Fuata Hatua Hizi Kumpata Mfadhili kwa Ajili ya Utekelezaji wa Mradi (Prospect Research)

Feb 5, 2022
31
48
1662898230995.png

Utafutaji wa wafadhili kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi (Prospects Research) ni hatua muhimu katika utekelezaji wa Mpango wa Utafutaji Rasilimali Fedha kwa Taasisi (Implementation of Fundraising Plan/Strategy). Taarifa za wafadhili kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi ni muhimu kwa sababu huipa Taasisi uwanda mpana juu ya ufadhili wa miradi yake.
Kadiri miaka inavyozidi kwenda, na utokeaji wa mabadiliko mbalimbali katika nyanza za ufadhili wa Miradi, mchakato wa Utafutaji wa Wafadhili (Prospects Research) umekuwa ukibadilika pia, lakini; msingi wake umebaki kuwa vile vile. Hivyo basi ili ufanikiwe kupata mfadhili wa kufadhili mradi wako, zingatia misingi ifuatayo;
  • Uhusiano/muunganiko (linkage). Msingi wa kwanza katika mchakato wa utafutaji wa Wafadhili ni kuhakikisha kunakuwa na mahusiano kati ya Taasisi na mfadhili mlengwa. Mahusiano yaweza kuwa katika sura hii; Mkurugenzi au Mjumbe wa Bodi au Afisa ndani ya Taasisi husika anafahamiana na Mfadhili (ikiwa mfadhili ni mtu mmoja na si Taaisisi) au anafahamiana na Mtendaji wa Taasisi yenye kutoa ufadhili.
  • Uwezo (ability). Msingi wa pili, ni kuhakikisha kwamba mfadhili unayemtafuta kwa ajili ya kufadhili mradi wako ana uwezo wa kutoa kiasi cha fedha au msaada unaohitaji. Kwa mfano huwezi ukapeleka andiko la Mradi wenye thamani ya Shilngi 100,000,000 kwa mfadhili ambae mara zote hutoa kiasi kati ya Shilingi 5,000,000 mpaka 10,000,000.
  • Interest, nimekosa neno sahihi kwa lugha ya kiswahili, (huu ni msingi wa tatu) ila ninachomaanisha hapa ni kwamba, wakati wa utafutaji wa mfadhili, hakikisha mfadhili husika ana "interest" na kile ambacho Taasisi yako inafanya. Hapa tunazungumzia imani ya mfadhili juu ya dhima ya Taasisi yako (mission), imani ya mfadhili juu ya dira ya Taasisi yako (vision) pia imani ya mfadhili juu ya tamaduni za Taasisi yako (organization culture & values)
Kifupi hii misingi hujulikana kama "LAI" yaani Linkage, Ability & Interest. Hivyo wakati wowote utafutapo wafadhili izingatie.

HATUA ZA KUFUATA KATIKA UTAFUTAJI WA MFADHILI
  • Kumtambua Mfadhili (Prospect Identification). Katika hatua hii unapaswa kuzingatia misingi yote mitatu niliyoainisha hapo juu, yaani "linkage, Ability & Interest". Katika zoezi la kuwatambua wafadhili, hakikisha unawaweka kwa makundi; kwa mfano kundi la wafadhili wakubwa (Major Gift Donors), hawa wapewe kipaumbele SANA, wafadhili wadogo/ wa kati (Minor Gift Donors) hawa wanaweza kuwa wajumbe wa bodi ya Taasisi yako n.k. Matokeo ya mchakato wote huu huleta kitu kinachoitwa DONOR PROFILE, bahati mbaya sana kwa Asasi nyingi za kITanzania hiki ni kitu kigeni.
  • Anza mawasiliano na Mfadhili husika(developing engagement) hatua hii itafuatwa endapo umemlenga mfadhili ambae hutoa fedha pasina kutoa wito wa uwasilishaji wa maombi ya fedha . JAPOKUWA, hata kama anatoa wito (Call for Proposals) kufanya ushawishi "lobbying" kwa kuanzisha mawasiliano nae ni muhimu sana, hi tunaitia "doing pre-proposal marketing"
  • Ushawishi kwa Mfadhili (Donor's Cultivation) Katika hatua hii ushawishi hufanyika katika namna tatu (1) Kumshawishi mfadhili alie kufadhili kiasi kidogo kipindi cha nyuma, aongeze kiasi (2) Kumshawishi mfadhili aliekufadhili kiasi kikubwa aendelee na kiasi hicho pasina kukipunguza kiasi (3) Kumshawishi mfadhili ambae hakuwahi kukufadhili hapo nyuma, akufadhili sasa
  • Uombaji wa fedha (solicitation) baada ya kuwa umemshawishi mfadhili, ni wakati sasa wa kumuomba fedha kwa utaratibu maalum ambao atakupatia.
  • Shukurani. Baada ya kupata fedha na kukamilisha shughuli za mradi ni, hatua sasa ya kumshukuru mfadhili na kumuonyesha ni jinsi gani ufadhili wake umeleta mabadilko kwenye jamii unayoihudumia.
AHSANTE

OMAR MSONGA (BA. PPM)
CONSULTANT
Project Management, Strategy, Fundraising & Training
Call: +255 719 518 367
Email: omarmsoga8@gmail.com
DAR ES SALAAM
TANZANIA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom