Usije kumlalamikia shida yoyote ile hata kama huna nia ya kumuomba,acha yeye ndo ajue shida yako kupitia yeye mwenyewe kuona au asimuliwe.

Kulalamika shida mbele ya tajiri mwiko !!


9. Usiwe unakubali vipesa anavyokupa kwa kumsaidia kazi ambazo hazina utaalamu kama vile kusukuma gari,kumsaidia kuingiza mzigo ndani n.k

Akikupa chochote mwambie usijali mkuu kawaida tu kusaidiana.

Ataona kwamba mali sio ishu kubwa kwako na kumbuka matajiri hawapendi watu wanaopenda mali zao,wanapenda watu wasiojali mali zao matajiri.


10.usimhoji kabisa kuhusu mali zake kazipata vipi ili na wewe upite njia hizo,usimhoji usimhoji usimhoji !!.


Kufanya kinyume na haya ni kutaka kuonekana msumbufu na atakuepuka alafu utapoteza malengo yako kama ulitaka kupata connection ama msaada wake.
Si bora tu nikae na umaskini wangu kama Bill Lugano kuliko kujitesa na hayo yote
 
Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana.
Hahaha mkuu zamani ndo palikuwa na watu wabishi kweli kweli.

We imagine mtu anajiita Mungu alafu anakomaa kabisa.

Unamuambia kuna Mungu anasema sawa yupo ila mimi ndio Mungu kubwa lao.

Zamani watu walikuwa wabishi haswa
 
11. Tajiri hana urafiki na maskini, ukipata chance ya kupiga mpige kiswasawa ukaanze mbele! Ukisubiri huruma utasubiri sana, narudia tena utasubiri sana!
Matajiri wenye huruma walipotea miaka 10 iliyopita!
Teknolojia imekuja na matajili wenye roho mbaya tupu
chuki na matajiri kumbuka ukimpiga unaenda kuwa tajiri wewe unahitaji matajiri wenzako km team, kusali pamoja, kuishi pamoja, sherehe pamoja sasa ukiwapiga utaungana na Maskini? nao watakupiga sababu dawa ya moto ni moto!!

utazunguka weeeeeeeeee
 
chuki na matajiri kumbuka ukimpiga unaenda kuwa tajiri wewe unahitaji matajiri wenzako km team, kusali pamoja, kuishi pamoja, sherehe pamoja sasa ukiwapiga utaungana na Maskini? nao watakupiga sababu dawa ya moto ni moto!!

utazunguka weeeeeeeeee
Hahahahhahahahhha
 
Generally,huwa napenda kumind business zangu,uwe tajiri uwe maskini kama unajidai mimi itaishia salamu tu na ukinizingua nakuchana!
Najishusha sana kwa yoyote anayeona thamani yangu na si vinginevyo!
Nafanya hivi kuepusha maumivu ya moyo yasiyo ya lazima bila hivi kuna watu wanaweza kukusababishia kifo kwa unneccessary frustrations!
 
Jamaa kuna mambo hapo ameongea hadi ya maisha nje ya Title yake, kwa mfano swala la salamu, nimejifunza kitu hapo. Ukiwa unamtafuta mtu kila siku kumsalimia anakudharau
Unajua mkuu kiukweli hasa kutembeleana kila siku sio mapenzi ni kuchoshana.
 
Hahahahhahahahhha
Yaani hawa watu wa hivi!! ndo wanaishiaga kufilisikia kwa waganga wa kienyeji!! wanaishi kimagutu magutu sana!! hawata tulia kamwe!! atamuhisi hata mwanae/ mkewe/nduguye anataka kumpiga pesa!! hajui kuwa ....

chanzo ni kuleee alipo piga kwa tajiri innocent!!! Nenda omba msamaha na lipa zaidi ya mara mbili ya ulichopiga ili uwe salama haijalishi km ukipata hela au laaa!! suala ni rudi uwe salama!!!! ajabu sasa unaiba mwenzako ndo anaagiza Semi trailer kumi!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom