FT: Ligi Kuu: Geita Gold 0-5 Simba / Uwanja wa CCM Kirumba - Mwanza / 18-12-2022

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Mchezo umemalizika

Kibu Denis anaipatia Simba goli la tano akimalizia pasi ya Chama
GOOOOOOOOOOOOOOOOO
85' Simba inataka kufanya mabadiliko ya wachezaji watatu kwa mpigo
Sakho anapiga shuti la mbali nje ya eneo la 18, anafunga baada ya kipa kutoka eneo lake
75' GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
74' Geita wanatengeneza mashambulizi licha ya kuwa nyuma lakini wanakosa umakini
68' Kanoute ametoka, anaingia Akpan, mabadiliko kwa Simba
58’ Luizio anapiga shuti kali linagonga nguzo na kurejea uwanjani
57’ Geita ni kama wamerudi nyuma kuanza kujipanga
50’ Simba wamemiliki mchezo
Sakho anaipatia Simba bao la tatu kwa shuti kali
47' GOOOOOOOOOOOOOOOO
Kipindi cha pili kimeanza

Half Time

45' Mapumziko, Simba inaongoza 2-0
Beki wa Geita, Kelvin Yondani hajaamini macho yake
Chama anaipatia Simba bao la pili baada ya gonga nzuri ya wachezaji wa Simba
40' GOOOOOOOOOOOOOOOO
37’ Timu zote zinapeana zamu kumiliki mpira
35’ Simba wanajibu mapigo kwa kutengeneza mashambulizi lakini walinzi walinzi
27’ Geita wameichukua mchezo, wanamiliki mpira na kupanga mashambulizi
22' Simba wanajipanga kwa kupiga pasi nyingi lakini Geita wanakuwa makini katika kuwapa presha
20' Geita wanaongeza umakini wanapokuwa na mpira
John Bocco anafunga kwa kichwa, akimalizia krosi ya Shomari Kapombe
11' GOOOOOOOOOOOOOO!!!
8' Kasi ya mchezo inaongezeka taratibu
4' Ndani ya muda mfupi wachezaji wamekataa mipira mitatu ikionekana kukosa ubora
2' Bado mchezo una kasi ndogo
Mchezo umeanza, idadi ya mashabiki ni wengi lakini bado Uwanja haujajaa. Huu ni uwanja ambao Geita wanaitumia katika mechi zao za nyumbani wanapocheza na Simba na Yanga.

FkQjnp5XEAA1g-k.jpg

Kikosi cha Simba kinachoanza

Kikosi cha Simba kipo uwanjani leo kuivaa Geita Gold kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, mchezo unapigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza katika mitaa ya Kirumba
 
Back
Top Bottom